Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Uhakika wa kufaulu upo kwenye private schools. Pitia matokeo shule za serikali. Hali ni mbaya.
hayo maneno ya "ufaulu umeongezeka" yasikie hivyo hivyo
Wanafalu na maisha???? Tumieni akili
 
Bu

Huo upumbavu binafsi nilishakiri humu sitakaa nifanye [emoji16][emoji16][emoji16]! Hio hela bora umwekezee mtoto tu akija kukua mtu mzima apate pa kushika. Ni fedhea sana kulipa mamilioni kisha mtoto aje kuzunguka na kibahasha kama mwendawazimu [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ktk maisha yangu nilishasema na hata watu wanajua, watoto wangu watasoma government school, haijalishi sijui nna pesa kiasi gan hat km cha kuweza kuhimili private..

Nyumbani kwetu wazazi wangu wana uwezo mkubwa tyuuh kifedha wa kuweza kutusomesha kwenye shule za magari ya njano, ila walitupitisha ktk shule za kidumu na mifagio huku wakiweka asset za baadae kwetu na wakitiliaa mkazo ktk kupata elimu yetu,

Kwa wakati ule tuliona wazazi ni bakhili na wabinafsi kwa kutuweka shule ambazo hazifanani na uwezo wala status zao km wazazi wa watoto husika, ila leo hii tunajivunia mno tena sana. Na tunashukuru zaidi kwani wazazi walikua wanatengeneza kitu muhimu na bora kwetu.

Now nipo chuo 2nd yr, na faculty yangu n 4yrs, na nasoma kwa pesa zangu, maana sikuomba na wala kuhitaji mkopo, asset ninazomiliki binafsi, kwangu tosha kabisa ku survive maisha yangu yote, na hapa nilipo wala sitegemei ajira hapo baadae labda itokee tyuuh. Ila sio mie kuzunguka na bahasha za kakhi mtaani. Hilo halitakuwepo na halipo.

Nawashukuru sana wazazi kwa msingi huu waliouweka ambao leo tunafaidi matunda yake.
Kumbe cocastic nawe bado wakusoma[emoji4]
 
Nina Rafiki yangu hali yake ya uchumi ni ngumu sasa awamu hii. Yani hana kazi maalumu na kipato chake hata kwa mwezi hakifiki 1m. Anawatoto 3. Wanasoma private school ada 1.8 kwa mwaka. Mpaka sasa hajalipa hata 100 ya adda ya mwaka huu. Na ile ya mwaka jana alikopa kwa ndugu baada ya wanafunzi kufukuzwa. Namshaur arudishe watoto kwenye shule za kawaida ila hasikii anataka aonekane wa kishua
Huyo anafilisika anajiona
 
Mwambie kabisa wewe ni mwanaume, shida yako unadanganya watu kuwa ni demu halafu baadae kwenye simu wanakuja kugundua kuwa ni mwanaume ndipo unapoleta shida wewe kijana
Duh! Masihara haya[emoji848]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Usicheke mkuu, mtoto ana masterz anatafta kazi ya laki 3 kwa mwezi huku thamani ya elimu yake ni ya kulipwa millions.

Si aheri hizo hela ungemfungulia biashara baada ya form 4 tu. Ikisimama aendelee na mpango wa kusoma masters ila akiwa anaingiza hela zake.
 
Kama unafikir elimu ni garama jaribu ujinga.
Mi mtu anaemsomesha mwanae kwa hela nyingi kwangu huyo ndio mpambanaji. Unachotakiwa umuandae mwanao kuajiriwa popote dunian sio lazima iwe hapa. Unatakiwa ujiulize kwanini wewe uliyezaliwa nyumba ya kawaida baadae unajenga gorofa kuna nini kipya hapo? Kwanini ucjenge nyumba ya milion 40 tu safi mpaka unatumia milion mia 3 mpaka 6 kujenga makaz yako. Mi nashaur kama unaweza wekeza kwenye elim elim elim na elim isiwe hii ya bure mzee. Mtu asikudanganye elimu ni huku mwanzo kule juu unamalizia ulichokianzisha. Mi nakumbuka niliwasomesha wadogo zangu nikiwa na banda. Matokeo nimeyaona na hata nikiona mtu anamaisha mabaya ciz anasomesha mi cmlaumu. Mjengee mwanao kujiamin. Ukiangalia utawala wa nchi yetu wa sasa ni matokeo ya kutokujiamin zile shule za kajamba nani walizopitia. Muda wote anahic wazugu au wenye hela wanataka kutuangamiz. Fear of unknown. Elim elim elim.
Ni Ushamba Sana kusomesha ukiwa na lengo moja TU la mwanao kua mwajiliwa.

Mjenge mwanao awe mbunifu,ajiamini na hata aweze kujiajili.
 
Tatizo watu wengi wanaagalia ufaulubwa darasanj tu wa ma hpa ya chuo nk.

But mtoto aliesoma international schools Na aliesoma Kayumba wanatofauti kubwa sana.

Tofauti kuu ni exposure aisee without exposure katika hii dunia utasota sana tena sana

Pia circle ya marafiki anao kuwa nao maconnection kibao.
Nadhan wee ndo umeenda kdg nje ya box,

Wengi humu naona wanabishana khs private za kina St.marys na hizi kayumba za serikali

Sio hizo international
 
Shule za kata na shule za akina Tabora boys,Kisimiri,Kibaha nk msiziweke kundi moja
Shule za private za St.marrys na tussiime zisiwekwe kundi moja na kina Tanganyika international schools
 
Shule za private za St.marrys na tussiime zisiwekwe kundi moja na kina Tanganyika international schools
IST anaweza amalize aende Yale,Havard, Salford . Sio aende chuo cha Genta. BUSISI UNIVERSITY
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na ceo wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi zao ambazo walikuwa wanasoma msingi, hizo olimpio na arusha school zilikuwepo tayari ila wala hawakusoma hizo shule na leo wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za bei nafuu kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Mtoa post ana kitu huyu asipuuzwe
 
Kuna baadhi ya watu humu wanachekesha.
Msizifananishe international schools zenye mitaala ya IB, Cambridge na Mitaala hii yetu.
Pia kama kipato kipo bora kupeleka watoto huko, bond na urafiki atakao kuwa nao utamnufaisha sana baadae na hiyo ni investment nyingine tofauti na kayumba.
 
Sehemu tulipowezwa ni hapa..

Mtoto wako, anakuja kuishi Tanzania hiii hiii unahangaika awe mzungu..hahaha.. na anafundishwa matatizo ya kizungu, kwa lugha ya kizungu..akitoka huko ameshakuwa mzungu anakuja kwa watanzania mtaani anaanza moja.. 🙂

Na cha kufurahisha ni sisi wazazi ndio tunakuwa tumewanunulia watoto wetu hiyo delay huku mtaani. Elimu tuliyomnunulia ndio imekuwa kikwazo..

Bora kila mwaka ungekuwa unamnunulia mtoto ng'ombe nne.. anasoma shule ya laki tano kwa Temu.. akija kumaliza shule anakuwa na ng'ombe 68, ukiweka kuzaa na kufa hakosi ng'ombe 100 kwenye kipindi cha miaka 16 ya kusomea elimu.

Na elimu yenyewe ndio imekuwa uchuro uchoro mtupu
Kama anaishi kimara ng'ombe 68🙄🙄
 
Back
Top Bottom