Nimetazama maazikisho ya miaka 60 ya Uhuru. Kwa silaha tulizoonesha zinanipa wasiwasi na uwezo wa jeshi letu.
Vitu vingi vilivyooneshwa ni silaha zilizotumika kipindi cha USSR.
Kuna BM 21. Kwa kweli tunatakiwa Ku modernize jeshi letu. Bado lipo nyuma sana.
kagame pale alikuwa anatuchora tu,.sisemi kwamba Rwanda itatushinda, ila kwa siku hizi, zana hizo wameonyesha ni za mwisho kabisa kutumiwa kwenye battle, kama Rwanda wanazo zana za kisasa za drones toka Israel, hizo wanakupiga vizuri tu ukienda kichwakichwa, ndio walitaka wazitumie kipindi kile watuaibishe, na wangetupa surprise kwelikweli.
sisi pia, tunatakiwa kuwa na akili, Uturuki ambao kwa sasa ni marafiki zetu sana, wametengeneza drones bora sana za kivita ambazo unazituma tu kule zinateketeza askari, Armenia imeshindwa vita na Azerbaijan, Azerbaijan ilikuwa nchi iliyoonewa sana na armenia iliporwa hata maeneo, armenia ilikuwa mbali sana kivita kuwazidi, wakaingia na mavifaru, azerbaijan wakapewa msaana na uturuki wakatumia drones tu ambazo waturuki wanatengeneza, waliwatandika waamenia hadi wakanyosha mikono na wakarudisha maeneo yao yote yaliyokuwa yameporwa. ni juzi tu hivi.
kwa hiyo na sisi utachane na masilaha ya aina hii, tunaweza kua nayo machache tu ila mengine tutumie technolojia ya kisasa zaidi, sio kwamba tuacha haya ila tuangalie nchi za wenzetu wanatumia nini.
though, kwa sasa Tanzania haiihitaji hata kupoteza pesa kununua silaha kwasababu sidhani kama kuna adui mkubwa ambaye ni nchi ni threat kwetu, hata Rwanda kipindi cha JK walikuwa wanaoogopa mno kwasababu tungewapiga au wangetupiga (jambo ambalo ni gumu kwao), they could not stand to live with a monster besides their country for therest of their lives, wasingeweza kustahimili kuishi na adui pembeni yao miaka ya mbeleni, hasa kagame ambaye anajua tungeweza kuweka hata rais mwingine akitokea Tanzania kama tukitaka kama tulivyofanya kwa m7.waasi wake wangekuja tu hapa na kuanzia safari hapa.