Heshima yako mkuu!
Kabla sijasoma post yako hata mimi nlichangia hoja hapa kuwa kuna nchi kama Kenya na Ethiopia. Hizi nchi ktk ukanda wetu zimepiga hatua kubwa mno ktk uwekezaji jeshini.
Hatuwez leo kusema tuna kikosi bora kwa kuwa tuliwapiga M23 au waasi wengine, ilishawahi kutokea miaka ya nyuma Tz tukashika namba ishirin na kitu kwenye vikosi bora ulimwenguni, watu tukasifia mno.
Lakini huwez amini mkuu, China, Korea zote mbil n.k hawamo mle ndan, je kusema sisi ni bora kulia wao? Tumekuwa watu wa kusifia hiki chombo lakini kiuhalisia hakina sifa ambazo zinazo.
Kwa zama hizi tuna jeshi la kawaida mno, tena tusije thubutu jifananisha na majeshi mengine hapa Afrika.