Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!

Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!

Hi stori in fact ni kinyume.
Na mengi kakuruouka tu au wanajuana na mchapishaji wa hilo gazeti.
Kawaida mengi alitakiwa alikomalie gazeti lakini yeye ameenda kwa kumtaka kikwete akanushe. Kitu ambacho hakiwezekani .
Yeye anatakiwa alishtaki gazeti ila hakufanya hivo .
Sasa hapa labda mengi anatumiwa na chadema au Rugemalira. Tukumbuke bado Ruge anazoo centi za Escrow .
Leo zitto atazungumza hili hivo tusubiri
..ona sasa vichwa panzi vya hawa baadhi ya wanachichiem!! ccm ya ukweli(ya kina mzee warioba) mnatakiwa mfukuze huu uchafu wa namna hii kutoka chaman kwa sababu ndo unaokichafua na kukididimiza hicho chama kila kukicha. hivi wewe crabat kati ya mengi na ikulu nani mwenye status zaidi? kwa hiyo ikulu kuchafuliwa wewe unaona sawa ikae kimya ila mengi harakaharak ndo unamwangushia mzigo wa kuprove???!!! yaan nyie watu mmeishusha sana hadhi magogoni, mnapaona kama kibanda cha bibi kizee kule kijijini. Ina maana wewe hushtuki ukisikia "ikulu ya nchi" inatajwatajwa kwenye mambo ya hovyo hovyo kama haya ya huyu msaliti zitto? yan hushtuki kabisa??!!! Huoni kwamba "ikulu ya nchi" ina duty na right ya kutoa ufafanuzi wa mambo kama haya haraka? hivi wewe huna hata chembe ya uzalendo ilokusalia?!! au wewe unafikiri ikulu ya nchi ni hizi nyumba zetu tunazojenga huku mtaani?

hopeless...
 
Hakika Bavicha wana ugonjwa wa kusahau...ndio maana wameamua kuungana na madisadi kumchafua Zitto.

kila kitu lawama kwa bavicha...utajaingiza bavicha ktk family issues,umekua sasa acha utoto kwa ufinyu wa fikra
 
Wanabodi,

Mimi ni muumini wa kitu kinachoitwa "karma" ambayo ndio hukumu pekee ya haki hapa duniani!. Hii karma wakati wa kuhukumu, haina huruma kwa sababu hukumu zake ni za haki, unaweza kulipa mema, au kupigwa na mapigo ya kufidia uovu!.

Karma ni powers of 'cause and effects' ambapo ukitenda mema, utalipwa mema, na ukitenda uovu utaadhibiwa kwa uovu wako.

Chadema walipomtimua Zitto kwa tuhuma za usaliti, nilisema humu kama kweli Zitto ni msaliti, then 'karma itamshughulikia Zitto na kumuadhibu, lakini kama Chadema haikumtendea haki Zitto, then Chadema itaadhibiwa kwa hukumu kali ya 'karma'.

Ni muda mrefu kumekuwa kukitolewa tuhuma mbalimbali kumhusu Zitto na zote kwa sababu ni tuhuma tuu, ama hukanushwa, au kupanguliwa kisha maisha yanaendelea.

Sasa kuna hii tuhuma mpya nimeisoma kumhusu Zitto.


Mpaka sasa, tuhuma hii, haijakanushwa na Zitto mwenyewe, wala haijakanushwa Ikulu, na huku hilo gazeti lilitochapisha tuhuma hiyo, likiachwa kuendelea kupeta!. ----------- lilipochapisha tuhuma kama hiyo, kesho yake tuu Ikulu iliiytisha press conference kukanusha na haikupita wiki, ----------- lilifungwa kifungo cha milele hadi leo!.

Sasa kama tuhuma hii ni kweli, then kwa mujibu wa reference ya 'karma', Zitto ni kweli atakuwa ni msaliti, na sasa kiuhakika kabisa bila kupepesa macho, wala kumung'unya maneno, "Huu sasa ndio mwisho rasmi wa Zitto Zuberi Kabwe!".

Nimesema huu ndio mwisho rasmi wa Zitto kwa sababu kuna watu kwanye jamii yetu, wamejaaliwa karama mbalimbali hivyo kuwa ni watu very powerful kwa nguvu ya 'karma' ya mema yao!. Sasa inapotokea mtu akatofautiana nao kwenye public, hadi kufikia kunyoosheana nao vidole kwenye media!, kama tuhuma hizo alizomsingizia Mengi ni kweli, then atasalimika, lakini kama sii kweli, that is the end of him!.

Kitendo cha Zitto kumsingizia Mengi, jambo kubwa kama hili (if he really did this), then this is the end of Zitto.

Hakuna hata mtu mmoja ambaye aliwahi kukorofishana na Mengi publicly akabaki salama!.

This is the list ya watangulizi wa Zitto angalia walifanya nini na nini kiliwatokea!.



