Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Huu ni unafiki mwingine wa wanasiasa, kwamba katika mambo mengi sana ya shughuli za kiserikali na kisiasa nchini, mnawaalika viongozi wa dini na kutaka wawabariki katika mamlaka yenu nk. Kila wakati tunawaona kina Makonda wakiomba waombewe na viongozi wa dini mara nyingine kwa magoti na machozi, ili watumikie nyadhifa zao kwa busara na hekima.
Halafu mnafurahia sana wanapowasifia, hasa wanaposema nafasi zenu ni chaguo la mungu. Hatusikii hata siku moja mkikanusha haya. Kama mnakubali nyie ni chaguo la mungu kama wanavyosema, basi kubalini ushauri mnaopewa na wale waanaoonwa na jamii kuwa ni watumishi wa mungu.
Sasa iweje pale ambapo wanapowakosoa au kuwashauri juu ya mambo ambayo hamfurahii ndio mnakumbuka kusema wasiingilie mambo ya siasa au utawala?
Mtu mwenye kukuongoza katika kutumia hicho kitabu unachoshika ukiapa unaanza kumfokea na kusema asikuingilie sijui nini. Basi shikeni vitabu vya hadithi za Abunuwasi wakati wa kuapa ili viongozi wa dini wasiwabugudhi kwa kuwashauri, muendelee kuwadanganya watu na hadithi za Abunuwasi bila shida
Acheni unafiki jamani. Kama hamtaki viongozi wa dini kutoa maoni juu ya uongozi wa nchi basi na nyie acheni kuwahusisha na mambo yenu ya uongozi, kutia ndani sherehe za kuapishwa na nyingine za kiserikali.