Kama umri ungerudi nyuma, kosa gani usingethubutu kulifanya tena kwenye mahusiano?

Kama umri ungerudi nyuma, kosa gani usingethubutu kulifanya tena kwenye mahusiano?

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Jana nikiwa kwenye bajaj niliwasikia Watu wazima wawili wakiongea na aliyekuwa akiendesha bajaj hiyo ambaye bado ni kijana mdogo, maongezi yaliianzia baada ya dereva bajaj kumaliza kumshusha abiria na kuanza kumuomba namba, kisha alipokaa bajaj akasema mtu mwenye mbaya kuliko mwanamke wangu ila unaringa.

Mwanaume wa kwanza akamwambia kijana, najua kwa sasa nikikwambia utasema ni uanaume na kwamba ni tamaa ila kama una mwanamke sahihi acha tulia.

Akaendelea, kama umri wangu ungerudi nyumba nisingetenda kosa la kushindwa kuidhibiti tamaa ambayo ilifanya nikapoteza mwanamke bora sana kwenye maisha yangu kisa wanawake ambao kwa sasa najuta kuwa nao kwani hawajawahi kuwa na mapenzi na mimi ila walikuwa nami sababu niliwapa pesa na baada ya kuisindwa kuwatimizia wamekimbia wote na sasa nipo nipo tu.

Mwingine akasema, Bora wewe Mzee, mimi kama umri ungerudi nyuma kamwe nisingekubali kuwachezea mabinti kwani nilichezea hisia za binti mmoja ambaye alishindwa kuvumilia maumivu akaja kujiua mbele ya nyumba yetu na akaacha ujumbe kuwa mimi ndio chanzo, tukio lile liliniweka mahabusu muda mrefu sana hali ambayo ilizima ndoto zangu nyingi mno mpaka sasa bado sijakaa sawa.

Stori zao ziliendelea nikashuka, nikawa natafakari kumbe kuna vitu mtu anaweza akafanya ambavyo akatamani visijirudie au kama kuna uwezekano wa kufuta kurasa basi angefuta kabisa.
 
Jana nikiwa kwenye bajaj niliwasikia Watu wazima wawili wakiongea na aliyekuwa akiendesha bajaj hiyo ambaye bado ni kijanaafakari kumbe kuna vitu mtu anaweza akafanya ambavyo akatamani visijirudie au kama kuna uwezekano wa kufuta kurasa basi angefuta kabisa.
Mapenzi yanaongoza dunia, kila mahali watu wanalalamika Wanaume kwa wanawake😅😅😅
 
Sina kosa lolote nilifanya kwenye mahusiano hata muda ukirudi nyuma nitafanya yale yale na haya haya nayofanya sasa

Ukianzisha uzi wa majuto ya kimaisha nje ya mahusiano nitag nije kutiririka

Haya maisha bana.

Usipoteseka kwenye mapenz . Utateseka kwenye mambo mengne.
Ili mradi tu uteseke.

Anyway, Tushukuru Mungu kwa kila kitu. Hasa tushukuru zaid kama kwa kipindi hiki ww hauteseki kwa Lolote.
 
kuna bwege nisinge zaa nae kabisa, ila kuna bwege zaidi nisinge mkula matakor yake alinipa gono super el-nino ya mwaka huu inasubiri

kubwa zaidi nisinge fuata makundi na kuacha kusoma hesabu leo inanigharimu pakubwa sana maana uwezo nilikuwa nao.
 
Shida ni kwamba hatuwezi kujua tusivyo vijua na ili la binadamu tujue na tujifunze, lazima tutende, tukosee. Then ndio tujifunze kutokana na makosa.

Na hii sio kwenye mapenzi ni kwenye kila kitu.

Athari zinapo tokea ndio mafunzo hupatikana.

Bila Athari hakuna mafunzo.
 
Back
Top Bottom