  1. Alipishana kauli na wamiliki wa DTV na CTN kuhusu haki za kuonyesha kombe la dunia, vituo hivi vyote vimekufa.
  2. Alipishana kauli na Shabir Dewji kuhusu wahindi kupendelewa, Shabir Dewji aliswekwa lupango na sijui siku hizi yuko wapi?!.
  3. Alipishana kauli na Katibu Mkuu, Mambo ya Ndani, Silvanus Adel alipomtoa Dewji lupango, Adel alimwaga unga wake!.
  4. Alipishana kauli na mmiliki wa Gazeti la Mtanzania, Generali Ulimwengu, kwa gazeti hilo kutoa siri kuwa Mengi anadaiwa na mabenki. Generali alifutiwa uraia na gazeti la Mtanzania likafilisika hadi kuuzwa!.
  5. Alipisha kauli na Lowasa, Mengi akiwa Mwenyekiti wa NEMCI, Lowasa akang'oka!.
  6. Alipishana kauli na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Shamin Khan, shamim aling'olewa!.
  7. Alipishana kauli na Waziri wa Utawala Bora, Wilson Masilingi, kuhusu "mchezo mchafu" wa ubinafsishaji wa Kilimanjaro Hotel, Masilingi aling'olewa!.
  8. Alipishana kauli na Iddi Simba kwenye mambo ya Uzawa, Iddi Simba alimwagwa!.
  9. Alipishana kauli na Basil Mramba akiwa waziri wa fedha kuhusu kodi ya Jack Pot Bingo, Mramba aling'oka!.
  10. Alipishana kauli na Adam Malima, almanusura Adam, yangemkuta, Sitta akamuombea msamaha!, ndio salama yake!.
  11. Alipishana kauli na Tido kuhusu TV inayolipwa na kodi za wananchi kugombea matangazo na TV binafsi!, Tido aling'oka!.
  12. Alipishana kauli na Waziri wa Mambo ya ndani, kuhusu 'mademu!', Masha, Masha kang'olewa!.
  13. Alipishana kauli na Mmiliki wa Channel Ten, Franco Tramontano, kugombea mademu fulani mamiss, Franco alikamatwa na kutupwa selo akisubiri deportation ya interpol
  14. Hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Sabas kiwango, alizuia Tramontano asiwe deported, Kiwanga akamwaga unga!.
  15. Akapishana kauli na Rostam Aziz, kwenye issue ya 'fisadi papa na fisadi nyangumi', Rostam alitimuliwa ubunge na sasa ameikimbia nchi!,
  16. Alipishana kauli na Balozi wa Uingereza kwenye kashfa ya Silvadale!, Balozi wa Uingerezwa aliondoshwa!.
  17. Alipishana kauli na Yusuph Manji, kuhusu Manji kuifilisi mifuko ya hifadhi za jamii, sasa soon Manji atafilisiwa!.
  18. Manji alipomfungulia Mengi kesi ya kumdai shilingi 1!, Wakili wa Manji, Sabas Kiwango alipishana kauli na Mengi, Kiwango akasitishwa uwakili!.
  19. Akapishana kauli na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhondo kuhusu wawekezaji wazawa kwenye issue ya gesi asilia, Prof. Muhongo katimuliwa uwaziri.
  20. Alipishana kauli na Mkurugenzi Mkuu, TPDC, Yona Kilaghane kuhusu kuweka masharti nafuu wazawa kumiliki vitalu vya gesi, Kilaghane ametimuliwa TPDC!.
  21. Alipishana kauli na wandeshaji wa Kipindi cha "Kiti Moto", Kiti Moto kilikufa.
  22. Alipishana kauli na 'mtangazaji mmoja maarufu' ambaye Mengi alimtaka ajiunge na ITV, huyo mtangazaji akagoma, mpaka leo huyo mtangazaji ni 'majalala', hoin bin taaban na hajawahi kupata tena ajira popote!.
  23. Alipishana kauli na mrembo Madam Ritta kuhusu mambo binafsi, sijui kwa sasa Madam Ritta ana hali gani?!.
  24. Alipishana kauli na Mrembo Madam Lily, katika mambo binafsi!, sijui majaaliwa ya huyu mrembo kwa sasa!.
  25. Sasa ndio amepishana kauli na Ziito Kabwe, tusubiri nini kitamtokea Zitto and it is soon!

NB. NB. Kama yote yanayosemwa kumhusu Zitto sii kweli kuwa ni msaliti, na haya Zitto aliyoyasema kumhusu Mengi ni kweli, then Zitto ataendelea kudunda na ACT yate itazidi kuja juu 'karma' sasa itaishughulikia Chadema hali kadhalika itamshughulikia tena Mzee Mengi kama ilivyokwisha mshughulikia kwa mengine kule nyuma!.

Uzuri wa karma, ikikushughulikia na kuanguka chini, ukimaliza kukulipa deni la adhabu ya karma ambayo huwa ni kupata mapigo, then unaweza kusimama tena, kunyanyuka na kuendelea kung'ara!.

