Supu ya kokoto
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 4,194
- 7,602
Mkuu, tatizo la mfumo wetu wa Elimu unaharibiwa na serikali. Kwa maana hiyo tatizo moja huzaa jingine.Sasa kama unajua Hilo mbona nyuzi nyingi humu zimekuwa za kulaumu hizi shule. Ni kama ndo chanzo Cha matatizo ya mfumo wetu wa elimu?
Mfano.
Kutokana na sera ya elimu ya serikali kulazimisha wanafunzi wasome tuu bila kurudia/kukariri madarasa imepelekea shule nyingi za private kushindwa kujipambanua kitaaluma,njia pekee iliyobaki kwenye hizi shule ni kuhakikisha hata wale wanafunzi wasiojiweza kwenye madarasa husika wanafaulu hata kuliko wanaojiweza.
Hali hii imeziua hata zile shule za vipaji maana wanapokea wanafunzi wasio type yao.
Tatizo hili limezifanya shule za private kuwa biashara. Huku tatizo serikali ikifurahia kodi wanazolipa na afisa uhamiaji wakifurahia rushwa za walimu na watumishi wasio wenyeji wa ttanzania kwenye shule hizi.
Hilo ni tatizo ndio maana nikasema tunaandaa bomu la majobless na incopetent working class kupitia mambo makuu mawili.
Elimu shule za private ni biashara.
Elimu shule za serikali ni siasa.
**thamani halisi ya elimu haipo tena.