Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Umeenda kutembea ukweni kwako baada ya chakula chausiku unapewa chumba chakulala inapofika usiku unatakakutoka kwenda kujisaidi kwasababu taa zimezimwa unapamia vyombo vya chakula sebleni kipindi unajalibu kupapasa uviweke sawa mala taa inawashwa na mama mkwe anaona umeshika vyombo anakwambia, baba kama hukushiba ungesema [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Unaamua kwenda ukweni kuwasalimia inafika usiku wanakupa chumba cha kulala unabanwa haja ndogo usiku unaamua kuamka kwenda chooni bahati mbaya unaingia jikoni kwa kuwa taa imezimwa unaparamia viombo vinaanguka ile hujui nini cha kufanya mara taa inawashwa kungalia mi mama mkwe anakwambia kama hukushiba siungesema tu baba......!
Hapo ndio utajua ukweni si kwenu
 
Leo nimepita sehemu moja hivi mara nikaona mtoto mmoja mkali sana huku akimbembeza jamaa mmoja wa hali ya chini amkubalie wawe wapenzi yani yule demu kambembeleza jamaa lakini jamaa kakataa nikaamua nijaribu bahati yangu nikaenda pale alipo yule demu na huyo jamaa nikafika nikampigia magoti yule demu nimbembeleze awe wangu........kabla hata sijaanza nikasikia sauti kali ikasema kutoka upande mwingine cut.... Cut... Kugeuka nikakuta kundi la watu limenikodolea nakwambia nimeondoka hapo mikono nyuma aibu niliyonayo naijua mwenyewe...!!
 
Mwalimu kaniulizaa kama mtoto mdogo anaitwa mchanga... Je mtu mkubwa anaitwaje? ... Nikamjibu anaitwa kokoto..... Ameniitaa staff room labda atakuwa ameniitia chai

Huyu mwalimu ana roho nzuri sio kama mwl Msigwa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119] [emoji119] [emoji119]
 
Kama utakipenda kimoja njoo PM tuzungumze biashara
1. Freezer aina ya Boss Tsh250000. Haina mlango wa mtungi wa gesi
.
2. Feni ya chini Tsh 15000/=. Inawaka kwa machale.. yaeza kukaa hadi masaa 2 haijaanza kuzunguka
,
3. Pasi ya umeme aina ya Phillips. Tsh 12000/=, haishiki moto kabisa hata ikae nusu saa kwny umeme na kidude cha kuregulate moto kimeharbika..

4. Meza ya plastic Tsh 75000/= ina miguu 3 na mmoja mfupi kidg.

5. Vikombe vya udongo Dozen 1 Tsh 25000/= ila vilipata ajali kidg.. vimekatika mikono na vingne vimetoboka chini
6.Redio ya caset lkini haina transiforma bei 34000
7.Flat scren bei 50000 kioo kimepasuka na haina rimot control na batan zime haribika fasta nichek [emoji41]
8.Simu aina ya Sumsung s7 edge 470000/= ilidondokea kwenye maji ikapiga shot, kitufe cha kuwashia hakipo na hata ukiweka kingine haiwaki, ni simu nzuri bora na ya kisasa!
9.Kamera aina ya sony mp 16 bei 62500/= haina lens, ni mbovu hata mafundi hawaitaki kama spea.
10.Bajaji aina ya tvs, bei 1400000/= haina matairi, viti wala usukani! Imetumika miaka 8 na inadaiwa kodi ya miaka 2!

Karibuni, bidhaa ni nyingi sana, zipo za aina tofauti tofauti kama magari, ndege, treni, meli, maparashuti, vifaru, n.k vyote hivyo vikiwa katika hali mbaya sana, (ikumbukwe hizi ni toys za watoto zilizotumika huko uswahilini na kutupwa kwenye majalala)
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji119]
 
Basi utaondoka na stress..!

Stress ni nini??
Stress ni pale umeenda kijijini kwa bibi ako huku umebeba jeans zako tano zile ja mtindo wa kuchanika (chanika jeans) sasa siku ukazifua ukazianika ukaenda zako kutembea ile unarudi jioni unakuta bibi yako kazianua afu kazishona zote!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Future [emoji289]
We ni nomaaa
 
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] pombe siyo chai!!
 
Kama utakipenda kimoja njoo PM tuzungumze biashara
1. Freezer aina ya Boss Tsh250000. Haina mlango wa mtungi wa gesi
.
2. Feni ya chini Tsh 15000/=. Inawaka kwa machale.. yaeza kukaa hadi masaa 2 haijaanza kuzunguka
,
3. Pasi ya umeme aina ya Phillips. Tsh 12000/=, haishiki moto kabisa hata ikae nusu saa kwny umeme na kidude cha kuregulate moto kimeharbika..

4. Meza ya plastic Tsh 75000/= ina miguu 3 na mmoja mfupi kidg.

5. Vikombe vya udongo Dozen 1 Tsh 25000/= ila vilipata ajali kidg.. vimekatika mikono na vingne vimetoboka chini
6.Redio ya caset lkini haina transiforma bei 34000
7.Flat scren bei 50000 kioo kimepasuka na haina rimot control na batan zime haribika fasta nichek [emoji41]
8.Simu aina ya Sumsung s7 edge 470000/= ilidondokea kwenye maji ikapiga shot, kitufe cha kuwashia hakipo na hata ukiweka kingine haiwaki, ni simu nzuri bora na ya kisasa!
9.Kamera aina ya sony mp 16 bei 62500/= haina lens, ni mbovu hata mafundi hawaitaki kama spea.
10.Bajaji aina ya tvs, bei 1400000/= haina matairi, viti wala usukani! Imetumika miaka 8 na inadaiwa kodi ya miaka 2!

Karibuni, bidhaa ni nyingi sana, zipo za aina tofauti tofauti kama magari, ndege, treni, meli, maparashuti, vifaru, n.k vyote hivyo vikiwa katika hali mbaya sana, (ikumbukwe hizi ni toys za watoto zilizotumika huko uswahilini na kutupwa kwenye majalala)
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka sanaaaa..

Asante stress zimepungua 20%
 
Jana nimepewa kazi ya kuandika DUKA LA DAWA MUHIMU sasa boos kaja kasema hanilipi nimeandika vibaya akaondoka sasa nimeamua kufuta MUHIMU nimeweka KULEVYA Niko home nasikia vin'gora bilashaka kuna mgonjwa ameletwa

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom