Kama ukiwa huna Bahati (luck) utatumia nguvu nyingi sana kwenye mambo mengi

Kama ukiwa huna Bahati (luck) utatumia nguvu nyingi sana kwenye mambo mengi

Unakosea etu wachaga Wana bahati sana unakosea sana mtu wangu tuko nao Wana njaa kibao

Usiingize kabila mzee Kuna vingi katika utajiri japo bahati nakubali 100% mi nilishwai kuwa na bahati namshukuru mungu kwa hapa nilipo

Wachaga hawana bahatu bali waliingia kweny system na kuungashana went bahati ni wale labda wanatokea Yale makabila na background hazijulikani na wanafika mbali
Hana mawazo huyu yeye anaona gepu lililokuwepo la kielimu Kati ya wachaga, wanyakyusa na wahaya dhid ya makabila mengine ni bahati? Huyu jamaa Kuna vitu havijui mm simlaumu
 
Mimi sipendi sana kuzungumzia makabila. Ninaishi Kilimanjaro, huwa nikiona mtu anasifia Wachagga kwa Mambo fulani namuona Kama mpumbavu ambaye hajawahi kutoka kwenye comfort zone yake.

Ukweli ni kwamba Wachagga wanazaliwa wakiwa katika mazingira ambayo yanawalazimisha kupambana kufa na kupona na kuthamini unachotafutaa kwasababu wanaona.

Uchaggani Hakuna ardhi kabisa na ardhi nzuri pia ni kidogo mnoo.

Kwahiyo, unazaliwa kwenu tu Hakuna ardhi na hata kama ukipewa wanaita Kihamba Ni kidogo na mkiwa wengi ni balaa zaidi.

Sometimes, Mzee wako anakupq anakwambia Jenga Happ, Kama huna kitu unajenga nyumba ya tope au mbao kulinda Kiwanja.

Huku Hakuna mtu atalia siku ya msiba wako, watu watajaa tu kuja kula na kunywa na kurithi ulicho acha.

Kama huna kipato huku uchaggani utazikwa Kama Mzoga wa mbwa Koko maana Hadi kaburi watu mpaka walipwe ndio wachimbe.

Na ndio maana mchagga Yuko tayari hata kuua watu ili apate pesa.

Kwenye system wengi walking enzi za Mkapa kupitia mke wa Mkapa.

Enzi hizo, Rais Mkapa mke wake ( Mchagga) halafu, Waziri Mkuu Sumaye na Waziri wa fedha Ni FISADI Mramba. Kwanza Rami ilipelekwa kibabe mpaka huko vijijini Rongai, Chaka poli karibu na Kenya.

Kwahiyo, katika mazingira hayo sioni Kama Kuna bahati yoyote.

Mchagga akitoka Old Moshi Hana ardhi, akifika Kishapu huko ardhi tele, na kwasababu thamani yake ananunua eneo kubwa sana analima, anafuga Nguruwe, ng'ombe na mbuzi. Huku akowa na biashara ya muda ana biashara ya Bar na Duka huwezi kusema Ni bahati.

Ni Mapambano yanayotokanq na kumbukumbu mbaya na uzoefu wa alikotoka.
Agreed 100%.

Hiyo laini ya mwisho nakubaliana nayo sana mkuu
 
Mhubiri 9:11 Nimeweka na andiko kutjibitisha mada hii.
 
Mengi uliyoandika ni sahihi, bahati inakuwa underrated sana kwenye mafanikio wa wanadamu.
Katika haya maisha kama huna Bahati mambo mengi sana utatumia nguvu

Hata kazin kama huna Bahati kupandishwa cheo itakua mtihani wanaweza wakaja wafanya wapya wakapewa vyeo kabla Yako mambo mengine sio uchawi Bali wanakua na bahati

Mfano kwa dar es salaam ukianzia mbezi, ukaenda buguruni mpaka kariakoo utaona watu wanavyopambana na maisha point yangu ni kwamba kupambana na huna Bahati utatumia nguvu sana

Ukija kwa wachaga wamefanikiwa sana ila wale watu wanabahati ambayo Haina maelezo sio kwamba makabila mengine hawajitumi Bali hawana Bahati

Ukija kwa wazungu ni kweli wanaakili sana ila wana Bahati sana Kuna mambo hawatumii nguvu kuyaelewa ni tofauti na race nyingine

Ukija kwa wanawake kama huna Bahati nao utatumia nguvu nyingi kuwapata na watakusumbua sana, Kuna jamaa ni wakawaida Ila mkienda nae sehemu mademu wa zuri Wanashobokea Sana Mara wanamfananisha ni basi tu waongee nae

Kuna watu wengi wanamaisha ya kawaida sio kwamba hawajitumi wanafanya sana kazi kwa bidii Ila hawana bahati
 
Nyota ni upuuzi, bahati ipo.

