Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Kama Serikali inashindwa kuendeleza miradi midogo kabisa ya Mabasi ya mwendokasi. Je, hiyo treni na ndege wataweza kweli?

Serikali uajili kwa vyeti. Sio uwezo nA UBUNIFU. Haina uwezo wa kuongeza tija. Unaweza ukaws mbunifu ukaongeza mapato ya kampuni lkn mshahara unabak vile vile
"UBUNIFU" ni kitu gani? Ni 'preserve' ya kundi maalum wasioweza kuwa katika jamii serikali inakowapata waajiriwa wake? Hii dhana uliipata wapi?
Sasa wewe unadhani hilo tatizo la kuongeza mshahara ndiyo iwe sababu ya serikali kutofanya vizuri katika mashirika yake? Serikali haiwezi kuliondoa tatizo hilo, kama kweli inaona ndilo linalozuia?
Kwa nini ndiyo iwe sababu ya serikali kutoweza kufanikisha kazi zake katika mashirika?

Hujatoa sababu hata moja, ya kueleza kwa nini serikali isifanye biashara na kufanikiwa. Haya unayorudiarudia ni mambo ya kukaririshwa tu basi.
 
hoja dhaifu. unajua kuwa profesa anayefundisha chuo kikuu ukimpa kufundisha darasa la kwanza litamshinda?
 
hoja dhaifu. unajua kuwa profesa anayefundisha chuo kikuu ukimpa kufundisha darasa la kwanza litamshinda?
Eeeenhee Heee, eti ee bhwana!

Sijapata kulipa fikra za namna hii hili jambo!

Kwanza Profesa kule kulituliza tu lile darasa liwe na utulivu ili aanze kazi ya kufundisha tu itakuwa ni kazi ngumu kwake!

Lakini, si atajifunza, siku mbili, wiki, na baada ya hapo mambo yanaendelea?

Kwa nini isiwe hivyo hivyo na serikali na mashirika yake!
 
Siyo lazima tuishi kama wachina, lakini tunaweza kutumia baadhi ya njia zao zinazofanikisha katika mazingira yetu. Kwa nini tuishi kama wao; kwani sisi hatuna akili za kufikiri na kupanga mambo tunayoona yanafaa?

Una maana unamwona mchina bora kuliko ulivyo wewe, hadi upende kuishi maisha yake?

Serikali zote dunia hutoa huduma, sio China pekee...

Hata hivyo, unaangalia tu huduma za mwendo kasi hapo, kwani huduma zinapotolewa hazipashwi kufanywa ili ziwe huduma bora?

Sikubaliani na wewe juu ya serikali ya china kutofanya biashara. Mashirika yote yaliyotapakaa duniani kote yanayojenga kila aina ya miundo mbinu yanatoa huduma?
TTCL hapa kwetu haiwezi kufanya biashara, kwa nini?
Sijasema wachina ni bora kuliko sisi, nilicho maanisha ni kwamba aina ya uongozi wao unatokana pia na utamaduni wao ambao umeathiriwa na historia yao.
Lakini wote tunajua namna uongozi bora unavyokuwa, ni vile tu huwa tunajiingiza kwenye ushabiki na pia ubinafsi unatuandama.

Dhana ya serikali kujiondoa kwenye biashara naamini ni kwasababu ya kukosa wasimamizi ambao watakuwa na uchungu na hizo biashara( kwani mtu anajua atakapostaafu hiyo si biashara yake tena na hivyo kufanya kikawaida tu ili mradi mshahara unaingia).

Kwanini serikali itoe huduma?(mwendo kasi ni mfano tu wa huduma mbalimbali) ,,- Serikali ina wajibu wa kuhudumia raia wake.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Biashara ipi na kwa mfano upi dhahili?
Mashirika yote yanayoendeshwa na selikali kwa 100% uendeshwa kwa hasara, hutegemea ruzuku tu kujiendesha na hayana UBUNIFU na mshindani. Mfano NI Tanesco, Posta, TLA,
Using'ang'anize hoja zisizo na uhalisia
Bro hebu fikiria ,umelisimamia shirika kwa nguvu zako zote hata limekuwa kubwa halafu unastaafu,, ukistaafu lile shirika halikuhusu tena kwa lolote.
Kwa hali kama hiyo huwezi pata mtu wa kusimamia biashara za serikali kwa moyo wake wote.
Hivyo serikali isitegemee kupata faida kwenye biashara inazoziendesha.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini serikali haitaki mashirika binafsi kutoa huduma ya moja kwa moja ya umeme kwa watumiaji wa mwisho?
Kwa nini inataka isambaze umeme yenyewe tu?
Kwa nini haitaki ushindani na makampuni binafsi kwenye hiyo sekta?
Kwa nini imeamua kuwa monopoly wa kulazimisha wa umeme?
Kwa nini kwa mfano, Tanesco iwe biashara ya hasara, hebu nieleze wewe? Na kwa nini hiyo biashara inatakiwa ifanywe na shirika binafsi ndipo liwe na faida, kwa nini?
Hapa ndipo ninapotaka ufafanue kwa nini iwe hivyo.

