Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kama sio tajiri na huna asset, kusomesha watoto shule za gharama ni ujinga unaongeza umaskini kwenye ukoo

Kunandungu yangu anasomesha kwa milion 5 kwa mwaka,watoto watatu wameanzia la kwanza private ad form four wa kwanza anamaliza mwaka huu

Hua napiga maesabu hizi milion 5 kwa mwaka Hadi wafike chuo sio chini ya milion 60 ad 80,hizi Hela ukiwanunulia madogo Kila Mmoja Kosta wakimaliza versity siwatakuja kuzipigia kazi kujiajiri kuliko kutumia nguvu nyingi mwanzo wakishamaliza utaskia mzazi anamwambia mtoto Mimi kazi yangu ya kukusomesha nishamaliza pambana kivyako
 
Mambo yanabadilika na Kila nyakati zina namna yake fanya Yake. Fanya yalio ndani uwezo wako ungekuwa umewahi kuwa kwenye panel ya interview Ukiona vijana wavyoteseka kisa lugha tu.

Hata law school pale kinachowafelisha wengi lugha inachangia . Wakenya kinawabeba lugha tu Ila wa kawaida tu Kama sisi sana

watalamu wanakubali kuwa mtoto aelewe vizuri anachofundishwa lazima afundishwe kwa mother tongue.
Nimewahi kufundisha kidato Cha kwanza yaan wtt wanateseka Sana na kukata tamaa mm nashauri serekali iitishe kura ya maoni tuamue lugha ya kufundisha primary mpaka chuo kikuu. Kwa waliowahi kufundisha watalikubali hili.
 
Noma hiv unaanzaje kumpeleka mtt wako shule ina walimu 10 wanafunzi 600+ walimu wenyewe wanamtumia mtoto wako ndo awauzie biashara zao za kababu na barafu shuleni
Hatujadharau Ila shule ya jirani hapa wapo 160 + darasani la nne wtt inabidi mzazi uwe na Muda kutosha kumfatilia mwanao Mungu amjalie ajitambue vinginevyo.
 
Ni kweli kwamba uwezo wa mtu unaweza onekana popote ila sio vibaya kumpa mwanao elimu nzuri.
 
Hii mambo ya kudiscourage watu wasisome wapate maarifa ni tabia fulani imeanza kujitokeza hivi karibuni hasa Tanzania

Hatuwezi kukaa hapa kama jamii eti tunapanga mipango ya ku-incentivize kutokusoma

Kama mtu anaweza kusoma kwa upeo wa akili yake afike level anayoitaka yeye na akienda zaidi kuwe na system ya ku-reward that maana elimu kubwa inasaidia kufanya innovation breakthrough fundamental kabisa ya civilization

Utajengaje spacecraft ya kwenda Mars au kurusha satelite ya internet communications ili tuweze kupata internet,etc bila kusoma advanced mathematics?

Kila mtu akiwa anakwepa nani atafanya?

Tutaishia kua taifa la consumption tu hakuna patents wala innovation serious we can offer the world and create wealth for the country and individuals

Elimu ni elimu tu haina shortcut,hutaenda darasani formally ila utafanya huko nje the same ili uwe na hayo maarifa....

Maarifa hayana mkato,aidha uyapate darasani au nje ya darasa


Kama hupendi mazingira ya darasa,thats on you,ila ukitaka kujua mahesabu ya kupeleka satelite kwenye orbit ni lazima usome uelewe ukiwa chini ya mti au gereji au chooni or whatever u wish!

Ila zile eliptical equations ni lazima uzipitie we dont care umejulia wapi Harvard au chooni kwenu huko madongo kuinama or whatever u call it.
Tatizo ya tz tuna watu wanamawazo ya biashara za survival mode tuu. Hayo unayosema wewe hututaki na kwa kuwa hatutaki basi tukubali kuwa watumwa wa wadhungu mpaka pale yesu atakaporudi
 
