Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Kuna mshikaji mmoja alikuwa jeuri sana kwa mabosi zake. Alikuwa ana uwezo wa kujibu nyodo anavyojisikia. Hapo ni kazi anafanya Serikalini. Baadae mambo ya dharau yalivyozidi waliamua kumuhamisha na akawekwa chini ya mtu ambapo pamoja na dharau zake alikuwa hawezi kufurukuta. Na ajabu zaidi hakupewa JD yoyote akabaki anauza sura tu ofisini. Baada ya miezi kadhaa akaamua kuacha kazi na kwenda kwenye kampuni nyingine. Hiyo kampuni akahama tena akapata nyingine. Kabla hajaanza hiyo kampuni ya nyingine ikabidi wafuatilie background ya jamaa kote alipopita. Walimchafua vibaya sana.
Sasa jamaa ana zaidi ya mwaka hana kazi. Nauli tu imekuwa ni shida sana.
Now atakuwa na adabu ya kutosha
 
Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atalayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hskuna atakayehangaika nawewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zalo ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipereka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gali zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

UMASIKINI HAUNA TOFAUTI NA MAKALIO YA MBWA!

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
Umenena msg...
 
Pwagu Aliacha Kazi Ya Kutumwa Akafungua Duka Lake Akajiajiri Akichoka Anafunga Duka Amekwenda Kulala

Sasa Wateja Wakuja Wakikuta Duka Limefungwa
Wanamgongea Basi Akitoka Ndani Mteja Anafokewa
😀😁😂😂😁😀😀🤣🤣🤣😃😂😄😄😅🤣😂
Mteja: Anaulizwa Hujaona Nimefunga Mlango
Nenda Kanunue Sehemu Nyingine



Pwagu: Nimeacha Kazi Ya Kutumwa Na Hii Kazi Ya Duka Sitaki Kero 😑😐😐😶😶
 
Mentality ya Kuajiriwa naona ndio inatuweka kuwa watumwa,....sisemi kuwa kuajiriwa ni kubaya la hasha. Nasema, unaajiriwa na kuanza mchakato wa kuangalia mbele baada ya miaka kadhaa malengo yangu ni yapi? Kwenye kuajiriwa kuna fanya mwaajiriwa kutofikiri nje ya Box, kwa maana kua anaangalia mwisho wa mwezi atapata mshahara, hata kama hautoshi(Na hautatosha maisha yote), yeye atajituma muda woote kufanya kazi ya kuajiriwa!

Sasa basi, suluhisho ni, tumia kazi ya kuajiriwa kama ngazi ya kuanza kujijenga, ukitumia kipato cha kazini, anza kuchukua mkopo wa kuanzisha kijibiashara.....usianze biashara kubwa, anza kitu kidogo kama hata kibanda cha kuuza vocha na soda. baada ya kumaliza mkopo huo, biashara inakua yako na ndio faida......chukua mkopo mwengine, anzisha biashara nyengine, hata kinyozi na kuendelea.

Baada ya miaka michache, utakuta umekua mjasirimali na vibiashara kadhaa. Anza kulea na kuboresha hizo biashara.
Itafika wakati, hizo biashara zako zinakupa zaidi ya mshahara............hapo sasa ndio unaweza kuachia pole pole huo utumwa.

Tatizo wafanyi kazi wengi huanza na kuchukua deni kununua gari...kujenga nyumba, kununua makochi..na kadhalika!

Kuajiriwa ni Slavery ndungu zangu.........mimi ni muajiriwa, lakini, ningepata ushauri mapema, ningekua Muajiri kwa sasa!
Umemaliza kila nilichotaka kuandika. Kiukweli kuongeza chanzo kingine cha mapato ndo jambo litakalomweka mtu huru. Na ili kuongeza kipato inahitaji roho ngumu na mipango thabiti ya muda mfupi na mrefu. Umeongelea hili tatizo la waajiriwa wengi anapata mshahara na kukimbilia kukopa ili ajenge au kununua gari. Sio jambo baya lakini kibiashara haiko sawa sana kwasababu hela iliyowekezwa hairudi na kuishia kuishi maisha magumu sana yenye kitanzi cha mkopo. Nawashauri watu wazingatie hii comment yako
 
Hahahaah niliwahi kuandika Mara nyingi ila kwa kirefu zaidi niliandika I think 2015-2016 hapo sikumbuki! Ila ninachoweza kukushauri ni kwamba, mshukuru Mungu saana sana unapokosa kazi ujue kuna milango mingine mwenyezi Mungu anakupa nafasi kujua mema makubwa
Sisi ma atheist, matumaini yetu tunaweka kwenye logic na science 😃
 
Sisi ma atheist, matumaini yetu tunaweka kwenye logic na science 😃
Whatever, tumia hio hip Logic and science kujua kuwa kuna fursa nyingi nje ya ajira (kuajiriwa)!!

Kumbuka, ajira yako ni nzuri sana ila ujue kuna siku itakoma! Siku ikikoma na ukiwa na umri mdogo utafanyeje? Usitegemee mifuko ya hifadhi ya jamii, I lost a friend of mine kwa kusumbuliwa na mfuko mmoja wapo Lapf to be specific. Alikua just 46yrs imagine.

Mungu atusaidie or whatever unaamini....
 
Back
Top Bottom