Usiseme tu kwa kuwa ni serikali haiwezi kufanya biashara, hiyo siyo sababu.

Ndio, kuna aina za biashara/huduma zinazohitaji kupewa ruzuku, lakini si zote.
 
Dhana ya serikali kujiondoa kwenye biashara naamini ni kwasababu ya kukosa wasimamizi ambao watakuwa na uchungu na hizo biashara( kwani mtu anajua atakapostaafu hiyo si biashara yake tena na hivyo kufanya kikawaida tu ili mradi mshahara unaingia).
Bado hatuelewani.

Hakuna sababu hata moja inayoeleza kwamba serikali haiwezi kuendesha mashirika yake mengi kwa faida. Siioni sababu hata moja.

Hata yale yatakayolazimu kupewa ruzuku ni kuongezea tu ili kufanikisha huduma ziendelee kuwa nzuri, na siyo serikali itoe hela zote kama ndio shirika limeanza kufanya kazi.
Bro hebu fikiria ,umelisimamia shirika kwa nguvu zako zote hata limekuwa kubwa halafu unastaafu,, ukistaafu lile shirika halikuhusu tena kwa lolote.
Kwa hali kama hiyo huwezi pata mtu wa kusimamia biashara za serikali kwa moyo wake wote.
Hivyo serikali isitegemee kupata faida kwenye biashara inazoziendesha.
Hebu ona sababu kama hii mkuu, hivi kweli uko 'serious' na haya unayochangia hapa?

Kwa sababu tu mtu anajua atastaafu, kwa hiyo asitimize wajibu wake kazini?

Kwa vile Rais anajua ngwe yake inakwisha baada ya miaka mitano au kumi, kwa hiyo aboronge tu?

Kwa maana hiyo, hata mfanyabiashara anajua atakufa tu baada ya miaka kadhaa, ya nini ahangaike na kuiboresha biashara yake?
 
Kwa nini serikali haitaki mashirika binafsi kutoa huduma ya moja kwa moja ya umeme kwa watumiaji wa mwisho?
Kwa nini inataka isambaze umeme yenyewe tu?
Kwa nini haitaki ushindani na makampuni binafsi kwenye hiyo sekta?
Kwa nini imeamua kuwa monopoly wa kulazimisha wa umeme?
Mkuu 'Yoda', umeuliza maswali ambayo mimi sina majibu yake; na kusema kweli, hayo maswali hayajibu hoja inayojadiliwa hapa kwamba "Serikali haiwezi kufanya biashara kwa ufanisi."
Hii ndiyo ninayoijadili mimi.
 
Bro hebu fikiria ,umelisimamia shirika kwa nguvu zako zote hata limekuwa kubwa halafu unastaafu,, ukistaafu lile shirika halikuhusu tena kwa lolote.
Kwa hali kama hiyo huwezi pata mtu wa kusimamia biashara za serikali kwa moyo wake wote.
Hivyo serikali isitegemee kupata faida kwenye biashara inazoziendesha.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Sio isitegemee faida Bali iache kabisa kufanya biashara imudu kusimAmia huduma Muhimu za kijamii na kuikusanya kodi
 
Robert Kisena achiwe aendeshe kampuni yake, aliwekwa ndani kwa hila tu za marehemu. Yaani marehemu alikuwa na roho mbaya sana.
Kisena hajawahi kuendesha hata mradi wa mikokoteni Leo hii aendeshe mradi wa mabasi 140?
 
Eeeenhee Heee, eti ee bhwana!

Sijapata kulipa fikra za namna hii hili jambo!

Kwanza Profesa kule kulituliza tu lile darasa liwe na utulivu ili aanze kazi ya kufundisha tu itakuwa ni kazi ngumu kwake!

Lakini, si atajifunza, siku mbili, wiki, na baada ya hapo mambo yanaendelea?

Kwa nini isiwe hivyo hivyo na serikali na mashirika yake!
Sio shirika tu kila kinachofanywa na serikali hakifanywi kwa ufanisi. Sema sekta nyingine zipo kihuduma tu. Ulizia shule au hospital Kuna shida Sana. Zaidi ya nusu NI huduma duni tu.
Kwa vitu tunavyotegemea kutengeneza faida lazma kubadili na kudili vizuri na mfumo wa usimamizi
 
Mkuu, ahsante kwa mchango wako, lakini dhana hii ni potofu kabisa.

Kwa nini watu wote hao walioko serikalini wote wawe hawana ubunifu, ila hawa wengine ndiko kuwe na wabunifu?

Umetoa mfano huo wa TTCL, ukalinganisha na TIGO, VODA na HALOTEL - hivi kweli unaweza kusema kwamba wafanyakazi walioko TTCL hawana ubunifu kama hao walioko kwenye mashirika hayo? Ushahidi wa hili ni upi?

Serikali wangetaka mashirika yao yafanye vizuri ingewezekana sana!

