Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atakayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hakuna atakayehangaika na wewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zako ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipeleka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo Mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

Haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gari zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

Kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
vijana mkajiajiri acheni utumwa
 
Mentality ya Kuajiriwa naona ndio inatuweka kuwa watumwa,....sisemi kuwa kuajiriwa ni kubaya la hasha. Nasema, unaajiriwa na kuanza mchakato wa kuangalia mbele baada ya miaka kadhaa malengo yangu ni yapi? Kwenye kuajiriwa kuna fanya mwaajiriwa kutofikiri nje ya Box, kwa maana kua anaangalia mwisho wa mwezi atapata mshahara, hata kama hautoshi(Na hautatosha maisha yote), yeye atajituma muda woote kufanya kazi ya kuajiriwa!

Sasa basi, suluhisho ni, tumia kazi ya kuajiriwa kama ngazi ya kuanza kujijenga, ukitumia kipato cha kazini, anza kuchukua mkopo wa kuanzisha kijibiashara.....usianze biashara kubwa, anza kitu kidogo kama hata kibanda cha kuuza vocha na soda. baada ya kumaliza mkopo huo, biashara inakua yako na ndio faida......chukua mkopo mwengine, anzisha biashara nyengine, hata kinyozi na kuendelea.

Baada ya miaka michache, utakuta umekua mjasirimali na vibiashara kadhaa. Anza kulea na kuboresha hizo biashara.
Itafika wakati, hizo biashara zako zinakupa zaidi ya mshahara............hapo sasa ndio unaweza kuachia pole pole huo utumwa.

Tatizo wafanyi kazi wengi huanza na kuchukua deni kununua gari...kujenga nyumba, kununua makochi..na kadhalika!

Kuajiriwa ni Slavery ndungu zangu.........mimi ni muajiriwa, lakini, ningepata ushauri mapema, ningekua Muajiri kwa sasa!
Kwahiyo uliyotuambia hapo juu unayafanya (implement)? Kama unafanya na yameenda kama ulivyokusudia tueleze, ili na sisi tufanye (sio tujaribu), maana nijuavyo mikopo ina masharti, ikiwa ni pamoja na dhamana (nyumba, kiwanja, shamba, nk). Tumeona wengi badala ya kupiga hatua, mikopo imewarudisha nyuma!
 
Umenena Vyema sana mkuu.

Back
Top Bottom