Jana nikiwa kwenye bajaj niliwasikia Watu wazima wawili wakiongea na aliyekuwa akiendesha bajaj hiyo ambaye bado ni kijana mdogo, maongezi yaliianzia baada ya dereva bajaj kumaliza kumshusha abiria na kuanza kumuomba namba, kisha alipokaa bajaj akasema mtu mwenye mbaya kuliko mwanamke wangu ila unaringa.
Mwanaume wa kwanza akamwambia kijana, najua kwa sasa nikikwambia utasema ni uanaume na kwamba ni tamaa ila kama una mwanamke sahihi acha tulia.
Akaendelea, kama umri wangu ungerudi nyumba nisingetenda kosa la kushindwa kuidhibiti tamaa ambayo ilifanya nikapoteza mwanamke bora sana kwenye maisha yangu kisa wanawake ambao kwa sasa najuta kuwa nao kwani hawajawahi kuwa na mapenzi na mimi ila walikuwa nami sababu niliwapa pesa na baada ya kuisindwa kuwatimizia wamekimbia wote na sasa nipo nipo tu.
Mwingine akasema, Bora wewe Mzee, mimi kama umri ungerudi nyuma kamwe nisingekubali kuwachezea mabinti kwani nilichezea hisia za binti mmoja ambaye alishindwa kuvumilia maumivu akaja kujiua mbele ya nyumba yetu na akaacha ujumbe kuwa mimi ndio chanzo, tukio lile liliniweka mahabusu muda mrefu sana hali ambayo ilizima ndoto zangu nyingi mno mpaka sasa bado sijakaa sawa.
Stori zao ziliendelea nikashuka, nikawa natafakari kumbe kuna vitu mtu anaweza akafanya ambavyo akatamani visijirudie au kama kuna uwezekano wa kufuta kurasa basi angefuta kabisa.