Tayari ashazidiwa kete kudadeki. Ujue mimi nilikuwa kwenye Mahusiano na huyu dada, mahusiano yalikaa muda mrefu nikaanza shughuli za ujenzi nikawa namshirikisha. Sasa akawa ananiambia eti nisiwaambie Nyumbani hata mzee wangu kuwa ninajenga. Nikamuuliza kwanini akasema eti wataroga nisifanikiwe na aliyekua anajua ninajenga ni yeye tu na hapo nilikuwa nimeanza taratibu za kwenda kujitambulisha kwao. Kimsingi niliwaza sana, huyu mwanamama hataki ndugu wajue ninachofanya ili siku nikifa aje kubeba tu maana kama ningemuoa alikuwa mrithi pamoja na kwamba mali kazikuta tayari nimeshachuma. Nilimshirikisha mzee mmoja ambaye tunaheshimiana kama ambavyo ilivyo Baba na kijana wake akaniambia huyo sio wa kuoa na ukijumlisha na kabila lake Atakutanguliza