Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atakayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hakuna atakayehangaika na wewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zako ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipeleka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo Mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gari zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

UMASIKINI HAUNA TOFAUTI NA MAKALIO YA MBWA!

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
Sawa
 
Umenena vyema mkuu..

Hakuna mtu namheshimu kama anayenijua since nastruggle na sina kitu[emoji848]

Haya mambo ya kukutana kazini kila mmoja ana mchele wake tujenge urafiki huwa siyaentantain kabisa, koz najua ni unafiki tuu..
Urafiki mwingi wa kazini unakuzwa kutokana na starehe mnazozifanya baada ya kazi na siyo shida ulizonazo nje ya kazi na ndo maana siku ukiikosa hiyo kazi na urafiki unaisha kwakua wanajua huna uwezo wa kumudu gharama za starehe Kama awali na sasa utahitaji msaada wao.

Ni vyema ukipata kazi acha kuiga maisha ya ulio wakuta kazini katika kufanya starehe na utengeneze njia yako ya ku save pesa na kuandaa maisha yako kwa nguvu kubwa Kama vile kesho utafukuzwa kazi na hautakua na wakukusaidia.
 
Absolutely correctly [emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]

Kuwa kivyako tu, mtu asijue ishu zako kabisa
 
Huo ni uoga wa maisha huwezi kufanikiwa kwa kutegemea kazi moja lazima uhangaike kila fursa inayojitokeza mbele yako

Inategemea na kazi ya aina gani tunaongelea mkuu, kazi na mishahara inatofautiana.

Kuna watu kazi zao, kuanzia makazi, bima ya afya, usafiri, ada ya shule watoto na mazagazaga kibao anapatiwa, hapo mamilioni ya mshahara wake uko palepale. Achilia mbali fursa za kupata mikopo taasisi za kibenki ili afanye mambo ya maendeleo, mtu kama huyo ukimwambia ajira hailipi anakutizama tu...hakujibu chochote.

Lakini mwisho wa siku, binafsi, namheshimu kupita maelezo mtu mwenye kuweza kutengeneza kiasi chochote cha pesa kwa kujiajiri au kuwa na biashara yake.
 
Acha kuogopesha watu wewe !

Watu tumepiga chini kazi na tukapata na tukapiga Tena chini kazi!

Maisha hayahitaji huo Uoga ,

Elimisha watu wawe na vyanzo mbalimbali vya mapato ili kujinasua na sio kuwa watumwa na kazi !

Mbona hujazungumzia Kama hizo ofisi ambazo zimewaajiri zitafunga shughuli mtu ataenda wapi?
 
Mazingira yanadumaza fikira haswa, watanzania tumedumaa sana, yaani unasema hata kama unapata 3000 kwa siku ambayo haitoshi, inaishia kula tu na wakati mwingne isitoshe, unaishia kukopa mpaka basi lakini bado unashauri mtu asiache aganganie mpaka kufa kwake. Kwani akiamua kupambana na kujiajiri mwenyewe kwa nguvu zote unafikiri hatafanikiwa? uvivu wa kufikiri na woga ndio unapelekea useme yote hayo na kuiona ajira ndoo kila kitu.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
Huyo Jamaa muoga Sana wa maisha.

Unawezaje kuridhika na unyonyaji ?

No human is Limit
 
Ha ha ha unajivuta taratibu mpaka kijiweni ku kill time😅
Amna namna mzee kijua kikizama najirudisha msobe msobe kwa mama watoto.
Hapo unakuta ashatoka kazini na ist kakapark tu anasubiri nije, ndiyo ile ananiona tu no kiss no salamu utasikia anaanza chukua ufunguo kabitini hapo upark gari mi nimechoka eti 😅

Afu kama amna samaki wa kesho emu washa gari kachukue shika pesa hii hapa unapewa liten unatulia kwa password 😂😂😂
Madhara ya mwanaume kukosa pesa mwezi tu.
 
Heheheheh mbona mkeo mzungu huyo, wengine vilanga kichizi 😅😅😅 atakunyali kwanza ndio akutume mkeo sounds kama ana ku please kabisa!
 
Sikubaliani na wewe. Hujawahi kusikia watu wameacha kazi tena ya misharaha mikubwa wakafanya investment zingine na wakatoboa zaidi?
Wapo akina Speshoz hao ila alipopigwa Pini na Ole Sabaya aliangukia ulevi mmbwa almanusura adate akaanza kunywa pombe zake mwenyewe anazozalisha kiwandani kwake 😅😅😅
 
Back
Top Bottom