Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Ulinzi ni pamoja na kuonesha uwezo ulionao. Kwa silaha zilizooneshwa kusema kweli ni hafifu. Zimepitwa ma wakati. Uganda na Kenya wana silaha bora kutuzidi.
We are weak compared to them.
Vita ni akili,sio maguvu.
 
Mkuu Navy ya Kenya ipo sawa,inalinda bahari yake kwa manowari zake za kila aina.
Sisi tunashida hapo,kama Nyerere angekuwa hai labda aibu hiyo ingeishafutika.
Ukishakuwa na ukanda wako wa bahari mkubwa,pammoja na maziwa ya kumwaga tena una share na majirani zako,na huku umeapa kulinda na kutetea mipaka yetu,bila kuwekeza ni hatari.
 
Tunawaambia hawa vijana kuwa tupo weak ktk hili eneo ila wanatupinga.

Si unaona miaka ya nyuma kuhusu ziwa Nyasa? Hayat Nyerere eneo la ulinzi hakutaka mchezo kabisa.

Kenya ipo hatua mbele zaidi ktk kila nyanja ya teknolojia dhidhi ya jeshi letu. Jamaa wapo mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mfuatiliaji wa silaha za nchi mbalimbali. Hakuna silaha za kutisha hapo. Uganda na Kenya display yao inatisha Mzee.
Sio lazima tuwaoneshe Cha uvunguni mkuu 👍👍
 
Mzee hiyo ni silaha ya 1967 USSR technology
M
Unajifanya unajua sana.

Sasa nenda kaangalie or tupe ni aina gani ya Surfaces to Air missiles ulimwenguni pekee zenye sifa ya kutungua stealth technology Multirole Jet Fighter.

Hizo ndio zilitungua hizo ndege za America zenye stealth technology in Chechnya.

Acheni ujuaji wa kijinga na ushamba.
 

Wewe nawe ni boya.

Kwenye list ile haikuwa na order, ikiwa na maana yaani wamepenga tu moja mpaka mwisho randomly.

Na pia, ilihusisha special forces only na sio jeshi kigezo kikubwa ni hiw well trained and equipped. Special Forces za Tanzania Congo walikua wakitumia Galil MAR na ndio maana kwenye list ile hata vikosi maalumu vya Romania vipo nao wanatumia Galil MAR kwakua sio silaha za mchezo mchezo.

Acheni ushamba na ujuaji wa kijinga!


"These are the world’s most elite military teams. They’re highly trained, best equipped and well-prepared fighting units specializing in surgical military operations, from ending a hostage situation swiftly to stealthily eliminating top terrorists.

Yeah, pity the fools who get on the wrong side of any of these elite fighting forces. Please keep in mind that this list is in no particular order. We just hope you enjoy this one."

35 Most Elite Special Forces Around The World


Yaani mpaka wameweka, "please!". Kama huelewi kingereza omba msaada.
 
Ulinzi ni pamoja na kuonesha uwezo ulionao. Kwa silaha zilizooneshwa kusema kweli ni hafifu. Zimepitwa ma wakati. Uganda na Kenya wana silaha bora kutuzidi.
We are weak compared to them.
hebu weka za Uganda na Kenya tuone
 
Mambo hayo ni ya kishamba na ya kizamani. Uganda wapo SU-30 wanaionesha tena kila mmoja anaiona.
Kenya wanaonesha silaha za kila aina. Rwanda nao wanaonesha silaha.

We are weak. Hatuna silaha za kutisha. Mpaka jeshi linaonesha madaraja kweli!?
silaha ya kutisha ni kama ipi mzee?
 
Mzee mambo ya watu kupiganisha yalishapitwa na wakati. Sasa hivi ni technology ndio inapigana. Achana na mawazo ya kijima ya Nduli Idd Amin Dadaa.
yamepitwa na wakati kivipi, US kaondoa lini majeshi yake kule Afghanistan? Mbona hazikupelekwa drones kule
 
Naamini malengo ya kuonyesha silaha ulizo nazo hutofautiana baina ya nchi mfano N. Korea huringishia dunia ili mabeberu wajifikirie mara mbili mbili kumuingia. Sidhani kama sisi tuna potential 'enemies' wa namna hiyo, plus naamini usiri ni moja ya sifa muhimu za jeshi.
Ila itapendeza sana kama jeshi letu likionyesha midubwana ya kutisha mara moja moja 😁
 
Ulinzi ni pamoja na kuonesha uwezo ulionao. Kwa silaha zilizooneshwa kusema kweli ni hafifu. Zimepitwa ma wakati. Uganda na Kenya wana silaha bora kutuzidi.
We are weak compared to them.
Walionyesha zao lini mkuu, mbona hukutuonyesha walipozitoa za kwao!

Mada yako hukuitendea haki kwa hayo uliyoandika hapo, yaani hayaelezi chochote, halafu unalalamika tu!

Eleza kikamilifu wewe umeona upungufu gani na wapi. Hivi vimistari mitatu kweli ndivyo unadhani vinaweza kuelezea nguvu au upungufu wa silaha za jeshi?

Kama wewe mwenye kujuwa unashindwa hatakuelezea unayoyajuwa, utalaumu vipi hali ambayo umeshindwa kuielezea?

Ni kama umetegeshea tu mada yako wachangiaji wakusaidie kujazia yale ambayo wewe mwenyewe umeshindwa kuyaelezea.

Unapoona upungufu, elezea kinagaubaga upungufu huo kwa ndani zaidi watu, hata wasiokuwa na uelewa wa hali hiyo wapate kufahamu. Wewe hapa una'assume' watakaokusoma watajuwa unachozungumzia?

Sasa sijui kama utaelewa nilichokueleza hapa! Pengine utadhani ninaku'criticize' bila ya sababu!
 
kwa amani iliyopo bongo kwanini usiwape hizo sifa? maana yake wanafanyA kaz yao ipasavyo. Ama Kuna kigezo kingine. Kuna mdau huko juu amesema ukijiona unakula nyama na bia kwa Aman ujue Kuna wanaume hawalali kuhakikisha hayo yote yanatokea. [emoji706][emoji706][emoji706]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…