Kukutana na watu sahihi nayo ni bahati, unaweza kuwa unamalizia chuo ukakutana na muajiri wako wa baadaye kwa bahati katika kupiga story akakuelewa akakuambia ukimaliza chuo uende akupe kazi wakati kuna watu wamemaliza muda mrefu chuo na kila siku wanaomba kazi kwenye hiyo kampuni yake bila mafanikio.

Kuzaliwa kwenye familia bora yenye maisha mazuri inayoweza kukusomesha elimu bora na kukupa kazi bila kusumbuka ni bahati tu.

Kuzaliwa na kipaji fulani ambacho kinaweza kukupa mafanikio kama Samatta au Diamond ni bahati.
hakuna kitu kinaitwa bahati wala nyota acheni kukalilisha watu upuuzi ninachojua dunia inataka juhudi na ukutane na watu sahihi enough
 
Kwa nini wengine wenye juhudi zaidi yake kazini hawakutani na watu sahihi?
Hiyo siwezi kutafsiri kama ni bahati mkuu labda kwa upande wako maana sijajua wewe hiyo umetoa wapi ! lakini mimi nilichokiona hapo ni juhudi yako kazini na ulikutana na mtu sahihi enough

Closed
 
Hakuna njia zozote unazoweza kufanya ili bahati ikifukie.
Ukiwa na bahati ni jambo zuri sasa ishu nyingine bahati inakuja vipi kwako au ni njia gani za kukufanya uwe na bahati (ngekewa) wataalam waje watusaidie [mention]Mshana Jr [/mention]
 
Uko sahihi
mkuu bahati huwa inakuja ukiwa hujategemea,na bahati haihitaji nguvu lakini si vizuri kuishi kwa kutegemea bahati ,heri kujituma na kutumia nguvu bahati ikitokea inakukuta njiani kuliko kusubiria
 
Neno bahati ni neno la kisingizio, kuamini katika bahati ni kama mcheza kamari tu.

Ukijiaminisha sana katika bahati utaacha hata kuamini Mungu. Utajiingiza kwenye shirki.

Binaadam unatakiwa ujifanyie mambo yako kwa kujipanga na kujitayarisha na si kutegemea bahati au kujiendekeza kwenye bahati.

Kuamini kila kitu kinategemea bahati ni uzembe.
 
Wachaga wamefanikiwa Nini hebu tueleweshe
Huenda tukajifunza kitu
 
Neno bahati ni neno la kisingizio, kuamini katika bahati ni kama mcheza kamari tu.

Ukijiaminisha sana katika bahati utaacha hata kuamini Mungu. Utajiingiza kwenye shirki.

Binaadam unatakiwa ujifanyie mambo yako kwa kujipanga na kujitayarisha na si kutegemea bahati au kujiendekeza kwenye bahati.

Kuamini kila kitu kinategemea bahati ni uzembe.

Umeelewa vizuri alichoandika mleta hoja?
Hakuna mahali amesema mtu asifanye juhudi au bidii kwenye mambo yake, la hasha. Kinachokngelewa hapa pamoja na bidii binafsi, kuna Bahati pia. Haimaanishi usifanye chochote kusubiria bahati.

Hata kwenye mashindano ya michezo mathalani mpira wa miguu, timu zote zitajitahidi, mnaweza washambulia sana wapinzani, mipira ikagonga Mwamba, mkapata penalt mkakosa, hapohapo beki wenu akajifunga wapinzani wakaibuka kidedea.

Mnapokua shule wote mnaweka bidii kwenye kusoma lakini wapo watasoma vitu vingi sana na havitatoka kwenye mtihani. Wako watasoma vichache Kwa Bahati mtihani unakuja mlemle, hiyo ni Bahati.

Kikubwa ni kuwa na utayari. Kuna mahali nilisoma Lucky = preparedness+ Opportunity
 
Bahati = Opportunity + preparations

Unataka kujitengenezea bahati jiandae kwa fursa fulani then tafuta mazingira yake.

Mfano. Diamond platinum alifanya maandalizi ya kuwa msanii atakaeweza kufanya show za kimataifa kwa kutazama hatua za ngazi atakayopitia.

Jambo ambalo kila msanii alipuuza. Ila leo wanaona kama mchawi au MUNGU kampendelea. Ila Kuna watu walikuwa na opportunity nyingi mara 100 ya diamond ila hawakuwa tayari kutengeneza (preparations) ngazi za kupandia.
 
Nyota yenyewe unajua ipoje au ndio bashikolobagendi?! [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna watu hawafanyi preparations zozote za kufanikiwa maishani na wanafanikiwa tu.

Nimeelewa na nnasema kutegemea eti kuna "bahati" ni uzembe.
 
Back
Top Bottom