Jana nilikula bakuli 4 za maharage.Demu wng akanipgia cm kunialika dinner home kwao,nikaenda.Nlipofika akanikumbatia kwa bashasha vile hakuamini km ningeenda,akaniambia "fumba macho,nna suprise kwako!".Nikafumba,akanifunga kitambaa cheusi usoni halaf akaniongoza had sebulen kwenye kiti.Mara cm yake ikaita chumban,akaniomba aende kuipokea ila akanisisitiza nisifungue kitambaa.Akaenda kupokea cm.Yale maharage nilokula yakanikoroga tumbo,likajaa gesi.Nikajibinua kwa kushoto nikapunguza gesi kidogo.Harufu ilikuwa kali,nikachukua leso mfukon nikapungapunga hewa kupunguza harufu huku nikiwa makini kusikiliza mazungumzo ya cm chumban.Nikajibinua kwa kulia nikaachia makombora matatu ya kimya kimya.Harufu ilikuwa mbaya zaid ya kabeji na maharage yalochacha.Nikachukua leso nikapukuta pukuta hewa.Mara simu ikakata huko chumbani,dem akaja,akaniuliza "hujafungua kitambaa kweli?",kwa sura isiyo na hatia nikamjibu,"hakyamungu sijafungua".Akanifungua.Ghafla wageni 12 akiwemo baba na mama yake wameketi huku wameziba pua!!