Kama tuhuma hii ni kweli, then this is The End of Zitto. Karma Ndio Itamaliza Kila Kitu!

Kwa hiyo kijana bila kujisalimisha, angemfuata aliemtuma siyo?
 
Asiyeweza jitetea!!!?[emoji15]

We ulitaka ajitetea akiwa hai kwani yule jamaa ana simile basi

Unadhani angembakisha hapa duniani!!!?

Acha aongee maadam ni muda sahihi yeye kuongea.

Wote walioongea neno dhidi ya kiumbe yule alijitetea kwa mabavu aidha walipotea kwenye uso wa dunia au waliishoa jela

We mwenyewe ni shuhuda wa lile swali ulilomuuliza pale magogoni ukihoja anayoyafanya kama ni kwa mujibu wa katiba na ukijiba kisanii "MAYALLA kwa kizilaNKENDE maana yake njaa..!?

Halafu ukaitwa dodoma na yule mgogo

Uliporudi toka kule ukawa kam roboti la matope[emoji2]

Hitler tunamnga hadi leo seuze huyo jamaa yenu[emoji849]
 
Muongo huyu Yan amiri jeshi mkuu atumie vijana wa mitaani Yan haogope kutoa amri kwa mkuu wa magereza, mkuu wa polisi mkuu wa majesh mkuu wa usalama, mkuu wa jkt

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu JPM ndo hayupo, ulitaka huyo mtu aliyechoma moto nyumba na shamba ajitokeze kabla JPM hajafa?
 
Mkuu JPM ndo hayupo, ulitaka huyo mtu aliyechoma moto nyumba na shamba ajitokeze kabla JPM hajafa?
Ukipewa tuhuma zozote za mtu yeyote aliye hai, unapaswa kumface na kumweleza, akifa kabla hujasema, then you just can't, you just take it a secret and you go with it to your grave!.
P
 
Ukipewa tuhuma zozote za mtu yeyote aliye hai, unapaswa kumface na kumweleza, akifa kabla hujasema, then you just can't, you just take it a secret and you go with it to your grave!.
P
No no no!
Wahanga wa Hitler walipewa nafasi nzuri tu, tena kimahakama, kueleza madhira yaliyowapata wakati wa Nuremberg Trials, baada ya mauaji ya kutisha 1945.
Huyo kijana aliyejitokeza kuomba radhi ni lazima nafsi ilikuwa inamsumbua na alikuwa na ile inaitwa PTSD(POST TRAUMA STRESS DISORDER).
Wengi wanaotumwa kazi hizo chafu si kwamba wanapenda, na nafsi zao zinaugua.
Ndio maana hata kule Afrika Kusini, Recoinciliation Commission ilisaidia sana kuondoa hisia chafu na mbaya za revenge.
Zitto angeweza vile vile kusamehe na kupeleka mahakamani suala hili, for records purposes.
 
Nime note Zitto anatajwa tajwa sana humu jukwaani, nikaona na mimi nijikumbushe niliwahi kuandika nini kumhusu mtu huyu.
All and all, huyu Zitto sio mtu wa mchezo mchezo, he is a man to watch very closely!, sio mtu wa kawaida!.
P
 
Hivi hiyo "laana' au "karma" huwapata tu watu kwa kuwa tu fulani wewe Pascal Mayalla umsema, au..?

CHADEMA ni karma gani inayowatandika kwa mfano...?
Mkuu The Palm Beach, karma is the law of cause & effects kwa kuhukumiwa kwa matendo yako, ukitenda mema, unalipwa mema, na ukitenda uovu unaafhibiwa!.

The biggest toll ya karma ni kifo.

Kila binadamu kuna mazuri yake na mabaya yake, akitenda mema anabarikiwa, akitenda maovu analaaniwa. Kila kitu kinachomtokea binadamu hapa duniani ni matokeo ya matendo yake.

Kwa upande wa Chama, pia kuna karma za taasisi na karma za viongozi wa taasisi ambazo ndio watoa maamuzi. Taasisi inapotoa maamuzi ya dhulma, taasisi inaadhibiwa na watoa maamuzi nao wanaadhibiwa individually!, wakati wale wanao dhulumiwa karma ikiwafidia kwa kuwabariki.

Angalia baadhi ya viongozi wa Chedema waliofukuzwa bila kutendewa haki, baada ya kutimuliwa Chadema au kujitoa Chadema, angalia walikuja kuwa wapi?.

Angalia ma sterling wa matukio haya kilikuja kuwakuta nini?.

Angalia hali ya sasa ya Chadema kama Chama kikuu cha upinzani huku bara, amini nakuambia mwisho wa siku, Chadema itafanikiwa kuwatimua hawa makamanda mabinti 19 lakini machozi yao jasho na damu walioigharimikia Chadema, hayatapotea bure!, there is a price to pay and Chadema will pay dearly!.

Kwa vile Chadema inayo katiba yake na imeweka taratibu za haki kabisa kushughilikia nidhamu, zikiwemo mamlaka tofauti tofauti za nidhamu kwa viongozi tofauti tofauti, kwanini hazifuatwi?.

Mfano wakati wa kumtimua Zitto, Zitto alikuwa NKM, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu na mamlaka yake ya rufaa ni Mkutano Mkuu, mamlaka ya CC ya Chadema ni kumsimamisha tuu na sio kusikiliza shauri lake!, sasa hiyo CC ya Chadema ilimtumua Zitto kwa mamlaka gani?. Angalia Zitto baada ya kutimuliwa alikuwaje na angalia yule sterling wa kutimuliwa Zitto nini kilikuja kumkuta?.