Angalia huyu mshamba mwingine huku duniani, watu wanamaanisha maisha ya mtu baadae pamoja na kusoma hizo english school na mtu aliyesoma kayumba,ukweli ni kwamba watu wa kayumba wengi ndo utakuta wanatoboa maisha, hawa wa kwenu ambo unakuta wanasoma wengine mihula ya uingereza huishiaga kwenye ubishoo tu na wanatafuta kwenda kufanya kazi nje, kule ukubwani au uzeeni wanarudi na mikogo tu ya kutembea wametanua mikono na miwani ya jua machoni huku wameacha kizazi chao kikiishi utumwani ugenini na kua wamekimbia aridhi ya uzao wao,endelea kumsifia wa kwako bado yuko darasa la 7, huyo siyo jiwe anakua, akikua utaona kitakacho tokea labda tu awe amezaliwa na utashi wa asili, vinginevyo utajuta tu maana tumewaona wengi kwenye familia na majirani
Huwaga wanawadai wazazi wao kazi..
 
Hujifunzi ndio tatizo lako.. India karibu kila State inlugha ya kufundishia.. wao waliofanya hivyo ni sisi tuliadopt kizungu nani anafanya vizuri kwenye eneo la ubunifu!?

Acha kupelekeshwa na dunia.. take a pause and think independently. Wanao unawafundisha majukumu yao ya nyumbani kwa kizungu!? Mbona wanayaelewa na wako very confident kuyaexpress kokote!?

Nakama hoja sio kuelewa.. shule wanaenda kufanya nini.. kuimba!?

Kwenye paragraph yako ya mwisho, elimu nayo ni asset. Pia curriculum na syllabuses ni zile zile.
Elimu hii hii ya kibongo mkuu?
 
Kunandungu yangu anasomesha kwa milion 5 kwa mwaka,watoto watatu wameanzia la kwanza private ad form four wa kwanza anamaliza mwaka huu

Hua napiga maesabu hizi milion 5 kwa mwaka Hadi wafike chuo sio chini ya milion 60 ad 80,hizi Hela ukiwanunulia madogo Kila Mmoja Kosta wakimaliza versity siwatakuja kuzipigia kazi kujiajiri kuliko kutumia nguvu nyingi mwanzo wakishamaliza utaskia mzazi anamwambia mtoto Mimi kazi yangu ya kukusomesha nishamaliza pambana kivyako
Hii mbinu ijaribishe kwako mkuu, yaan uanze kusave m5 kila mwaka afu ununue Costa uone kama ni rahisi, kilimo cha tikiti kwenye karatasi ni rahisi sana
 
Habari wadau..

January imeisha .. wazazi wengi walikuwa wanalalamika school fees tatizo.

Kwa maoni yangu kama mtu huna mali za kutosha, huna kampuni ya kueleweka wala huna mtaji wa kutosha... baba mzazi wewe mwenyewe unategemea ajira za laki nane ama milioni moja, kusomesha watoto wako shule za gharama sio jambo zuri.

Hakuna CEO Mtanzania ambaye ameajiriwa ambaye hayupo kwenye kampuni ya baba yake kama Mo, ambaye amesoma international schools, ama shule za bei nafuu za kiingereza ambazo tunaita english medium... tukumbuke english medium zipo Tanzania miaka kibao kama IST, Arusha school ama Olimpio.

Kuna CEO wengi wazawa kama Dada CEO wa NMB Ruth Zaipuna ama wa CRDB Majid Nsekela na ceo wengine wengi hawajapita Olimpio wala Arusha schools enzi zao ambazo walikuwa wanasoma msingi, hizo olimpio na arusha school zilikuwepo tayari ila wala hawakusoma hizo shule na leo wamepata nafasi kubwa kwa uwezo wao binafsi wa kazi..

Mzazi ambaye huna hela za kutosha peleka mwanao shule za serikali kisha msimamie mwanao vizuri, kila siku mfatilie. Hela ya ada ya kulipa Tusiime nunua asset unazozimudu mwanao zitamsaidia kuliko kumlipia ada mamilioni.
Tatizo watanzania wengi ni bendera fwata mkumbo. Hawafanyi vitu kwa kutumia akili zao wenyewe, kufanya uchambuzi wa kina na kuangalia uhalisia wa maisha yao, ndio maana mwisho wa siku, wanajikuta wana nasa. Yani watanzania ni watu wa kuigaiga tu. We angalia jinsi wanavyoigana kununua magari, kwamfano gari kama nissan dualis, subaru forester, toyota crown athlete, escudo etc etc.

