Mkuu
The Palm Beach, karma is the law of cause & effects kwa kuhukumiwa kwa matendo yako, ukitenda mema, unalipwa mema, na ukitenda uovu unaafhibiwa!.
The biggest toll ya karma ni kifo.
Kila binadamu kuna mazuri yake na mabaya yake, akitenda mema anabarikiwa, akitenda maovu analaaniwa. Kila kitu kinachomtokea binadamu hapa duniani ni matokeo ya matendo yake.
Kwa upande wa Chama, pia kuna karma za taasisi na karma za viongozi wa taasisi ambazo ndio watoa maamuzi. Taasisi inapotoa maamuzi ya dhulma, taasisi inaadhibiwa na watoa maamuzi nao wanaadhibiwa individually!, wakati wale wanao dhulumiwa karma ikiwafidia kwa kuwabariki.
Angalia baadhi ya viongozi wa Chedema waliofukuzwa bila kutendewa haki, baada ya kutimuliwa Chadema au kujitoa Chadema, angalia walikuja kuwa wapi?.
Angalia ma sterling wa matukio haya kilikuja kuwakuta nini?.
Angalia hali ya sasa ya Chadema kama Chama kikuu cha upinzani huku bara, amini nakuambia mwisho wa siku, Chadema itafanikiwa kuwatimua hawa makamanda mabinti 19 lakini machozi yao jasho na damu walioigharimikia Chadema, hayatapotea bure!, there is a price to pay and Chadema will pay dearly!.
Kwa vile Chadema inayo katiba yake na imeweka taratibu za haki kabisa kushughilikia nidhamu, zikiwemo mamlaka tofauti tofauti za nidhamu kwa viongozi tofauti tofauti, kwanini hazifuatwi?.
Mfano wakati wa kumtimua Zitto, Zitto alikuwa NKM, kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu na mamlaka yake ya rufaa ni Mkutano Mkuu, mamlaka ya CC ya Chadema ni kumsimamisha tuu na sio kusikiliza shauri lake!, sasa hiyo CC ya Chadema ilimtumua Zitto kwa mamlaka gani?. Angalia
Zitto baada ya kutimuliwa alikuwaje na angalia yule sterling wa kutimuliwa Zitto nini kilikuja kumkuta?.
Angalia
Kitila Mkumbo baada ya kutimuliwa Chadema alikuja kuwa nani?.
Angalia
Juliana Shonza baada ya kutumiwa Chadema alikuja kuwa nani
Hivyo kiukweli kabisa karma ipo and it acts upon us kwa matendo yetu!.
P.