Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kufaulu maisha?
We hujui kitu,watoto wetu tunawapeleka private kuanzia la kwanza had I kidato cha NNE,wakifaulu kwenda form five kwenda shule za sirikali za kata tunawapeleka ili waingie kwenye mfumo na wanakimbiza mbaya huko.

Ndo hao unaoowaona wamejazana hhuko kwenye mabenki,TRA,hata serikalini wapo tu.
 
Hakikisha awachallenge kimaisha pia, sio amalize degree na ma AAA yake uanze kumlisha ugali akiwa 30yrs hapo kwako.😁😁😁 sababu hana pa kupeleka cheti apate chochote kitu.
Ushauri mzuri mkuu,
Nina maisha magumu sana mkuu sio kwamba Nina hela hivyo ada yenyewe wakati mwingine huwa nakopa hela nazilipa kwa riba ili tu madogo wasome,na sishahuriki mkuu.

Huko mbeleni kuanzia A Lev tunawachanganya na kwenye shule za kata,ila kwa kuwa wankuwa na msingi mzuri Wa elimu ya awali huko no mdebwedo tu,na mwisho Wa siku wanaingia tu serikalini kamma kawa wakibahatisha.
 
Kuna wazazi wanapata stress ikifika kipindi cha kulipa ada mpaka wanatia huruma.
Kuna mtoto amekaa wiki tatu hajaenda shule tatizo ada.
Mwingine alikuwa analalamika hela imekuwa ngumu plus anadaiwa term ya nyuma hivo mtoto hatapokelewa atleast angekuwa anadaiwa mwaka huu mpya wa masomo wangemvumilia kidogo.
Mimi kwakweli nikija jaaliwa kama nikiona maisha yangu tia maji tia maji wala sitaki stress aende tu kayumba nitajitahidi asikose tution na kumsimamia.
Muda mwingine unakuta mtu anateseka na kumhamisha hawezi anawaza walimwengu watamuonaje.
Pata picha una watoto watatu halafu hela yenyew yamawazo lazima akili ikukae sawa.

Kabisa watu wanaangalia wataonajwe na walimwengu akipeleka watoto KAYUMBA.
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Elimu bure chumba kimoja cha darasa watoto 300 akitoka hapo anaenda secondary ya kata kisha kidato cha tano na sita Azania kisha chuo

Akija kuomba kazi katika usahili anakutana na wenzake walio pitia English media yeye na the,the zake labda huyo HR awe mjomba wake ndio atapata kazi siongei kiushabiki nina experience na hili

Ushauri wangu kwako siku hizi English media zipo kibao tena bei chee tu mtafutie mwanao shule ya karibu ili akikua kidogo ache kupanda school bus ili kupunguza gharama

Na uvyosema sijui ada million 3 inaonekana wewe hujawahi kusomesha maana hiyo ada inalipwa kidogo kidogo ndani ya mwaka mzima
 
Dah, yaani umeongea kama wale jamaa wa kulima matikiti kwenye pdf.
Hahahaha! We unamatatizo.
Ajira hakuna ..balance kipato.. sio unapeleka m3 kila mwaka mwenzako anabadilisha Prado na kuongeza nyumba ununio.. wewe na mwanao mkishamaliza umepukutisha tens of millions na anamkopo juu.. ni mdaiwa .. 🙂 halafu unaanza kusumbu watu.. na simu mwanao atafutiwe kitengo. Mtunzie kuanzia chake kama Sehemu ya package yake ya elimu.
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
[emoji3]
 
Una mawazo mazuri ila unavoyawasilisha kama mapovu flani hivi au mkuu unaona wivu watoto wa wenzio kusoma shile za kishua
 
Mm nimesoma kayumba ,kiingereza nakijua kuongea vizur bila mtetemo ,ila kwa shule za kayumba za Leo hapana aisee siwez peleka mtoto huko labda nisiwe na hela kabsaa nimechoka ......lazima nipeleke mtoto eng.medium akapanue wigo na kukutana na marafiki wenye ahueni ya maisha ..baadaye watapeana connection za kimaisha

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Umeongea maneno makubwa sana mkuu..
Yapaswa uwe na mawazo ya mbali sana kulielewa hilo..
Utakuta mtu ni kapuku kabisa, hana chochote nae anashindana na wenzie mtaani kupeleka mtoto shule za kurudishwa na gari.

Ukimuuliza kwa nini usisomeshe mtoto shule ya kawaida?
Anasema siwezi kumsomesha mwanangu shule kama nilizosoma Mimi..