Kuna watu wanachukua mikopo mikubwa mikubwa benki ili wasomeshe watoto wao shule za gharama, ili waonekane na wao wako fresh, mwisho wa siku wanaumia tu, nyumba zinauzwa na mabenki kila siku, na asilimia kubwa wanaoleta haya matatizo yote ni wanawake, wanaharibu sana watoto.
 
Hii mbinu ijaribishe kwako mkuu, yaan uanze kusave m5 kila mwaka afu ununue Costa uone kama ni rahisi, kilimo cha tikiti kwenye karatasi ni rahisi sana
Mkuu save Hela madogo zije ziwasaidie baadae kujiajiri,tatizo wazazi wamekalili mtoto asome aje kua dakatari,injinia,wakishamaliza wanabaki wanabaki wamejishikiza na vimshahara vya laki 2,kwasasa supply ni kubwa mno kuliko demands,na madogo wanafaulu kweli,wakati unasomesha usisahau kusevu Hela kwa ajili ya madogo baadae,sio unatumia nguvu nyingi mwanzoni akimaliza unamtelekeza
 
Mimi namtazamo mwingine japo sitofauti sana na wewe, mimi naona ni vyema kipindi hichi wazazi wenye kipato cha kawaida wakawa na malengo ya kuja kuwekeza zaidi kwa watoto wao kwenye elimu ya juu huku chini hakuna haja sana sababu watoto wanaishia kujua lugha tu.
Me nadhani bora huku kwenye elimu ya chini ndo uwekeze zaidi kwa mtoto uko juu anakua tayari keshajitambua lkn pia anamsingi mzuri uliomjengea tangu awali anaweza akaandelea vzr tuu
 
Mshahara haueleweki, unakuta mtumishi anasomesha watoto watatu shule ya mabasi ya njano, Kivumbi na jasho.

Sehemu nyingine familia haina kipato Cha uhakika mathalani ni wafabiashara ndogondogo nao huingiwa na ulimbukeni kupeleka watoto huko matokeo yake ni madeni na maisha ya aibu.

Wazazi wengine huenda mbali zaidi mpaka kuuza ardhi ya familia Ili wapate ada ya shule.
 
Mkuu

Hii kitu Huwa nabishana Sanna na staff members pale kazini!!

Conservatives wananiona mkoloni,lakini nawaambia Mungu ni tajiri Dana hajaumba Kila Binadamu lazima afike chuo kikuu,lazima awe na vyeti fulani fulani!

Wengine watakula Kwa vipaji vyao kama ufundi,biashara na mengineyo sio lazima uue kipaji Cha mtoto Kwa kukaa shuleni miaka 16 ahitimu degree!!

Wananiona mshamba sana!!

Mi nawaambia live nimezaa watoto sio lazina wooote waende chuo kikuu wengine wataishia vyuo vya ufundi wengine form four na wengine wataenda Hadi huko.versity watafanya kazi za kujiajiri na frem na location nishajenga njia panda muda ukifika TU nawaondoa wapangaji na wao wataanza Biashara zao rasmi waingie kwenye mfumo wa ujasiria mali!!

Huu ujinga wa kulemaza vipaji vya watu Kwa elimu ya kukariri Hadi versity ni ujinga was karne wasome wenye vipaji sio kulazimisha kila mtu!!
Namba moja naomba ukiwa nikumbuke kwenye uwaziri wa afya hakika una kitu na utafika mbali

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mambo yanabadilika na Kila nyakati zina namna yake fanya Yake. Fanya yalio ndani uwezo wako ungekuwa umewahi kuwa kwenye panel ya interview Ukiona vijana wavyoteseka kisa lugha tu.

Hata law school pale kinachowafelisha wengi lugha inachangia . Wakenya kinawabeba lugha tu Ila wa kawaida tu Kama sisi sana

watalamu wanakubali kuwa mtoto aelewe vizuri anachofundishwa lazima afundishwe kwa mother tongue.
Nimewahi kufundisha kidato Cha kwanza yaan wtt wanateseka Sana na kukata tamaa mm nashauri serekali iitishe kura ya maoni tuamue lugha ya kufundisha primary mpaka chuo kikuu. Kwa waliowahi kufundisha watalikubali hili.
Point nzuri sana
 
Back
Top Bottom