Kama sio janja ya kutengeneza upigaji kwa manufaa ya tumbo lake hii ni nini? Waziri wa Nishati kuanzisha mradi wa Tril 1.7 kabla JNHP kukamilika

Sielewi kwa nini na sisi tunatafuta kuiga 'model' ileile ambayo inawapa matatizo makubwa wenzetu hawa!
Si kuiga model ya Kenya, kwanza kwanini tuige kama kweli tuna wasomi na wataalamu?

Lengo ni kuonesha jinsi gani tumesheheni kwa kila kitu isipokuwa kwa akili tu.
 
Si kuiga model ya Kenya, kwanza kwanini tuige kama kweli tuna wasomi na wataalamu?

Lengo ni kuonesha jinsi gani tumesheheni kwa kila kitu isipokuwa kwa akili tu.
Wasomi wana njaa; hapana. Wasomi ni walafi. Hawatumii vichwa, wanatumia tumbo.
 
We jamaa sijui January kakufanya nn???
 
tuvumilie tu muda ni rafiki wa kweli
mahitaji ya nchi maskini ni mengi mno na hasa ukizingatiwa wengi huwenda hatujui tunahitaji nini zaidi ya kusubiri na kuogopa kufa.
 
Mimi nazungumzia kweli
Wewe huzungumzi kweli Bali una NONGWA. au ukweli wako unalenga usiowapenda.
Ipo hivi.
Magufuli alifanya mambo mengi sana ya kipuuzi kwenye nchi inayoitwa TANZANIA hatujawahi kusikia ukisema. Unaweza kuthibitisha. Leo ukweli unatoaje wapi ndugu wewe? Waliosema ukweli chini ya dictator uchwara unapajua walipo leo???
Tuache unafiki
 
Urefu wa kamba unaamliwa na mbiuzi au mwenye mbuzi?
 
Tukiwaambia CCM ni janga nchi hii mnakataa
 
Subirieni Kwanza tuwanyonye mpaka mavu ndio mpate akili.
Tunapambana kutengeneza kizazi kitakachowanyonya wajukuu na wajukuu zenu ama hamuoni Koo ya Kenyatta ,bush was USA na wengine akina sultan seyyid said,barghash, wanatoke Koo ile ile.
Sasa wewe kalisha kalio lako na ofa yako ya un na tekno yako wakati sie wazee walihangaika kupambana wakati wazee wenu kazi ilikuwa Ni kufaki na kuongeza wake wengi.mmezaliwa wengi na hakuna mjanja wa kupambana ili afike 5% ya wajanja wa duniani waliokalia wengine mabegani.
Tutawanyonya kwa Kodi lukuki Kila Kona saivi hata kumtumia mama yako kijijini kahamsini kutoka laki tank unayoipata tunakanyonya.
Sie wanetu wanasoma nje nyie mnafhrahia bure.
Hakuna namna kubalini tu mliwe ,na uzuri tunatumia masikini wenzenu ambao Ni Askari kuwabana ama kuwashika ili mtuliwe mnaponyonywa damu.
Yaani nachukua masikini wenzako nawapa mafunzo ya kutulinda ili tuwanyonye tunawapa silaha na mamlaka ya kushuti unapoleta kidomo.
Na yeye anachoangalia Ni tumbo basi Mana hawezi peleka kijana wake hata chip akamlipia Ada atabakia kutulilia sie.

Wewe Lina asali yako umwa na nyuki halafu mie naichukua kiulaini Kama hutaki namwambia polisi anakubana pumbo mpaka ujanja unaisha.

Bisha Sasa uone.
Yaani masikini akipewa mkate akaambiwa ua masikini mwenzako Ni fasta sana.

Na bado tutanzisha miradi mingi.
Bwawa litachukua miaka 50 kukamilika.
Ama hamuoni hoja tayari na mazingira yameshaanza bungeni kuwandaa kisaikilojia.
Na ile hela ya software ya wahindi nilikula Sasa unatakaje.
Kazi ya mtawala Ni kuhakikisha unatawalika kiulaini bila ya pingamizi.

Karibia na uchaguzi masikini Ni cheap sana ananulika hata na kofia ya Mia tano pombe na chakula.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…