Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Namba 5.

Mkuu maboneng na Underson street and Harrison unaicha vipi Reef Hotel pale club moja matata ipo juu ya ghorofa?

JoJo
Cosmopolitan
HQ
Bila kusahau Royal park Hotel.
unainaje pale alafu siku moja moja usiende kuenjoy haiwezekani.

Konka unapaonaje mkuu balaa kabisa.

Ukitafuta pesa usisahau na kuishi pia siku moja moja.
Nimekuelewa mkuu, lakini nilishauri mtu afanye starehe zake kimagutu. Yani mguu mmoja ndani mungine nje, sababu akijisahau na kuingiza miguu yote basi atasombwa tu na maji na nyumbani kwao watamsahau.

Itabaki story tu kwamba tuna brother wetu au ndugu yetu yupo South. Wakati huku wewe mwenyewe ushapoteza channel zote huujui mchana wala usiku, upo upo tu 🤣🤣🤣
 
Ninachofahamu mimi viza ya work permit unaipata ubalozini. Hapa ni zile viza za kuingia na kutoka (visitor).
Work permit viza ni za white color job kama kina Mwamvita Makamba unatoka na ajira yako Bongo.

Vijana wanaojitambuwa waombe vyuo kozi ndefu tu, maana ukiomba short course no need of student visa.
 
Work permit viza ni za white color job kama kina Mwamvita Makamba unatoka na ajira yako Bongo.

Vijana wanaojitambuwa waombe vyuo kozi ndefu tu, maana ukiomba short course no need of student visa.
Ya shukran mkuu kwa ufafanuzi wako. Na mimi nilikuwa namjibu jamaa alietaka kuja kutafuta work permit huku, ili afanye kazi hapa.
 
Na yalitimia kwa kweli
Kuna wakati alieenda kwao likizo alivyorudi anipigia stori za huyo boyfriend yake kuwa alisema kama ningeenda nae angeenda kutafuta Desert Eagle
Kuja kugugo desert eagle ni nini nakutana hii kitu, roho ilipiga paa

View attachment 3082410
Desert eagle ni bastola ya mkononi lakini ina nguvu mno.
Mtu akipigwa kichwani na risasi ya desert eagle ni kichwa kitasambaa inawezekana usijulikane sura.

Mlio wake ikipigwa mtaani watu wanalala hata kama ni saa 12 jioni.

Bastola moja hatari sana.
 
Watu wengi huuwawa kwa sababu ya kugoma kutoa ushirikiano. Juzikati kuna mpopo fulani alikuwa anatoka kwake nafikiri kuelekea katika mizunguko yake.

Sasa ile anafungua gate atoke jamaa watatu wakamsogelea vizuri tu na kumuomba sim ili waondoke. Mpopo alipoona anaombwa sim akaleta mgomo. Jamaa wakataka watumie nguvu kuichukua. Yule mpopo kwa vile tayari alikuwa ashafunga gate, basi akairusha ile sim kwa ndani ili jamaa wasipate kitu.

Aisee kitendo kile walikichukulia kama dharau, wawili kati yao wakatoa bastola kila mmoja ya kwake. Basi wakawa wanapokezana. Mmoja kapiga ya paja, mungine akapiga kichwani, mungine tena kifuani, mungine akamalizia tumboni na kusepa zao kusikojulikana.
Kuuana kisa simu.
Hivi serikali ya SA imejipanga vipi kupambana na huo uhalifu?
 
Please share your experience if it is okay with you; some future travellers are here, silently reading this thread.
Naona umeamua kupiga ngeli kabisa upo kwenye maandalizi. Haya kazamie tu😂😂
 

Attachments

  • 20240819_162432.jpg
    20240819_162432.jpg
    29.8 KB · Views: 6
Kweli mkuu, hali imekuwa ngumu kila sehemu. Wewe ukitoka South na kukimbilia Botswana, wenzako wanatoka Botswana na kukimbilia South.
Gaborone utafanya nini pale kwa watu wanaoanza life wenyeji wenyewe nipo nao huku Centurion wamekimbia pale sasa hivi Gabs ni kwa Ma Legends uchukue gari za Kijapani ukimbize Tanzania maana zimejaa pale wakipewa mshahara wanauza gari ya zamani wao wanataka ku drive gari mpya kila siku na Wapakistani wa magari ya Japan/Durban wamejaa pale.
 
Gaborone utafanya nini pale kwa watu wanaoanza life wenyeji wenyewe nipo nao huku Centurion wamekimbia pale sasa hivi Gabs ni kwa Ma Legends uchukue gari za Kijapani ukimbize Tanzania maana zimejaa pale wakipewa mshahara wanauza gari ya zamani wao wanataka ku drive gari mpya kila siku na Wapakistani wa magari ya Japan/Durban wamejaa pale.
Noma sana mkuu.
 
Kila mtu anakusanya pesa mnampatia dreva? Sijaelewa mkuu
Maana yake nauli mnachangishana wenyewe kuanzia waliokaa siti za nya then mwisho anapewa aliyekaa siti ya mbele ambaye uweka nauli yake na kumkabidhi dereva!! Dereva yeye anahesabu kuwa mf kama Ali kuwa na abilia 20 na nauli ni 500 maana yake anatakiwa apokee elf 10 kutoka kwako uliyekaa siti ya mbele sasa wewe kama ulipewa pesa pungufu au kuna wanaoitaj change ni jukumu lako Kurdish hyo chenji ukizingua dereva anaanza na wewe!! Kwa nilivyomuelewa mleta Mada
 
Na dunia iliyoendelea Ulaya na marekani hakuna conductor mkusanya hela ni unalipia kwenye mlango kwa driver kwa kadi au cash japo wengi ni kwa card tena unakuta ni ya mwezi mzima (kama kwenye train au hizo bus za town ) hii ya konda na abiria ni huku kwetu
Tukiamua tunaweza ila kuamua kila mtu kua na basi ndo mana iyo systen haiwezekani
 
Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.

Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.

Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.

Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.

Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.

1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.

2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.

Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.

3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.

4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.

5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.

6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Mitaa ya Hilbrow jijini Johannesburg. Unakabwa kweupeee na hakuna anae kusaidia. 👇

 
Video ikiwaonesha wachimbaji madini haramu wanaojulikana kama Zama Zama wakifurahia jambo huku wakiwa na silaha nzito za moto. Kundi hili limelaumiwa kwa kusababisha vurugu na mauaji huko Roodepoort mashariki mwa Jiji la Johannesburg.
 
Back
Top Bottom