kinje ketile
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 5,089
- 9,664
Huu Sasa ndo Ushuhuda Unaotakiwa..!Sista yetu alibeba mimba akiwa mtaani kamaliza form 4, huku na kule baba kaingia mitini(aliko naomba awe kati yawanaotangazwa kuikwaa korona). Matokeo yametoka kachaguliwa kujiunga chuo cha ualimu so alivojifungua akanyonyesha wiki 2 tu akalazimika kumuacha mtoto awahi registration otherwise nafasi anapewa mwingine so mzigo ungekua mkubwa kulea mama na mwanae. Akapaka ndizi mbivu za kutosha kwenye maziwa mzigo ukaanza kunyauka akasepa. Mtoto tukabaki nae akaishi kwa maziwa ya kopo(ni kipindi hiki ndo tulidevelop ile hali ya kupenda mtoto kutoka moyoni.
Akilia au akiugua unahisi uchungu ule wa ndani kabisa kama mzazi). Leo sista ni mwalimu wa shule ya msingi na yuko kwenye ndoa toka 2007 na mambo yanaenda fuleshi kabisa. Binti yake yuko form 3 na anaishi kwa mama yetu kule kwa mama yake anaenda kusalimia mara moja moja kuepuka migongano mingine isiyo ya lazima.. Singo maza wanaoleka so kudum au kutokudum kwenye ndoa ni swala la tabia binafsi za mmoja mmoja..
Jinsi Ya Kuenenda na hali iliyopo.!
Kwanza Kuhakikisha anafuta memory Zote Za Yule 'Mjinga mjinga' Aliyemtelekeza na Kupambana na Maisha.
Kiukweli japo Single Maza Wanashambuliwa Sana Lkn Waowaji Wengi Huwa Wanatamani Saaana Kumpata Mwanamke 'mpambanaji' anayejitambua...!
Na Mwanaume ukifanikiwa Kumpata anayejitambua hlf mpambanaji, Usifanye kosa la Kutomjali Mtoto uliyemkuta.
Mara nyingi Hivyo vitoto Huwa vinarithi roho ngumu Ya Upambanaji na Baadae vinakuwa na nafasi bora.Hapo nawe unakuwa proud kama Sehemu ya Mafanikio.