Sasa kama shule hizo za kayumba hazina msaada mbona wewe sasa unaweza kumsomesha mwanao,,shule ya gharama kubwa?
Je kama shule uliyosoma haikukusaidia ungewezaje kupata kazi nzr ya kuweza kumsomesha mwanao shule ya gharama Leo?

Jibu ni college , mtoto hata umsomeshe shule ya gharama kiasi gani bila kwenda chuo ni sawa na zero..

Na mtoto hata asome shule duni kiasi gani lakini akifika chuo hatokuwa na tofauti na yule aliyesoma shule za gharama.

Wakikutana chuoni hakuna utofauti wowote.
 
Mpeleke mtoto shule akajue lugha, lugha hasa English ni muhimu sana kwa kizazi hichi. Achana na masuala ya gharama..tafuta pesa wacha excuses za kijinga ...unakwepa gharama za leo huku mtoto unam'bebesha gharama za maisha yake ..kama unampenda mwanao basi utamlinda...

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Sehemu tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watanzania mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne.. anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68, ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Mzazi unaishi mjini hao ng'ombe utawatunzia wapi? Kama umeajiriwa hao ng'ombe nani ataangalia..? So unaandika andika tu mkuu, siyo rahisi kiivyo

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Uzuri tumejifunza kitu the hard way, ukikosa pesa huthaminiki! Hili ndio kosa la kwanza kurekebisha kwa watoto wetu ambao ndio generation ijayo. [emoji23][emoji23][emoji23] Cheti bila pesa ni Utopolo tu! Kijana wangu asije kushindwa kuchakata mama kali bure kwa kigezo hana mawe akae kinyonge staki kabisa huo upumbavu! Elimu atapata ila lazma awe na mzigo pia. Nitahakikisha hilo!
Utamjenga vip kijana wako aje kuwa mwanaume bora? Hiyo ni changamoto yako ..kama umeanza kumnyoa maviduku, anapiga ma kata k mapema mzee hapo unampoteza ..nimesema tu ..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Uzuri tumejifunza kitu the hard way, ukikosa pesa huthaminiki! Hili ndio kosa la kwanza kurekebisha kwa watoto wetu ambao ndio generation ijayo. [emoji23][emoji23][emoji23] Cheti bila pesa ni Utopolo tu! Kijana wangu asije kushindwa kuchakata mama kali bure kwa kigezo hana mawe akae kinyonge staki kabisa huo upumbavu! Elimu atapata ila lazma awe na mzigo pia. Nitahakikisha hilo!

Mayweather anasemekana hana shule ila hakuna mpuuzi ambaye anaweza kuonesha aina yeyote ya dharau kwake!
Usichanganye kipaji na elimu, uko umeenda mbali kwani Diamond ana hata Diploma? Lakini ni Millionaire anawazidi maisha Maprofesa wote wa Tanzania.

Ana pesa kuliko Maprofesa wote wa Tanzania.
 
True.. mtu analipa milioni 3 ama nne kwa mwaka ili mwanae ajue kiingereza tu... huku sylabus anayofundishwa mwanae wa tusiime ni ile ile ambayo wa elimu bure anafundishwa. Tofauti ni lugha tu.

Tatizo la elimu yetu ni sylabus.. jaribu kuwaza hiyo milion 3 kila mwaka mnunulie kiwanja ndani ya miaka 7 atakuwa na asset kiasi gani huyo mtoto.

Mtoto atakuwa na uhakika wa kupata elimu ya juu ama basic need hata kama mzazi umefariki...
Katika maisha kila mmoja anacho akipendacho kila mtu ampeleke mwanae shule anayopenda na hata Kama Ni ya zaid ya m 3,so wote tupelake kwa elimu bure,na pia hii husaidia walimu wetu waliokosa ajira serikali Ni kupata ajira katika hizi shule za private sector hivo mi sioni tatizo kuwapeleka uko

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi ambazo wanasoma msingi zilikuwepo tayari ila wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Mimi nilisoma shule ya Serikali miaka ile ya utawala kipindi cha kwanza cha Mwinyi. Kipindi kile, shule bora kabisa zilikuwa ni za Serikali na Seminari. Shule binafsi zilizoitwa za Wazazi hazikuwa zinafaulisha. Shule niliyosoma ilikuwa na mikondo minne ya watoto 45 kila darasa. Leo hali ikoje, kama mtoto wako hajitambui kusoma shule ya Serikali uwezekano wa kupata IV au 0 ni mkubwa sana ila shule za makanisa zinazosimamiwa vizuri uhakika wa mtoto kupa Div 1 - III ni mkubwa sana; ndio kusema wanaowapeleka watoto wao hizo shule ni maamuzi sahihi kama ada si tatizo
 
Sikuelewi unaposema mtoto wako wa Std 7 medium School Ana m Challenge Mtu wa A Level za Kata !!!
Mtu wa Combination gani ipi hasa.
Kweli?