Angalia Kitila Mkumbo baada ya kutimuliwa Chadema alikuja kuwa nani?.
Angalia Juliana Shonza baada ya kutumiwa Chadema alikuja kuwa nani

Hivyo kiukweli kabisa karma ipo and it acts upon us kwa matendo yetu!.

P.
 
You are very wrong, either purposely au dhamira yako inakuongoza hivyo. Kwa sababu binadamu ni mtumwa wa dhamira yake.
Hakuna karma yeyote iliyomkuta kiongozi yeyote wa CHADEMA zaidi ya matendo ya kikatili yaliyofanywa na viongozi wa serikali ya CCM dhidi yao.
Viongozi wa CHADEMA waliotimuliwa kwa usaliti walilambishwa asali na mamlaka iliyowatuma kwa kupewa nafasi za teuzi za uongozi, na kama hii kwako ni malipo basi you are deluded au ni kiwango kikubwa cha unafiki kinachokupofusha.
CHADEMA kiko imara mioyoni mwa wananchi licha ya figisu kutoka kwa viongozi wa serikali ya CCM, kubambikiwa kesi za ugaidi na watawala, kushambuliwa, kuzuiwa kufanya siasa kinyume na katiba kama kwako ni karma basi you are worse kuliko muuaji mwendazake.
Kama CHADEMA haifuati katiba yake katika kushughulikia uendeshaji wake Zitto baada ya kufukuzwa alivyoenda mahakamani iliamuaje? Au na mahakama nayo itakumbwa na karma?
Kama Kitila suala lake kwenda ACT hadi kupewa nafasi ya uongozi na dikteta na kupitishwa kuwa mbunge wa CCM kwenye uchafuzi wa 2020 ni malipo ya karma basi nimeamini karma itakuwa ni uchawi wa kisukuma
 
Uteuzi wa hawa mabinti 19 walioteuliwa na kupitishwa kuwa wabunge kinyume na katiba ya CHADEMA, waliopitishwa na CCM kwa maslahi ya CCM kwa kuvunja katiba ya nchi na ya CHADEMA karma ije iwalipe?
Aliyekuwa Magereza kwa kesi ya kubambikiwa na watawala atolewe gerezani usiku kinyume cha sheria akaapishwe kinyume cha sheria na CHADEMA inayotetea haki yake kama chama iadhibiwe na karma uko serious kweli?
Karma itakuwa ni uchawi wa kisukuma
 
Unajua hata maana ya "karma" kweli wewe...?

Yaani wewe Pascal Mayalla unavizia wenzako porini unawakata mapanga au unawapiga risasi kijambazi jambazi halafu wewe huyo huyo unakwenda mitaani na kipaza sauti una - shout kuwa

".....oooh, jamani eeeh karma inamtandika huyo......!!!???"

Really? Really? Yaani wewe na shahada yako ya chuo kikuu unatetea ujinga kwa hoja hizi...?

Bila shaka, kama ndivyo, basi mtu huyu atakuwa ni shetani ahamishiaye uovu wake alioutenda tangu mwanzo kwa wanadamu na kujifanya yeye huyohuyo anawashitaki kwa Mungu...!

Haya ndiyo mawazo yako na hiki ndicho unachojaribu ku - justify hapa...

Yaani hata kama ni propaganda basi unazifanya kijinga na kitoto sana...

Kwanza inakuwaje unaingiza ishu ya katiba ya CHADEMA kwenye kesi mbalimbali za wanachama wake wakosefu huku ukijua kabisa katika kesi zote hizo hakuna hukumu ya mahakama hata moja iliyowahi kui - disqualify ibara au kifungu chochote cha katiba hiyo ya CHADEMA ili kuwapa ushindi waliokuwa wakiegemeza utetezi wa makosa yao kwenye maeneo hayo ya katiba...!
 
Zitto anajulikana mpaka kwa walio mkiza kuwa ni msalti na mjanja mjanja . kwahivo haiwezi kuwa ajabu leo.
 
Kumsingizia kitu cha uongo, kumchafua marehemu, asiyeweza kujitetea...
karma yake ni usipime!.
P
Amesingiziwa nini kwa mfano..?

Wewe Pascal Mayalla ukifa ndiye utakuwa marehemu maana Tanzania na watanzania hawakujui kwa sbb huna maslahi nao na hujawahi kuwahusu...!

Lakini John P. Magufuli yeye si marehemu, maamuzi na matendo yake mbalimbali juu ya nchi na taifa hili yanaishi na yako recorded na yalituhusu kwa kutuathiri positively au negatively...

Watetezi wake (JPM) wapo. Ni nyie na hiyo ndiyo inayothibisha kuwa hajafa huyo, yupo aishi...

Lakini shida ni utetezi wenu hauwezi kufuta rekodi mbaya ya maamuzi na matendo yake. Watoto wa mjini wanasema, hamna uwezo wa kushinda mechi kwa sbb timu yenu haina uwezo...!
 
Huyu amekuwa ni mnafiki na nimekumbuka kuna mtu amesema kuwa ili uwe chawa lazima uwe muongo muongo, mnafiki, mpambe mwenye hila na inawezekana na ushirikina juu.
Nahisi mengi ya haya Pascal Mayala atakuwa na sifa hizi. Haaminiki amepofushwa sababu ya upambe
 
Kumbe issue ya EK ilianzia hapa, Gazeti la HabariLeo lilivyoripoti juu ya kukamatwa mwandishi Erick Kabendera mwaka 2013
Alimkorofisha huyu mzee, ukimkorofisha tuu, huyu mzee, unalo!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…