Imani ya dini ni tofauti na imani ya itikadi ya vyama vya siasa ingawa zinaweza kufanana kwenye maeneo fulani, ila kwa ujumla,
Imani ya dini inahusu masuala ya kiroho, uhusiano wa mwanadamu na Mungu wake, imani kwa Mungu, wakati imani ya itikadi za kisiasa inahusu namna jamii inavyopaswa kuongozwa, imani kwa mtawala/kiongozi, imani kwa mamlaka za duniani.
Mnaweza kumkamata Lissu wafuasi wake wakakaa kimya kwa hofu ya kuumizwa kimwili, lakini ukimkamata Fr. Kitima unagusa mambo ya kiroho, waumini wake wataumia kimwili na kiroho pia, hawatakaa kimya, kuna dini zingine waumini wao hudiriki kujitoa mhanga kutetea imani.
Kwahiyo kama serikali imepanga kuwakamata baadhi ya viongozi wa dini kwa sababu yeyote ile, ijiulize mara mbili kabla ya kutekeleza adhima hiyo.
Serikali icheze na vyote icheze na wanasiasa lakini isicheze na imani za dini na viongozi wake, mtaichoma nchi moto mchana kweupe.