Kama ukiwa huna Bahati (luck) utatumia nguvu nyingi sana kwenye mambo mengi

Kama ukiwa huna Bahati (luck) utatumia nguvu nyingi sana kwenye mambo mengi

•Hakuna Bahati wala Nyota katika maisha ya Binadamu ndani ya huu ulimwengu wetu

•Ukiamini katika bahati na Nyota,tayari unakuwa umeingia katika ulimwengu Wa shirki(Nguvu za Giza)

•Kuna wakati mambo yako yataenda tofauti na unavyotegemea na utaanza kuhisi huenda kuna watu wanakuzunguka wamechukua Nyota yako ya kupata bahati na tayari utakuwa umeingia kwenye shirki

•Pia katika Imani yangu ya dini,tunaelekezwa kumuomba mwenyezi mungu atukutanishe na watu sahihi katika Cycle ya maisha yetu,kwani kupitia wao ndo tutapata kazi zitakazotuletea riziki ya maisha yetu

•Up to you kuwajua hao watu sahihi wako wapi? Ambao watakuletea neema katika maisha yako
 
Mwenyezi Mungu hutoa Neema,riziki,kipato,mafanikio kupitia watu.........ukielewa hii concept hutaweza kuabudu Miungu Wa Nyota na Bahati ili ufanikiwe katika maisha yako
 
U
Kitu Gani kinakufanya wewe ukutane na watu sahihi na mwingine asikutane nao?
Unaamua mwenyewe kutengeneza mazingira ya kukutana na watu sahihi.

Bahati kila mtu anayo kichwani..Kaa peke yako kila siku Kwa nusu saa ukifikiria ukiwqzua mambo mbalimbali. Usikubali kuongozwa na nafsi iliyonakasoro kwenye fikra usiiruhusu.

Unajua unataka nini elekea huko utakutana na unaowahitaji.

 
Pia ukitaka kujua Bahati hakuna katika maisha,angalia siku hizi Graduates wengi wanatafuta Connection ya watu wenye mamlaka(watu sahihi) ili wapate kazi na sio kukaa na vyeti vyako ili upate Bahati

Kupitia kutafuta Connection ndio utakutanishwa na mtu sahihi atayekupa kazi itakayokuletea riziki katika maisha yako
 
Kutokana na hoja yako binafsi naamini hiyo bahati kila mtu anayo ila iko specific kwenye jambo fulani, labda kuna wengine wana bahati kwenye mambo mengi.

Lakini hakuna mtu asiye na bahati kabisa.
 
Suala la kujiona una bahati au la ni suala la kibinaadamu zaidi.

Cha kujiuliza hapa ni hiyo bahati unaihesabu ukilinganisha na nini?...maana utamkuta Mtu ana afya njema yupo Barabarani anatembea lakini atalalamika hana bahati kwa kuwa tu amepeleka maombi kumi ya kazi na akakosa zote. Sasa je huo uwezo wa kuamka na kutembea huko barabarani kwake sio bahati?. au yeye anasubiri siku akikutana na asiye na uwezo wa kuinuka kutembea akilalamika ndio aone kumbe hana sababu ya kulalamika?.

Ukifuatilia Watu wengi wanaolalamika kuwa hawana bahati ni kwa sababu hawapo tayari kuhesabu yale waliyojaaliwa....wanaona tu vile vichache wanavyokosa kuwa ndio kukosa bahati.
 
Luck is when opportunity meets preparation...

Bahati ni pale fursa inapomkuta mtu aliyekwisha jiandaa kuipokea...
 
Kuna watu Wana ndugu, majirani, marafiki zao wanaela lakin hawawasaidii wanaenda kusaidia watu wengine unaweza ukawa umezungukwa na watu sahii wasiwe na msaada kwako ukaja saidiwa na mtu stranger

Ndio maana nimeuliza huyo mkuu hapo anaposema make sure unazungukwa na watu sahihi, hiyo kuwang'amua hao watu sahihi ni Bahati pia. Kwanini wakusaidie wewe na si wengine?
 
Ndio maana nimeuliza huyo mkuu hapo anaposema make sure unazungukwa na watu sahihi, hiyo kuwang'amua hao watu sahihi ni Bahati pia. Kwanini wakusaidie wewe na si wengine?
Watu sahihi sio kazi yako kuwatambua,kuwajua na kuwafahamu ila hao watu sahihi ndio watatambua potential,skills and talent uliyonayo ww

Cha msingi kutoka kwako ni pure engagement na jamii kwa ujumla na automatically watu sahihi watakuja kwako
 
Watu sahihi sio kazi yako kuwatambua,kuwajua na kuwafahamu ila hao watu sahihi ndio watatambua potential,skills and talent uliyonayo ww

Cha msingi kutoka kwako ni pure engagement na jamii kwa ujumla na automatically watu sahihi watakuja kwako

Kwahiyo wote wenye pure engagement na jamii wanakutana na watu sahihi na kusaidiwa?
 
Back
Top Bottom