We jamaa umekomaa combination tu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Elimu ni kubwa , the guy is talking about GENERAL KNOWLEDGE . Kwa uwezo ule wa mtoto ni something to be proud of . Tanzania [emoji1241] tena kwa sasa tuko nyuma sana kwenye elimu yetu , we need general changes kwa utaalamu mzuri kwenye KAYUMBA NA HIZI ZOTE ENGLISH MEDIUM SCHOOLS zinazotumia NECTA SYLLABUS. Wote tunafail kama taifa ila KAMA UNA HELA NI VYEMA UENDE TU HIZO ENGLISH MEDIUM kwani ni afadhali kidogo . TAKE MY WORDS . Mie nimesoma KISUTU PRIMARY SCHOOL ( kayumba ) nikawa napiga tution ya kingereza kwa Mwalimu Norah wa ACADEMICS PRIMARY SCHOOL , nikitoka tunakutana na wanafunzi wote wa International schools mbali mbali anaowafundisha kingereza na maths aisee huwezi amini katika Mwalimu aliyenisaidia sana kufika hapa nilipo ni huyu Mama , kwa kifupi i was very good in class when it comes to ngeli na other stuffs kwa kuwa mie niko sharp kidogo nilikuwa sikosekani top ten kila ya semister kufunga shule primary , nikatoka hapo nikagonga SHAABAN ROBERT SECONDARY SCHOOL , i had the best O LEVEL AND A LEVEL there , Mungu akasaidia nikapiga Chuo NEW DELHI na SASA niko BEIJING . Maisha yanasogea na ninaona Duniani kote nilipopita pita watu niliosoma nao na pia nilijuana nao MAISHANI .. JAMANI WAPENI WATOTO ELIMU BORA AT ANY COST , UTAKACHOKIPATA HUKO MBELENI hukijui , TAIFA LINAHITAJI WASOMI WENYE UELEWA MPANA NA SI STORY STORY , we are LACKING BEHIND GUYS .... WATU HUKU WAKO 6g sie tunasoma sijui utopolo gani alafu bado mnausifia
 
Mzazi unaishi mjini hao ng'ombe utawatunzia wapi? Kama umeajiriwa hao ng'ombe nani ataangalia..? So unaandika andika tu mkuu, siyo rahisi kiivyo

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Nyie mnaokaa mijini mimi niko mbwinde kilindi huku.. pigania wanao.. sio fedha yao yote unampelekea mtu awape cheti.. ukishindwa ng'ombe wapandie shamba la miti, watunzie bank hiyo milioni mbili kila mwaka, wanunulie hisa... Wanunulie ardhi.. wajengee .. sio pesa yote unapeleka apate elimu.. halafu akitoka mnakaa mnaangaliana.. ukipanda ujue kuna palizi na baadae kuna kuvuna.. sio unapanda halafu unaenda.. mazao yatadumaa, na mwisho yataoozea shambani
 
Utakuta mtu ni kapuku kabisa, hana chochote nae anashindana na wenzie mtaani kupeleka mtoto shule za kurudishwa na gari.

Ukimuuliza kwa nini usisomeshe mtoto shule ya kawaida?
Anasema siwezi kumsomesha mwanangu shule kama nilizosoma Mimi..

Sasa kama shule hizo za kayumba hazina msaada mbona wewe sasa unaweza kumsomesha mwanao,,shule ya gharama kubwa?
Je kama shule uliyosoma haikukusaidia ungewezaje kupata kazi nzr ya kuweza kumsomesha mwanao shule ya gharama Leo?
Unajichanganya au umechanganyikiwa na hoja yako!!

Unamuongelea kapuku hana chochote kwamba anashindana na wenzie kusomesha shule za gharama.

Hapo hapo unahoji kama shule aliyosoma haijamsaidia amewezaje kupata kazi nzuri!

Huyo huyo kapuku ndo huyu mwenye kazi nzuri au umeungaunga kwa gundi watu tofauti?

Hoja yako ni ya kuokoteza.
 
Back
Top Bottom