Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Sipati picha nimefulia eti mke ndo ananilisha 😄😄😄😄
Nahitaji ela la voucher ananitolea kwenye handbag yake aiseeee
Eeh mzee baba usiombe, ukiwaza unatakiwa uanze kuchoma mahindi stand wakati ulikuwa unarudishwa kibosi na Prado lenye namba SU mtaani kwako basi unaona wacha nitulie kwenye kochi nitafakari cha kufanya kwanza😅 huku wife yeye akiwasha IST yake na kwenda zake Access bank kila panapokuchwa!
 
Sometimes ukifukuzwa kazi ujue unaweza kujifunza jambo then ukaja kushukuru kupoteza kazi yenyewe
Kuna kitu hukijui mkuu,
Nitaleta uzi kuelezea,

kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ugumu wa kimaisha ndio unakuwa imara zaidi

just imagine enzi zile form four candidate mwenye division four anahitimu chuo cha ualimu Singida na kupangiwa ajira moja kwa moja bila hata kuaply

Leo hii unaonaje mziki wa ajira
 
Nimeshuhudia mtu akidharauliwa na ki secretary kimoja hivi cha serikalini nkatafakari sana
Kuna mshikaji mmoja alikuwa jeuri sana kwa mabosi zake. Alikuwa ana uwezo wa kujibu nyodo anavyojisikia. Hapo ni kazi anafanya Serikalini. Baadae mambo ya dharau yalivyozidi waliamua kumuhamisha na akawekwa chini ya mtu ambapo pamoja na dharau zake alikuwa hawezi kufurukuta. Na ajabu zaidi hakupewa JD yoyote akabaki anauza sura tu ofisini. Baada ya miezi kadhaa akaamua kuacha kazi na kwenda kwenye kampuni nyingine. Hiyo kampuni akahama tena akapata nyingine. Kabla hajaanza hiyo kampuni ya nyingine ikabidi wafuatilie background ya jamaa kote alipopita. Walimchafua vibaya sana.
Sasa jamaa ana zaidi ya mwaka hana kazi. Nauli tu imekuwa ni shida sana.
 
Hizi ndiyo nyuzi sasa big man ndiyo mara ya kwanza kwa mwaka huu nasoma uzi umejaa points toka mstari wa kwanza mpaka wa mwisho
 
Na akifika ofisini muda wa lunchtime
Stori na marafiki zake ni wewe anaomba ushauri akufanyaje maana huna mbele wala nyuma
 
Sibishani Mpwa wala sikatai ila naamini kwamba kila binadamu ana uwezo wa ku--survive kutokana na mazingira! Kikubwa usikate tamaaa. Mimi ni mfano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…