Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Uganda ni majirani zetu na wametangaza Eid ni kesho; lakini pia Uarabuni Napo Eid ni kesho.

Kwanini Tanzania wamepanga iwe jumamosi?
Funga kwanza ndo ulalamike. Unacheua kitimoto kwa shibe afu unaulizia mambo ya mfungo? Usiingilie utaratibu wa watu.
 
Haya mambo ya mitandao siku hizi kila mtu anajifanya mtaalamu, hizi tofauti hazijaanza juzi wala jana.
 
Muft kasema amewasiliana na kenya ameambiwa hawajauona mwezi ila kenya wametangaza kuuona sjui kawasiliana na kenya ipi!!

Poleni na huu mzimu wa bakuata mtaendelea kuachwaa
Ila sio lazima kufuata Bakwata, wapo wasiofuata Bakwata hapa Tanzania.
 
Mkuu Dr Matola PhD mambo ya waislamu ungewaachia tu wenyewe mkuu maana kila mtu anajua anachokifanya.

Kwa kukuhabarisha kuna misimamo ya aina mbili na yote ni sawa, kuna msimamo wa kufunga na kufungua kwa mwandamo wa mwezi wa kitaifa na hili halina ubaya.

Na pili kuna msimamo wa kufunga na kufungua kwa mwezi wa kimataifa yaani unaoandama popote na hili halina ubaya.

Bakwata wameamua kushikilia msimamo wa mwezi wa kitaifa na waumini wana uhuru wa kuwafuata au kuswali kesho, kuna ubaya gani? hapa kuna utapeli upi? sisi wengine tunaswali kesho na tuko huru kufanya hivyo.

Nashauri wakati mwingine ungeachana na haya mambo maana ni comments zako nyingi unazungumzia utapeli n.k shika kile unachokiona ni sawa na mambo ya waislamu waachie wenyewe.

Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…