Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Your browser is not able to display this video.
 
Ila mnamatatizo nyie watu, kabla ya kuwepo kwa simu na internet mlikuwa mnajuaje mambo ya mwezi kuonekana Kenya ili mjue kwamba ni Eid
Watu wanasema mambo ambayo hawayaelewi. Uislamu ni dini ya kanuni na kanuni zake ni kitabu Qur'an na Sunna yaani mwenendo wa mtume. Hakuna kufuata nchi hata kama ni saudia. Ikiwa wanachokifanya ni tofauti na kitabu na sunna basi tunafuata kanuni sio nchi.
 
Kwahiyo hizo nchi nyingine za Sunni nao hawali Iddy kesho?
Suni wao hula Eid el Fitr siku moja kabla, hali kadhalika huanza kufunga mfungo wa Ramadhani siku moja kabla ya hao wengine.
 
Umesoma Maelezo wanakula eid kulingana na muonekano wa mwezi
Katika uislam suala la mwezi mwandamo lina hitilafu. Wanazuoni wanatofautiana rai katika kutafsiri mwezi muandamo. Wapo wanaosema ukionekana popote duniani kwa sababu ya utandawazi na mawasiliano basi imetihibiti wanauita mwezi wa kimataifa. Na wapo wanaosema sunna ni kuona wenyewe katika mamlaka ya eneo lenu.
Kwa taarifa yako hata hao Saudia hawafuati mwezi wa kuonekana popote
 
Umesoma Maelezo wanakula eid kulingana na muonekano wa mwezi
Na hiyo hitilafu inaanzia katika kutafsiri neno la kiarabu "suumu li ru'uuyatihi..." kuna wanaotafsiri kuwa ni " fungeni kwa kuonekana ..." na kuna wanaotafsiri kuwa ni "... fungeni kwa kuuona.."
Hapa wataalamu wabobevu a lugha wanafunua vitabu lukuki hoja na dalili.. kiasi kwamba msikilizaji kama sio alimu unaishia kuchanganyikiwa....
Mantiki rahisi kabisa ni kufuata mtume alifanyaje basi. Na ukifanya hivyo utaona ni sahihi kila nchi na mwandamo wake..
Na mwandamo ulizingatia uwepo vizjizi vya kutoweza kuuona mwezi basi hapo mnahesabu ikifika siku 30. Mmekamilisha. Allahu atuongoze katika njia sahihi..
 
 
Allah akulipe kheri ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…