Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Leo Kwenye Basi Kuna Wadada Wawili Walikua Wanagombaniana Seat Moja, Dereva Kwa Hasira akasema "Mwenye sura mbaya ndo akalie hiyo Seat" Yani mpaka tunafika Wote Wawili Walikua Wamesimama. Kuna Madereva Wana Hekima Kama Mfalme Solomon [emoji3][emoji23][emoji23]```
Hahaha [emoji23][emoji23]
 
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu

JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu

RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana

JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.

RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia

RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?

JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’
[emoji3][emoji3][emoji4] angejua huyo nguruwe ni nan....
 
Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini...
Ahhh!!!! [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station "naitwa Juma nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki7, ATM card na karatasi yenye PIN ya ATM card na kijimfuko cha dhahabu" Mtangazaji akasema, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama anakusikiliza? Jamaa akajibu; hapana, ninaomba kumuombea dedication wimbo wa R.Kelly usemao "U SAVED ME" umfikie popote alipo!!
 
Jana nilipanda daladala nikapata seat nikaketi, nikawa nimejiachia ninachati kwenye simu yangu(Smart phone), kukawa na jamaa kasimama pembeni yangu, ye hakupata seat. Sasa akawa anasoma message zangu bila aibu yani anafutilia ninavyochati… Basi nikasema ngoja nimtie Adabu mshenzi huyu…. Nikacheck saa yangu yamkononi kisha nikatext: "Oya Ben Kwaheri bwana, zimebaki sekunde 30 tu hili bomu💣 lilipuke… najua hatutaonana tena, nitunzie Familia yangu, wambie nawapenda sana…" Yule jamaa akajirusha dirishani……😂😅
 
Haya mabango ya barabarani yataniua Jamani naombeni mnisaidie nipo natembea kwa mguu katika kutembea kwangu nimekuta kibao kimeandikwa punguza mwendo mimi mwendo nimepunguza ila kwa mbele tena nikakuta kibao kimeandikwa taratibu mbele kuna kona kali nikatembea mwendo wa kinyonga cha ajabu zaidi nimekuta tena kibao kimeandikwa tembea spid 30 apo ndio sijaweza kujua mwendo ninio tembea ni spidi ngapi 😱😱😱
 
Katika kikao cha familia, kichaa wa hiyo familia alisimama kabla wengine hawajaongea nakusema: nashangaa kuona hali ya familia yetu,naona kama inalaaniwa mana katika familia hakuna hata mbunge,askari, mwanamuziki; yaani mimi mwenyewe nisingekazana hata kichaa asingekuepo🤣🤣🤣🤣🤣 kikao kiliishia hapo mana kila mtu aliondoka
 
Swali: KULOGWA NI NINI? Jibu: Kurogwa ni Pale unapotembea Kilometa 10 Kwenda kazini.. Unafika kazini kwako unagundua kuwa funguo za ofisi umeziacha home.. Unarudi home ukiwa na hasira na unaamua kuliacha begi Mlangoni pa ofisi.. Unafika home na unakumbuka funguo za nyumbani umeziacha kwenye begi Mlangoni pa ofisi.. Unarudi ofisini kuchukua funguo za mlangoni.. unaamua kuchukua begi lenye funguo na kurudi nalo home. Unafka home na unatoa funguo za mlangoni ktk begi. Ndipo unagundua kuwa funguo za ofisi pia zipo katika begi!!
 
wewe ni kijana umeoa unaish na mkeo kwa aman na furaha jion moja anakweleza kuwa kuna marafiki zake watakuja kesho yake kumsalimia🤝🤝unakubaliana nae kuwa ni vyema tu asbh na mapema unatoka unaenda kazin mchana ukiwa mizunguko unakutana na wadada wawili wakiwa ktk maongezi yao ukayaskia bila kukusudia kwa uchache* dada 1; _hv ulisema shost nae alikuganda umfanyie mipango ya zile dawa?_ dada 2: _aliniganda kama nn👌👌nkaona nimsaidie tu na ndo hvy nampelekea_ *ukaendelea na mizunguko yako mpk mda ukarudi nyumbn ile kuingia 😳😳😳😳unakutana na wale wadada wakicheka na kugonga na mkeo ukaanza jiuliza maswali????? ghafla mkeo akakutambulisha kuwa ndo wagen aliokua akiwasubiria na anashukuru kutwa nzima wamempa kampan ukiwa bado unajiuliza na kushangaa mkeo anakukaribisha chakula akidai wao walishakula umebakia wewe tu utachukua hatua gan?
 
Msanii mmoja anaitwa ''KINYA'' alikuwa ana perfom jukwaan..!!! Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:- ''YEAH NI TEMBA hapa au YEAH NI CHEGE hapa…!!! Yeye akasema: "YEAH NIKINYA HAPA…!!!" Watu wakapiga kelele ''UTAZOAAA'' mwenyewe bwenge wee
 
Mfugaji mmoja alikwenda kwa mfugaji mwenzake (ambae pia ni bwana mifugo wa eneo lao) asubuhi moja. Alipobisha hodi mtoto wa kiume wa umri upatao miaka 12 akamfungulia mlango. Mazungumzo yafuatayo yakafuatia: Mkulima: Baba yako yupo? Mtoto: Hapana Mzee, amekwenda mjini. Mkulima: Mama yako? Mtoto: Nae kaenda mjini na baba. Mkulima: Kaka yako Howard yupo? Mtoto: Nae hayupo, wote yeye, baba na mama wamekwenda mjini. Kwani una shida gani? Kama kuna kitu unahitaji niambie maana nimeachiwa funguo na najua vifaa vinapowekwa. Mzee akawaza kidogo halafu akasema: Kwa kweli nilitaka kuongea na baba, mama au kaka yako kwa kuwa kaka yako amempa mimba binti yangu. Mtoto akafikiria kidogo halafu akasema: Kusema ukweli itabidi umsubirie baba, ila kwa kukusaidia ni kuwa baba hulipisha shilingi laki moja kwa kupandisha dume la ng'ombe na elfu hamsini kwa beberu. Ila sijui baba hutoza shilingi ngapi kwa Howard akifanikiwa kutia mimba. 😁😁😁😂
 
Back
Top Bottom