Kuna wadada nawafahamu wameolewa wakiwa single moms lkn ndoa zao zinaenda poa tu.
Nadhani inategemea na single mama mwenyewe anajitambuaje, kuna ambao ni wastaarabu ni vile ilitokea tu hao baba watoto wao wakaenda zao, au utoto ile stage ya balehe wakajikuta wanapata ujauzito, so huyu akipata mume atakua serious na mwenye kujiheshimu.
Changamoto inatoka kwa sisi watu wa pembeni kuwanyooshea vidole, like "yule ni firstborn wake si mtoto wa huyo mume wake" nk, inawafanya wajiskie vibaya. Ila ni watu poa na wanajua maisha coz wamepitia mengi. Vijana acheni woga oeni.