Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Haya ndio madhara ya ujuaji.

Silaha za jeshi zipo outdated, outdated unadhani silaha ni smartphone zinazotoka kila mwaka na muda wowote utakuwa na budget ya kununua?

Silaha ni silaha sio smartphone au jaribu kuchukua Dreyse Reichsrevolver ambayo imetengenezwa mwaka 1879 then weka utosini na upull ile trigger kama haitakumwaga ubongo basi hii hoja yako ya silaha kuwa outdated kama windows xp itamake sense.
 
Wewe kichwa udongo mbona hujibu swali ninalokuuliza? Askari wa miguu wanaweza kupambana na Su-30
Huwa sijadiliani na watu wenye kumbukumbu duni na uwezo mdogo wa kufikiri na kujengwa hoja
 
Huwa sijadiliani na watu wenye kumbukumbu duni na uwezo mdogo wa kufikiri na kujengwa hoja
Jibu swali mzee acha kuwaka kwa hasira. Askari waendao kwa miguu wanaweza kupambana Su-30 ya uganda?

 
Watu wameshatoka huko kwenye uzalendo sijui heshima.

Sasa hivi Jeshi ni SILAHA, SILAHA ni TECKNOLOJIA.
Jeshi ni silaha, silaha ni technology.

Mkuu unaandika utadhani tanzania inakimbizana kiuchumi na USA.
Au unadhani hizo silaha na technology zake watu walitengeneza na wanagawa bure?
 
Nataman kuendelea kuzungumza na wewe kuhusu hii mada lakini naomba ufute neno la kuniita Boya.

Sipendagi kabisa kuona mtu akinitusi ukitazama tungeweza kuzungumza kawaida tu.

Hata siku mama yako akitofautiana na jirani au baba yako sidhani kama utafurahia akiitwa Boya. Hatujuani humu ndani, hivyo kutofautiana kimtazamo kusifanye kumdharau mwenzio na kumuita majina kama hayo.
 
Wewe ni expert tangu lini na una uzoefu wa miaka mingapi kwenye sekta ya technology na silaha za jeshi?
 
Mzee nimefuatilia comments zako katika thread hii, umekuja kuchamba watu kama Mange. Sijaona hoja comment yoyote uliyoweka tukuone wewe ni GT.
Mimi nimemsoma nikaona ngoja nimkalie kimya. Naona anaropokaropoka tu kama mtoto mwenye njaa aliyekosa vitumbua na sambusa.
 
Hawawezi kukuelewa vijana wa miaka ya 90 na 2000, wasamehe tu.

Tunahitaji mabadiliko makubwa ya kiteknolojia ktk hiki chombo.
 
Sidhani kwa intelligence ya kawaida kabisa unaweza kutoa silaha zako muhimu ukaanika mbele ya wageni
 
Tuna rasilimali kila eneo, badala ya kuonesha nini tumefanya na wapi tunaenda, tunaonesha mtu kushuka ktk helkopta, tunaonesha bunduk za kuangulia ndege, zama hizi jeshi linahitaji vitu hivi?

Watu siku hizi wanakaa zanzibar, wanapaki meli msumbiji then wanatarget Pwani au Mtwara, hakuna tena mambo ya kupeleka watu eneo la tukio. Watu wanaenda baada ya kusafishwa kwanza.
 
Hao vijana kukuelewa ni ngumu.

US ilivyojiandaa dhidi ya mapambano yale, sivyo ambavyo alichokikuta.

Akirudia kukusoma kwa makini ataelewa umemaanisha nini.
 
Propaganda tu hizo. Design za socialist countries..... Maonyesho kama haya utayaona tu kwenye nchi kama North Korea, China, Russia.

Sijui wa namaanisha kuwa hiyo miaka 60 wanafanikiwa kujenga jeshi imara.....!!!
Sehemu kubwa wenzetu ktk show off hizi zile silaha wanakuwa wametengeneza wao. So wanaonesha moja ya maendeleo ya mafanikio yao.

Sijajua sisi hapa tunaonesha for what.
 
Ukitaja Blackhawk unaongelea moja ya most advanced chopper si ndio, na mission ikafeli pia. So vita sio silaha tu pekee ndo zitakazo guarantee ushindi. Ama sivyo!?[emoji3] Wale wasomali walikuwa wanatumia AK tu na RPGs
 
Tanzania akuna stable jeshi,.. siasa nyingi sana mwanajeshi anasikia kuandamana anaenda kufanya usafi badala wawe upande na wananchi kudai haki yao...
Muda gani wanapata ku- assambble na ku- configure mitambo ..hakuna kazi pale
Uliwahi isikia ile trilion 3 ya mnadhimu mkuu wa jeshi?

Umeongea ukweli mtupu, kama police ilivyotafunwa na siasa, ndivyo ambavyo na jeshi pia lilivyomegwa.

Hakuna tena ule uzalendo ila kila mtu anatazama anaweka nini ndani ya tumbo lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…