Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Sipati picha nimefulia eti mke ndo ananilisha 😄😄😄😄
Nahitaji ela la voucher ananitolea kwenye handbag yake aiseeee
Eeh mzee baba usiombe, ukiwaza unatakiwa uanze kuchoma mahindi stand wakati ulikuwa unarudishwa kibosi na Prado lenye namba SU mtaani kwako basi unaona wacha nitulie kwenye kochi nitafakari cha kufanya kwanza😅 huku wife yeye akiwasha IST yake na kwenda zake Access bank kila panapokuchwa!
 
Sometimes ukifukuzwa kazi ujue unaweza kujifunza jambo then ukaja kushukuru kupoteza kazi yenyewe
Kuna kitu hukijui mkuu,
Nitaleta uzi kuelezea,

kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ugumu wa kimaisha ndio unakuwa imara zaidi

just imagine enzi zile form four candidate mwenye division four anahitimu chuo cha ualimu Singida na kupangiwa ajira moja kwa moja bila hata kuaply

Leo hii unaonaje mziki wa ajira
 
Nimeshuhudia mtu akidharauliwa na ki secretary kimoja hivi cha serikalini nkatafakari sana
Kuna mshikaji mmoja alikuwa jeuri sana kwa mabosi zake. Alikuwa ana uwezo wa kujibu nyodo anavyojisikia. Hapo ni kazi anafanya Serikalini. Baadae mambo ya dharau yalivyozidi waliamua kumuhamisha na akawekwa chini ya mtu ambapo pamoja na dharau zake alikuwa hawezi kufurukuta. Na ajabu zaidi hakupewa JD yoyote akabaki anauza sura tu ofisini. Baada ya miezi kadhaa akaamua kuacha kazi na kwenda kwenye kampuni nyingine. Hiyo kampuni akahama tena akapata nyingine. Kabla hajaanza hiyo kampuni ya nyingine ikabidi wafuatilie background ya jamaa kote alipopita. Walimchafua vibaya sana.
Sasa jamaa ana zaidi ya mwaka hana kazi. Nauli tu imekuwa ni shida sana.
 
Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atalayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hskuna atakayehangaika nawewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zalo ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipereka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gali zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

UMASIKINI HAUNA TOFAUTI NA MAKALIO YA MBWA!

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
Hizi ndiyo nyuzi sasa big man ndiyo mara ya kwanza kwa mwaka huu nasoma uzi umejaa points toka mstari wa kwanza mpaka wa mwisho
 
Eeh mzee baba usiombe, ukiwaza unatakiwa uanze kuchoma mahindi stand wakati ulikuwa unarudishwa kibosi na Prado lenye namba SU mtaani kwako basi unaona wacha nitulie kwenye kochi nitafakari cha kufanya kwanza😅 huku wife yeye akiwasha IST yake na kwenda zake Access bank kila panapokuchwa
Na akifika ofisini muda wa lunchtime
Stori na marafiki zake ni wewe anaomba ushauri akufanyaje maana huna mbele wala nyuma
 
Kuna kitu hukijui mkuu,
Nitaleta uzi kuelezea,

kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ugumu wa kimaisha ndio unakuwa imara zaidi

just imagine enzi zile form four candidate mwenye division four anahitimu chuo cha ualimu Singida na kupangiwa ajira moja kwa moja bila hata kuaply

Leo hii unaonaje mziki wa ajira
Sibishani Mpwa wala sikatai ila naamini kwamba kila binadamu ana uwezo wa ku--survive kutokana na mazingira! Kikubwa usikate tamaaa. Mimi ni mfano
 
Back
Top Bottom