Pasco
Pasco wakati mwingine nakukubali na wakati mwingine sikuelewi au wewe ni nyoka mwenye makengeza. Hongera kwa uzi huu
 
Kama hii habari niya kweli sasa tusubiri ligi yake Mengi nani atanyoosha mikono


Duh mkuu ligi ya Zitto na Mengi hujui nani atashindwa??

Mswahili....mpuuzi na masikini Kama Zitto anaweza shindana na Mengi??

He is just a smaller dog !!!!

Amekwisha!!!!!!
 
Wakati Zitto anawasilisha ripoti ya PAC bungeni rais Kikwete alikuwa Marekani kwenye matibabu.

Huu sio ulimwengu wa analogia bali ulimwengu wa digital. Tunapojadiliana wewe Ritz na mimi hatujakaa meza moja ndicho kinachoweza kutokea Zitto kumfikishia kikwete habari hizo.
 
Huu sio ulimwengu wa analogia bali ulimwengu wa digital. Tunapojadiliana wewe Ritz na mimi hatujakaa meza moja ndicho kinachoweza kutokea Zitto kumfikishia kikwete habari hizo.

Mkuu wangu uwezo Wa kufikiria ulioufikia wewe huyo KENGE hana!!!!

Labda kuisoma ile minyoo yao hapo utampata lakini kwa issue hiyo he is too low!!!
 
Duh mkuu ligi ya Zitto na Mengi hujui nani atashindwa??

Mswahili....mpuuzi na masikini Kama Zitto anaweza shindana na Mengi??

He is just a smaller dog !!!!

Amekwisha!!!!!!

Wachaga wana madharau ! wewe kwa Mengi ni tajiri mwenzio au mlinzi wake ?......au kanguruwe fulani hivi ? lusungo
 
Last edited by a moderator:
Namwona kwa mbaliiii zitto akielekea kuwa another new mrema hahahahah ni bora akaacha siasa tu

Mrema ametengeneza history ktk nchi hii.amepata cheo ambacho hakipo kikatiba na dunia itamkumbuka kwa hilo.we masaburi umeacha nn
 
Kama kweli Zitto kafanya hivi, then si mwanasiasa mzuri na makini. Pia atakuwa hana akili kabisa, nasi tunajua anazo akili.
Lakini kama hizi tuhuma si za kweli kwa nini hajakanusha hadi Leo? Ukimya ina maana unakubaliana na kilichosemwa kutegemeana na unyeti Wa jambo. Hili ni jambo nyeti ambalo hakupaswa kulifumbia macho.
 
babu anatafuta kick,ngoja jion utaskia mwanaume atakavyojibu kiuungwana,babu chezea wote sio huyu nyerere wa pili utauza had huyo mjukuu wako uliemuoa juzi.

Ni mwenye mtindio wa Ubongo pekee atasema kuna mtu ana sifa za Nyerere wa pili. Huyu mpenda sifa hana hadhi hiyo! Never on earth!
 
Pasco, wakati huu wachaMungu wamezama katika maombi wakimlilia Mola atupatie Rais BORA! Huyu Zitto yumo TANURUNI na akivuka salama yeye ndiye Rais ajaye, utamsikia tu Lubuva kwa uwezo wa Mungu anaahirisha uchaguzi ili matakwa ya KATIBA yatimilizwe!
 
Wachaga wana madharau ! wewe kwa Mengi ni tajiri mwenzio au mlinzi wake ?......au kanguruwe fulani hivi ?
. mkiambiwa mfanye kazi na kujisomea hamtaki, mmebakia tu kutangaza udini na ukabila, kazi hamfanyi, shule hamtaki kwenda. mnataka wao wachaga wafanyeje? kwa hiyo wachaga waache kujitafutia maisha ili wawe sawa na wavivu ninyi msiotaka kufanya kazi mmekalia kueneza siasa za udini, ukanda na ukabila??!! mtavuna mnachopanda. lakni hata muwachukie vipi wachaga watabakia kuwa wachaga tu. makabila ya stahili hii yapo kila nchi duniani. hapo kenya wapo wakikuyu. bahati nzuri mliyonayio wachaga hawana roho mbaya na hawana ukabila. mkitaka kujifunza kwao nendeni tu, ilmu mtapewa bure.
 
Last emperor;Inamaana ni kwamba hujui kiswahili au unataka kutuonyesha unajua viingereza vingi vya kuokota maneno kwenye dictionary? Acha mbwembwe dogo.. Unataka watu wakuone umesooma!

=Is your head okay?
 
Hakuna lolote Pasco , kuna wengine umewataja hapo lakini wako vizuri tu upande mwingine wanakula good time! ila siamini hayo kama kweli Zitto kamsingizia!
 
Last emperor;Inamaana ni kwamba hujui kiswahili au unataka kutuonyesha unajua viingereza vingi vya kuokota maneno kwenye dictionary? Acha mbwembwe dogo.. Unataka watu wakuone umesooma!

=Is your head okay?
i don think so, he is symbolizing his mabosity too much!!
 
Back
Top Bottom