Basi tu, hatujapata viongozi ambao wana nia ya kuyafanya haya mashirika yawe imara. Ni mambo ya uzembe tu na kukosa usimamizi unaotakiwa kuyawezesha mashirika yafanye kazi vizuri.
Kwanza mtu kuwaza kuajiliwa na Serikali NI upungufu wa UBUNIFU, uoga wa kuthubutu. Hivyo watu Hawa hawawezi kuleta tija
 
Kwanza mtu kuwaza kuajiliwa na Serikali NI upungufu wa UBUNIFU, uoga wa kuthubutu. Hivyo watu Hawa hawawezi kuleta tija
Uongo unaoonyesha huna shule.

Ninaweza kusema wewe ni aina ya watu wanaotafuta majibu mepesimepesi kwa jambo ambalo hawana ujuzi nalo. Ili nisionekane ninakuonea, sisemi ni wewe pekee mwenye tabia hizi, ni wengi, na hasa wale waliomo kwenye ngazi za uongozi wa taifa letu.

Badala ya kutumia muda na akili kutafuta ufumbuzi wa matatizo, kama hilo la wafanya kazi kutofanya kazi ipasavyo huko serikalini, wanarukia tu visababu, kama hiki chako ulichotoa hapa.

Na sio ajabu, nawe ukajihesabu kuwa katika hiyo sekta binafsi, na mawazo/majibu ya aina hii! Unatofauti gani na hao walioko TTCL!
 
Sio shirika tu kila kinachofanywa na serikali hakifanywi kwa ufanisi. Sema sekta nyingine zipo kihuduma tu. Ulizia shule au hospital Kuna shida Sana. Zaidi ya nusu NI huduma duni tu.
Kwa vitu tunavyotegemea kutengeneza faida lazma kubadili na kudili vizuri na mfumo wa usimamizi
Haijalishi.
Liwe ni shirika la kutoa huduma au kupata faida, yote yanatakiwa yafanye kazi zao kwa ufanisi mkubwa. Jibu ambalo hutaki kuliandika au hulijui, ni kwa nini iwe hivyo!

Achana na hili la "ubunifu" uliloweka hapo chini. Hiyo siyo sababu hata kidogo.
 
Kwenye maendeleo yoyote na mafanikio yoyote kinachotangulia NI UBUNIFU. Wanaofanikiwa wote au kufanya vitu vizuri huja na kubuni vitu vipya au kuboresha Sana vilivyopo. Utumishi na Kazi za umma ufungwa na Sheria ngumu ili kuzilinda zisiibiwe. Kinachofata watumishi huumiza kichwa na kubuni mbinu za kuiibia kampuni na sio kuiboresha.

Ata waendeshaji na umiliki wa shirika la ndege la Uingereza NI watu binafsi. Lazma tukubali tu uhalisia huo.

Bill gets, Alloyn Musk, Jack Na na mabilioneo wote duniani wamefanikiwa kwasababu wanaongoza kampuni zao. Ila zingekuwa NI za Serikali Mambo mengi wasingekubali kufanya.

Kampuni za umma haziwezi kurisk hivyo kufanya Mambo kwa namna iliyofanyika awali na kusibitika inafaa hivyo kukosa kutanguliza mbinu mpya za kuvutia soko.
 
Huu ni utopolo mkuu!

Hauelezi chochote juu ya mashirika ya umma kutofanya shughuli zao kwa ufanisi.

Na usidhani sielewi maana na mchango wa "Ubunifu"; lakini hakuna lolote uliloeleza hapa linalojibu hoja iliyopo.
 
Serikali haiwezi kufanya biashara. Hasa hizi za kwetu.

Kama Waziri Mkuu anaona madudu kwenye mradi wa mwendokasi.

Kama Serikali imeshindwa kufanya miradi ya reli ya Kati na TAZARA, vivuko, ndege na sasa Mabasi ya mwendokasi kujiendesha ni wakati wa kubadili mtazamo.

Wajiondoe waruhusu sekta binafsi iviendeshe yenyewe ichukue Kodi na idili na kutoa huduma kwa wananchi.
Ngoja tusubiri CCM ina Watu Makini sana ATCL inaingiza FAIDA KUBWA SANA
 
Labda nikueleweshe kiufupi tu!

Sio kwamba serikalini hakuna watu wenye ubunifu, ila hakuna mazingira yanayohamasisha waajiriwa kuwa wabunifu kila kitu mpaka bodi ya wakurugenzi ikae na maazimio ya kikao lazima yapelekwe kwa waziri ili yapatiwe solution

Wakati huo huo huko voda na tigo wamepewa uhuru wa kufanya jambo lolote ilimradi lina faida kwa taasisi

TTCL wakitaka wafanikiwe walitoe shirika kwenye rada za wanasiasa liwe linajitegemea kwa kila kitu.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Uoongozi wa kibiashara ni sawa na soka tu. Kwanza kipaji baadae ndio elimu. Tunawatu wenye elimu serikalini lakini sio wafanya biashara.

Leo akina mbawala wanaliona hilo
 
Back
Top Bottom