Kwenye hospitali ya vichaa,
mwandishi wa habari akamwuliza daktari:
"Wewe huwa unatambuaje mgonjwa huyu ni wa kulazwa, na huyu si wa kulazwa "?
Daktari akajibu:
"Kuna njia nyingi ... kwa mfano naweza kujaza maji kwenye sinki la bafuni, nikamwekea hapo kijiko cha mezani,
kikombe na ndoo;
Kisha nikamwagiza amwage maji yote
yaliyo kwenye sinki.
Mwandishi: "Bila shaka aliye timamu
atatumia ndoo .. . Maana ndoo ndiyo
kubwa! Si ndivyo? "
Daktari: "Hapana! Mtu mwenye akili timamu atafungulia koki ya chini ya sinki!
Tafadhali na wewe nenda kalale kitanda Namba-39 .. . Nitakuja kuendelea
kukuchunguza zaidi! "
.
Hahhahaaa! Hivi kweli na wewe pia uliwaza ndoo?
Basi, kitanda chako ni Namba-40 !!
#Natania_tu
#Kwanza_me_naongea_na_simu