Kama Serikali ya CCM imechoka kukaa madarakani ithubutu kuwakamata viongozi wa dini

Wewe utakuwa huwajui waTanzania. Hao viongozi wanaweza kukamatwa na maisha yakaendelea tu bila Shida yoyote. Ngoja nikupe mifano 2:
1. Kuna wakati TANESCO Walikuwa wanajenga lakini kubwa ya Umeme kutoka Ubungo kuelekea Mwenge kupitia jirani na Kanisa la Kakobe. Kakobe akahamasisha waumini wake wakae pale nje na wawazuie TANESCO kupitisha Umeme mbele ya Kanisa. Waumini wakatii na kufanya hivyo. Serikali ikaleta FFU kuwashughulikia , Umeme ukapitishwa na hao waumini na mchungaji wao hawakifanya lolote.

2. Kanisa la Gwajima lilifungiwa, waumini wakaleta fujo za siku mbili tatu wakazimwa na Polisi, maisha yakaendelea

Kwa hiyo usitishe mamlaka Kwa vitu visivyokuwapo.
 
Watanzania wapi unaowaongelea hapa? mfano Fr Kitima labda serikali inywee kwa sababu ya kuihofia vatican ila sio kuwahofia watanzania.
 
That was then this is today after 30 year's ago ambapo uelewa wa wananchi ulikuwa chini, Gwajima alinyamaza angesema su kwa waumini wake sijui kama leo tungekuwa tunazungumza hivi.

Nevertheless let them try.
 
Nakuelewa mkuu kama kweli kuna huo mpango bora wakaachana nao tu.

Mambo ya imani ni magumu sana wafuasi wa imani huwa wanaweka akili nyuma hisia mbele ni rahisi sana kuiingiza nchi katika vita na visasi visivyo kwisha.
 
Hao ni viongozi wa dini gani? Je,hao kama ni viongozi wa dini wao wapo juu ya sheria kama watafanya kinyume na sheria za nchi? Naomba kuelimishwa
Awamu hii, ccm inawaona viongozi wa dini ya kikristo kama chadema tuu.
 
Viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakikamatwa na kuwekwa ndani kwa miaka mingi na wengine mpaka sasa wako jera na hakujawahi kutokea chochote.

Alafu ikitokea wamekamatwa watakuwa wamekamatwa kwa sababu za kisiasa na si za kidini.
 
Nakuelewa mkuu kama kweli kuna huo mpango bora wakaachana nao tu.

Mambo ya imani ni magumu sana wafuasi wa imani huwa wanaweka akili nyuma hisia mbele ni rahisi sana kuiingiza nchi katika vita na visasi visivyo kwisha.
Mkuu kumbe siku hizi ukisha kuwa kiongozi wa dini tiyari unakuwa umejiwekea kinga ya kutokugusika na kuwa juu ya Sheria?

Mbona viongozi wengine wa dini ya kiislam wako jera na haya unayo yasema hayajawahi kutokea?
 
Akuna kitu kitatokea sababu akuna watu wa hovyo kama watanzania

Ingekua mambo ya simba na yanga sawa ila siasa na kuitetea nchi yao watanzania ni watu wa hovyo sana
 

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
You have made my day, nadhani hata wewe huwa unajicheka ukiwa nje ya humu
 
Kuwa Kiongozi wa dini hakukupi Haki ya kukiuka sheria au kuwa Juu ya sheria.

Kuna wanaojiita viongozi wa dini Wana kesi za wizi na ubakaji na wengine mauaji ya kimbali
Kama Kuna watu Wana hatua utaona kama hawana utaona pia so relax Mzee.

Chawa mjaniona mko sahihi lakini jamii ina waona ni vituko. Angalia mtu kama Lucas, tlatlaaaaaa na wengine kama wewe jinsi jamii inavyo wadharau
 
Viongozi wa dini ya kiislam wamekuwa wakikamatwa na kuwekwa ndani kwa miaka mingi na wengine mpaka sasa wako jera na hakujawahi kutokea chochote.

Alafu ikitokea wamekamatwa watakuwa wamekamatwa kwa sababu za kisiasa na si za kidini.
Inategemea kosa walilokamatiwa lkn kama la kuonea na kisiasa ni hatari sana.



Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab wa nchini Somalia.
 
Chawa mjaniona mko sahihi lakini jamii ina waona ni vituko. Angalia mtu kama Lucas, tlatlaaaaaa na wengine kama wewe jinsi jamii inavyo wadharau
Jamii idiyotii sheria itashurutishwa ,hii sio Nchi ya kambale kwamba Kila mtu ana ndevu,lazima utaratibu na utii wa sheria bila shuruti uheshimiwe.
 
Kanisa lenye nguvu duniani limekaa kimya kanakwamba Tz kuna amani. Kwanini?

Kama mliweza kugundua mpango wa kulipua pentagon, kwanini mnashindwa hili?
 
Wanaweza kuwakamata na kuwafunga na hamna mtanzania atatoka kufanya lolote! Sio kwa hizi IQ zetu mkuu wacha kujipa matumaini, wakamataji wanajua hamna kitu kitatokea na maisha yataendelea shitholeni

Issue siyo IQ, kama una akili timamu na unajua historia huwezi kuwabeza Watanzania kiasi hiki.

Kwa sasa Tanzania haina jeshi lolote. Hawa wanaofunzwa kwa kodi zetu ni jeshi la mjanja mmoja tu, hupokea maelekezo na siyo kutumia weledi wa kitaaluma. Katika hayo mazingira, mtu yuko tayari hata kumwua mzazi wake bila kosa, ilimradi tu atii amri ya boss wake.

Hata wewe hauko tayari kufa. Nasema hata wewe hauko tayari kufa. Unataka nani afe? Nina uhakika mwaka jana hukuandamana. Kwanini hukuandamana? Acha akili ya akina mange wanaotuhimiza twende tukafe huku wao wakila bata ughaibuni halafu wanatuhimiza tuandamane, wakati alipotakiwa akamatwe alikimbia nchi tena kwa njia za panya.

Siku ya maandamano, akina Lema walikuwepo barabarani?

Mtoa mada una tatizo la kufikiri.
 

Wewe ulie seriuos umefanaya lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…