Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Wanasayansi waliwahi kufanya utafiti ili kupima nguvu ya “self-belief”(Hali ya kujiamini katika kufanya mambo).Waliamua kumchukua tembo aliyezaliwa na kumfunga kwa kamba kwenye mti tangu siku ya kwanza alipozaliwa.Tembo yule kila alipojaribu kutoka,kamba ilimzuia na kumuwekea mipaka ya umbali ambao anaweza kwenda.Baada ya Muda alijikuta anazunguka kwenye umbali unaoendana na urefu wa Kamba yake tu. . Tembo yule alikua mkubwa na kutokana na UZITO na UKUBWA wake angeweza KUKATA ile Kamba kwa kujivuta na kuwa HURU lakini cha kushangaza HAKUJARIBU KABISA kufanya hivyo.Hata pale alipowaona wenzake wakubwa kama yeye wakiwa HURU yeye aliamini hawezi kufanya lolote lile zaidi ya kubakia kwenye urefu wa ile kamba nyembamba. . Watu wengi wana UWEZO mkubwa sana ila WAMESHIKILIWA na KAMBA NYEMBAMBA ambazo haziwaruhusu kufanya mambo MAKUBWA. . Kwenye kila OFISI kuna watu wameshajiwekea MIPAKA ya UWEZO wao kutokana na UZOEFU,ELIMU ama mambo yaliyowahi kuwatokea huko nyuma.Kuna watu hawapigi hatua kwenye BIASHARA kwa sababu kuna Kitu wanaamini KINAWAZUIA hata kama hakina UWEZO wa kuwazuia.Kuna watu wana KAMBA kuhusiana na MAFANIKIO YAO YA KIFEDHA,wengine hawaamini kama wanaweza kuwa na MAHUSIANO MAZURI yenye FURAHA TENA n.k . Watu wenye Kamba utafanya tu,kila siku utawasikia “Hiki Hakiwezekani”,”Hii nilijaribu nikafeli”,”Fulani alifanya hakufanikiwa” n.k Wengi wenye kamba huwa wanataka wakufunge na wewe kwenye kamba zao.Uwe makini! . Wengi wana UWEZO ila wameruhusu KAMBA ziwafelishe
 
Hio feni
Kama utakipenda kimoja njoo PM tuzungumze biashara
1. Freezer aina ya Boss Tsh250000. Haina mlango wa mtungi wa gesi
.
2. Feni ya chini Tsh 15000/=. Inawaka kwa machale.. yaeza kukaa hadi masaa 2 haijaanza kuzunguka
,
3. Pasi ya umeme aina ya Phillips. Tsh 12000/=, haishiki moto kabisa hata ikae nusu saa kwny umeme na kidude cha kuregulate moto kimeharbika..

4. Meza ya plastic Tsh 75000/= ina miguu 3 na mmoja mfupi kidg.

5. Vikombe vya udongo Dozen 1 Tsh 25000/= ila vilipata ajali kidg.. vimekatika mikono na vingne vimetoboka chini
6.Redio ya caset lkini haina transiforma bei 34000
7.Flat scren bei 50000 kioo kimepasuka na haina rimot control na batan zime haribika fasta nichek [emoji41]
8.Simu aina ya Sumsung s7 edge 470000/= ilidondokea kwenye maji ikapiga shot, kitufe cha kuwashia hakipo na hata ukiweka kingine haiwaki, ni simu nzuri bora na ya kisasa!
9.Kamera aina ya sony mp 16 bei 62500/= haina lens, ni mbovu hata mafundi hawaitaki kama spea.
10.Bajaji aina ya tvs, bei 1400000/= haina matairi, viti wala usukani! Imetumika miaka 8 na inadaiwa kodi ya miaka 2!

Karibuni, bidhaa ni nyingi sana, zipo za aina tofauti tofauti kama magari, ndege, treni, meli, maparashuti, vifaru, n.k vyote hivyo vikiwa katika hali mbaya sana, (ikumbukwe hizi ni toys za watoto zilizotumika huko uswahilini na kutupwa kwenye majalala)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasayansi waliwahi kufanya utafiti ili kupima nguvu ya “self-belief”(Hali ya kujiamini katika kufanya mambo).Waliamua kumchukua tembo aliyezaliwa na kumfunga kwa kamba kwenye mti tangu siku ya kwanza alipozaliwa.Tembo yule kila alipojaribu kutoka,kamba ilimzuia na kumuwekea mipaka ya umbali ambao anaweza kwenda.Baada ya Muda alijikuta anazunguka kwenye umbali unaoendana na urefu wa Kamba yake tu. . Tembo yule alikua mkubwa na kutokana na UZITO na UKUBWA wake angeweza KUKATA ile Kamba kwa kujivuta na kuwa HURU lakini cha kushangaza HAKUJARIBU KABISA kufanya hivyo.Hata pale alipowaona wenzake wakubwa kama yeye wakiwa HURU yeye aliamini hawezi kufanya lolote lile zaidi ya kubakia kwenye urefu wa ile kamba nyembamba. . Watu wengi wana UWEZO mkubwa sana ila WAMESHIKILIWA na KAMBA NYEMBAMBA ambazo haziwaruhusu kufanya mambo MAKUBWA. . Kwenye kila OFISI kuna watu wameshajiwekea MIPAKA ya UWEZO wao kutokana na UZOEFU,ELIMU ama mambo yaliyowahi kuwatokea huko nyuma.Kuna watu hawapigi hatua kwenye BIASHARA kwa sababu kuna Kitu wanaamini KINAWAZUIA hata kama hakina UWEZO wa kuwazuia.Kuna watu wana KAMBA kuhusiana na MAFANIKIO YAO YA KIFEDHA,wengine hawaamini kama wanaweza kuwa na MAHUSIANO MAZURI yenye FURAHA TENA n.k . Watu wenye Kamba utafanya tu,kila siku utawasikia “Hiki Hakiwezekani”,”Hii nilijaribu nikafeli”,”Fulani alifanya hakufanikiwa” n.k Wengi wenye kamba huwa wanataka wakufunge na wewe kwenye kamba zao.Uwe makini! . Wengi wana UWEZO ila wameruhusu KAMBA ziwafelishe
Good advice. Thanks

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... the reality ...
20190320_164313.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DALILI ZA KUJUA KUWA UNADATE NA BINTI WA KITANZANIA
- Anasikia Njaa Hapo Hapo Baada ya kutongozwa
- Nywele Zake Zinafumuka muda huo huo
- Siku Yake Ya Kuzaliwa Inakaribia siku mbili sijazo
- Simu Yake Inaharibika baadae yake kidogo [emoji16]
- Kodi Ya Nyumba Inaisha siku chache zijazo
- Mama Yake Anaumwa [emoji23]
Ukimaliza kutatua manne kati ya hayo au zote kwa pamoja muite aje geto sasa utamsikia "yaani tumbo linauma M'P haikati[emoji23]mpaka mm mwenyewe najishangaa, nngekuwa nimepata hela nngeenda kuangalia tatizo ninini my"[emoji13][emoji13]
Kama hadi unafikia Huku mwishoni na haujastuka tu basi wewe ni zaidi ya punjumbu [emoji23][emoji23]

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
@fredo fred yaani mwalimu wao ni yuleyule, wamekariri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom