Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Kama silaha zilizooneshwa ndio za Jeshi letu, bado tupo nyuma sana

Rafiki sikupingi. Yale madude yetu adui akiamua kutumia modernized drones anayalevel hata kabla Misa ya kwanza haijaisha.

We need to modernize real. Display zile zile kila mwaka! Bora hata wasiyaoneshe.

Bunduki zenyewe asilimia kubwa ni mabunduki ya vita ya kwanza ya dunia
Kaka, Uganda ana sukhoi, anapenya popote hapa kwetu na anatokomea pasipojulikana.
 
Hakuna mapambano ya ana kwa ana katika ulimwengu wa sasa. Sasa hivi ni Tehnologies tu zinapambana.
Askari wa miguu watapambana na Rocket?
Ama kweli wewe ni mtalaamu wa masuala ya vita kupitia Google!

Ndo mnavyodanganyana, sio?! Hivi una habari moja ya sababu ya kwanini Marekani vita vyake huwa vinachukua muda mrefu sana hata kupigana na wanamgambo ni kwa sababu anaogopa vita vya ana kwa ana?! Chifu, kuna na masilaha kama yote lakini hayo hayana uwezo wa kuteka hata ofisi ya mtendaji wa kijiji unless kama lengo lako ni kufanya tu destruction kisha ukimbie!!

Vurumisha makombora yako kama yote na kutoka kokote kule duniani lakini mwisho wa siku ni lazima uingize boots ardhini kwenda kumaliza mchezo!!! Wale M23 wa Kagame kama tungetumia ndege wala tusingeweza kuwafuta haraka lakini ni boots ardhini ndizo ziliweza kumaliza mchezo asubuhi hata jua halijatoka! US walimaliza mapema Vita na Saadam Hussein 2003 kwa sababu walikuwa na askari ardhini! Hawa askari ndio waliteka sehemu zote muhimu including uwanja wa jeshi! Hivyo ndivyo vita vinamalizwa!

Tofauti na 2003 Iraq War, angalia Afghanistan alikokuwa anaogopa kupeleka majeshi ardhini, matokeo yake vita vimedumu for almost 20 years hadi walipoamua kuondoka kwa sababu wakati wao wananarusha makombora na drones, wenzao wamejichimbia kwenye mahandaki wanakusubitri uchoke kurudha makombora yako, kisha wanarudi mzigoni!!
 
nilitegemea jibu kama hili baada tu ya kumaliza kusoma hoja, na hizi ni kauliz nzuri mno za kujipa moyo, ni vizuri kwa kweli.
Watu watazame ktk sites mbalimbali kwa sasa tupo nafasi ya ngapi.

Vijana hawa ukiwaambia hata vita ya ug tulisaidiwa na vikundi vingi vya kumwondoa Idi Amin hawawez kukuelewa.
 
wataalam hebu tuambieni hizi zana zilitengenezwa lini na nchi gani?

Pia zile ndege lilizokuwa zinatupigie makelele zikiruka chini chini je zina aslimilia ngapi ya kujificha kwenye rada ya adui?

ni hayo tu.
Zile ndege hakuna kitu kaka.
 
Dhana nzima ya kuchukulia sikukuu ya Uhuru na kuifanya ionekane kama military exhibition ni utoto. Hatuna adui aliyetuzunguka, why waste our meagre resources on nonsense. Sherehe tulitegemea tuone ngoma na nyimbo na miundombinu ambayo inamgusa raia. not anything to do with war. Hii ni ufinyu wa akili.
Watu wenye akili timamu mnasema hivi, matahira watakupinga.
 
Vijana wengi wanaangalia movies zinawachanganya sana, hawajui mambo kwa ground ni tofauti kabisa.

Tanzania ni nchi ya Kijamaa, mambo yake mengi ni siri, hicho wanachoonyesha sicho kilichopo...

Kila Mwaka bajeti ya wizara ya Ulinzi na usalama inatengwa tena ya kutosha, umewahi kusikia wametangaza kununua hiki ama kile...

Ukiona umekaa sehemu unashushia bia na nyama choma tena kwa amani kabisa jua kuna wanaume hawalali huko.
Hapana. ....usijipe moyo...zile ndiyo silaha zetu kali
 
Taliban walitumia AK47 na mabomu ya kutega barabarani tuu na waliweza kumshinda Mwamerika mwenye kila aina ya silaha ambazo ziltengenezwa kwa matrilioni ya dola. Kuwa na silaha mpya siyo muhimu kama utayari wa kupigana.
Aisee😂😂
 
Sio dharau mkuu. Nikisema fulani ana elimu ya darasa la saba na huyu ana PhD utasema namdharau mwenye la saba B. Yani kuwa muwazi kibongo inaitwa dharau. Nchi nyingine zinaita tenda inajadiliwa na bunge na vyombo vya habari vinahoji, watu wanaanzisha debate kushindanisha silaha gani wanunue kwa fungu walilonalo. Watu wanatoka wanaenda Dubai Airshow, Army Expo, MAKS Airshow na wakirudi wanasema ukweli walioona nchi inaamua.

Last week mpaka leo kuna matukio kadhaa. India kasaini mkataba wa kutengeneza assault rifle za Kalashnikov ya Russia. UAE imenunua Rafales 80 kutoka Ufaransa kwa zaidi ya trilioni 43 za kibongo. Finland imesaini kununua F-35 kutoka Marekani. Hizi zote zinafanyiwa mchuano mkali na tenda zinakuwa wazi na wananchi wana haki ya kuhoji.

Sisi hapa tukisema tunaitwa wajuaji na wajinga. Maana ya jeshi la wananchi haipo wala haizingatiwi. Ila Afrika ndo ilivyo hata ndoto tunazoota sidhani kama wazungu huota hivi
Umemaliza kaka, barikiwa sana
 
Mkuu yaani unagundua ubora wa ndege kwa mlio wa engine? tena engine ya fighter jet? sio bodaboda wala bajaji?
Kitu ambacho hukioni mara kwa mara wala technology iliyotumika au unategemea engine ya fighter jet inayotembea atleast at 1000km/h iwe na sound kama ndege ya abiria au pikipiki ya boxer?
Seriously?

Mkuu lini umekuwa expert wa maswala ya engine za fighter jets na ubora wake au wewe ni army pilot?
Wapi nimetaja mlio wa engine au umechanganyikiwa?
 
Wewe kichwa udongo mbona hujibu swali ninalokuuliza? Askari wa miguu wanaweza kupambana na Su-30
We nae uache ujuaji wa kitoto unaelekezwa hutaki , hiyo su 30 inaweza kuokoa mateka waliowekwa sehemu na watekaji? Sikia mpaka dunia inaisha askari wa miguu bado wana umuhimu sana sana hizo teknolojia zipo kurahisisha mfano kuna watu wametekwa na kufichwa sehemu fulani hebu nielezee hapa hapa jinsi hizo sukhoi zako zitakavyowaokoa mateka pekee .
 
Na ukitaka kujua mswahili mtu mbaya sanaaaaa , endapo zingepitishwa ma advanced weapons za kutisha ile amsha amsha popo humu kungetamalaki mapovu mara masilaha yote ya nini kwani tuna vita? mara nchi haina hata matundu ya vyoo mnanunua masilaha ya kisasa,mara pembejeo zinapanda bei mnanunua madege ya vita 😂😂😂😂mswahili yookwe alafu yule jamaa mwenye uzi wa "usiwasaidie masikini acha wafe yuko wapi mkweli sana yule wabongo wengi roho inatusumbua ya kulalama na kulalama na umasikini ni kota na pichu
 
Nataman kuendelea kuzungumza na wewe kuhusu hii mada lakini naomba ufute neno la kuniita Boya.

Sipendagi kabisa kuona mtu akinitusi ukitazama tungeweza kuzungumza kawaida tu.

Hata siku mama yako akitofautiana na jirani au baba yako sidhani kama utafurahia akiitwa Boya. Hatujuani humu ndani, hivyo kutofautiana kimtazamo kusifanye kumdharau mwenzio na kumuita majina kama hayo.
Maswala ya Jeshi ni very complex sana, mwenye utimamu wa akili awezi ongelea hii mada kama mnavyofanya.

Walioamua kutoa hizo silaha in public ni wao kwahiyo ni wao wanaamua watoe nini na wataonekanaje kwa public.

Acheni ujuaji usiokua na mpango!
 
Tunawaambia hawa vijana kuwa tupo weak ktk hili eneo ila wanatupinga.

Si unaona miaka ya nyuma kuhusu ziwa Nyasa? Hayat Nyerere eneo la ulinzi hakutaka mchezo kabisa.

Kenya ipo hatua mbele zaidi ktk kila nyanja ya teknolojia dhidhi ya jeshi letu. Jamaa wapo mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nimeshuhudia Kenya Navy si mara mmoja ni mara nyingi tu kwa miaka kadha anaita hiyo meli inayoonekana kwenye radar ujitambulishe labda uko maili 200 kutoka Mombasa huko deep sea. Na ukikaidi unaweza ghafla ukashtukia manowali nyingine ya Kenya Navy iliopo karibu nawewe inakusogelea.
Aibu kwa taifa langu hiyo bahari ya Indi eneo letuinalindwa na nini?Hakuna patrol vessel ndio sababu madawa ya kulevya yanasushwa hadi karibu na pwani zetu,Wavuvi haramu wanavua hadi milangoni mwa Dar sababu hakuna ulinzi hata wa sungusungu ni aibu.
Lakini cha ajabu naona Navy ina maofisa wengi wa nyota kibao hali huku hawana manowari za kufanyia kazi, kama vinavyoonyesha vyeo vyao.Swali hawa wanapandishwaje bila kuwa na zana husika?Kwa kuwa vigezo vilivyoiweka Navy kuwa kikosi kamili vimepwaya je nini kifuate?
 
Back
Top Bottom