Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 301,221
- 1,172,274
Siku fulani hivi, Mwanandoa mmoja mpya aitwaye Paulo (sio jina lake halisi), alikuwa akirudi nyumbani toka kazini mida kama ya saa mbili usiku huku mkewe akimsubiri. . Wakati akiwa njiani, Paulo alimuona msichana mmoja mrembo akiwa amesimama peke yake barabarani akisubiri daladala. . Mr. Paulo, licha ya kuvutiwa na urembo wa yule msichana, pia, huruma ilimwingia na kuamua kusimamisha gari ili amsalimie na ampe hisani ya lift. . Lakini yule msichana hakuonesha ushirikiano wowote, Paulo aliendelea kumbembeleza japo kupokea salamu tu lakini dada aliweka ngumu na kuanza kuondoka eneo lile. Paulo akaanza kumfuata kwa nyuma. Hii ni kwa kuwa alikuwa akimuonea huruma asije shambuliwa na wahuni na pia, kwa ajili ya kutuliza tamaa yake ambayo ilishamwingia. Ghafla yule binti akasimama na kumgeukia Paulo. Kisha akamwambia. "Boss najua unanifuatilia na najua ni nini unachotaka kutoka kwangu." . Paulo akatabasamu na kisha akachukua simu yake na kuizima, maana, mkewe alikuwa akimpigia mara kwa mara kiasi cha kumsumbua. . Yule msichana akamwambia, najua unanitaka kimapenzi. Basi, nitakubali nikalale na wewe endapo utakuwa mwema kwangu pamoja na kunijali. Paulo akamuahidi kuwa, kwa hilo tu wala asijali maana yeye ndiye Sultan Suleman Khan wa himaya ya Ottoman! Akajitapa kuwa anajua kupenda na atamthibitishia hilo. . Akamchukua, wakapanda kwenye gari na kumpeleka kwenye hoteli nzuri iliyokuwa karibu na eneo lile. . Wakiwa ndani ya chumba cha hotel, Paulo akavua nguo zake zote. Kisha, akaanza kumvua na yule binti. . Wakati akiendelea kumvua, mara akaona kitu cha ajabu kwa yule dada. Ambapo, hakukitegemea kabisa kukiona maishani mwake. Kitu ambacho kilimfanya ajutie tabia yake ya uzinzi..... . Bado unasoma stori hii? . Lengo langu ni wale wasiopenda kusoma post ndefu wapate tabu, sasa sijui namna gani niimalize hii stori yangu ya uongo...😂😂 . Hata hivyo, unaweza kunisaidia kuumalizia uongo huu....... 🏃 🏃 .