Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Kaka, Uganda ana sukhoi, anapenya popote hapa kwetu na anatokomea pasipojulikana.
 
Hakuna mapambano ya ana kwa ana katika ulimwengu wa sasa. Sasa hivi ni Tehnologies tu zinapambana.
Askari wa miguu watapambana na Rocket?
Ama kweli wewe ni mtalaamu wa masuala ya vita kupitia Google!

Ndo mnavyodanganyana, sio?! Hivi una habari moja ya sababu ya kwanini Marekani vita vyake huwa vinachukua muda mrefu sana hata kupigana na wanamgambo ni kwa sababu anaogopa vita vya ana kwa ana?! Chifu, kuna na masilaha kama yote lakini hayo hayana uwezo wa kuteka hata ofisi ya mtendaji wa kijiji unless kama lengo lako ni kufanya tu destruction kisha ukimbie!!

Vurumisha makombora yako kama yote na kutoka kokote kule duniani lakini mwisho wa siku ni lazima uingize boots ardhini kwenda kumaliza mchezo!!! Wale M23 wa Kagame kama tungetumia ndege wala tusingeweza kuwafuta haraka lakini ni boots ardhini ndizo ziliweza kumaliza mchezo asubuhi hata jua halijatoka! US walimaliza mapema Vita na Saadam Hussein 2003 kwa sababu walikuwa na askari ardhini! Hawa askari ndio waliteka sehemu zote muhimu including uwanja wa jeshi! Hivyo ndivyo vita vinamalizwa!

Tofauti na 2003 Iraq War, angalia Afghanistan alikokuwa anaogopa kupeleka majeshi ardhini, matokeo yake vita vimedumu for almost 20 years hadi walipoamua kuondoka kwa sababu wakati wao wananarusha makombora na drones, wenzao wamejichimbia kwenye mahandaki wanakusubitri uchoke kurudha makombora yako, kisha wanarudi mzigoni!!
 
nilitegemea jibu kama hili baada tu ya kumaliza kusoma hoja, na hizi ni kauliz nzuri mno za kujipa moyo, ni vizuri kwa kweli.
Watu watazame ktk sites mbalimbali kwa sasa tupo nafasi ya ngapi.

Vijana hawa ukiwaambia hata vita ya ug tulisaidiwa na vikundi vingi vya kumwondoa Idi Amin hawawez kukuelewa.
 
wataalam hebu tuambieni hizi zana zilitengenezwa lini na nchi gani?

Pia zile ndege lilizokuwa zinatupigie makelele zikiruka chini chini je zina aslimilia ngapi ya kujificha kwenye rada ya adui?

ni hayo tu.
Zile ndege hakuna kitu kaka.
 
Watu wenye akili timamu mnasema hivi, matahira watakupinga.
 
Hapana. ....usijipe moyo...zile ndiyo silaha zetu kali
 
Taliban walitumia AK47 na mabomu ya kutega barabarani tuu na waliweza kumshinda Mwamerika mwenye kila aina ya silaha ambazo ziltengenezwa kwa matrilioni ya dola. Kuwa na silaha mpya siyo muhimu kama utayari wa kupigana.
Aisee😂😂
 
Ww unazani silaa za kivita ni bei rahisi hivyo..
 
Umemaliza kaka, barikiwa sana
 
Wapi nimetaja mlio wa engine au umechanganyikiwa?
 
Wewe kichwa udongo mbona hujibu swali ninalokuuliza? Askari wa miguu wanaweza kupambana na Su-30
We nae uache ujuaji wa kitoto unaelekezwa hutaki , hiyo su 30 inaweza kuokoa mateka waliowekwa sehemu na watekaji? Sikia mpaka dunia inaisha askari wa miguu bado wana umuhimu sana sana hizo teknolojia zipo kurahisisha mfano kuna watu wametekwa na kufichwa sehemu fulani hebu nielezee hapa hapa jinsi hizo sukhoi zako zitakavyowaokoa mateka pekee .
 
Na ukitaka kujua mswahili mtu mbaya sanaaaaa , endapo zingepitishwa ma advanced weapons za kutisha ile amsha amsha popo humu kungetamalaki mapovu mara masilaha yote ya nini kwani tuna vita? mara nchi haina hata matundu ya vyoo mnanunua masilaha ya kisasa,mara pembejeo zinapanda bei mnanunua madege ya vita 😂😂😂😂mswahili yookwe alafu yule jamaa mwenye uzi wa "usiwasaidie masikini acha wafe yuko wapi mkweli sana yule wabongo wengi roho inatusumbua ya kulalama na kulalama na umasikini ni kota na pichu
 
Maswala ya Jeshi ni very complex sana, mwenye utimamu wa akili awezi ongelea hii mada kama mnavyofanya.

Walioamua kutoa hizo silaha in public ni wao kwahiyo ni wao wanaamua watoe nini na wataonekanaje kwa public.

Acheni ujuaji usiokua na mpango!
 
Mkuu nimeshuhudia Kenya Navy si mara mmoja ni mara nyingi tu kwa miaka kadha anaita hiyo meli inayoonekana kwenye radar ujitambulishe labda uko maili 200 kutoka Mombasa huko deep sea. Na ukikaidi unaweza ghafla ukashtukia manowali nyingine ya Kenya Navy iliopo karibu nawewe inakusogelea.
Aibu kwa taifa langu hiyo bahari ya Indi eneo letuinalindwa na nini?Hakuna patrol vessel ndio sababu madawa ya kulevya yanasushwa hadi karibu na pwani zetu,Wavuvi haramu wanavua hadi milangoni mwa Dar sababu hakuna ulinzi hata wa sungusungu ni aibu.
Lakini cha ajabu naona Navy ina maofisa wengi wa nyota kibao hali huku hawana manowari za kufanyia kazi, kama vinavyoonyesha vyeo vyao.Swali hawa wanapandishwaje bila kuwa na zana husika?Kwa kuwa vigezo vilivyoiweka Navy kuwa kikosi kamili vimepwaya je nini kifuate?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…