Kama una ugonjwa unaokupa tabu maishani na unarithishwa fikiria kuhusu kuasili

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Nimetoka kucheki documentary ya magonjwa yanayorithika nimeona nije kuweka maoni,

Magonjwa ya kuruthi:
  • kifafa cha kurithi.
  • sickle cell.
  • CCHS ; tunavyopumua huwa hatufikirii kupumua, wenye ygonjwa huu inabidi wafikirie ili wapumue, wanapolala inabidi watumie mashine kuwasaidia.
  • Kansa ya mifupa, maumivu ni makali sana.
  • Magonjwa ya kiakili yanayorithishwa kama tay-sachs na Huntington's n.k.
Kama nina ugonjwa unaoweza kurithishwa kwa mtoto wangu, ni heri nisiwe na mtoto maana najua kabisa watapitia hali ambayo inanitesa, na hio ndio maana halisi ya kuwa na mapenzi kwa kizazi chako, naji sacrifice mwenyewe ili watoto wasije kuishi kwa taabu, sipo tayari kumuona mtoto akiteseka maksudi kabisa kwajili yangu.

wanadamu wanaojijua kabisa wana magonjwa mazito yanayorithishwa ila wanaamua kuwa na watoto wapo selfish sana kutaka wanachotaka bila kufikiria watu wengine (watoto wao).

Tukumbuke watoto sio kama mapambo tunayonunua sokoni tunakuja kuyahifadhi tu majumbani, watoto ni binadamu wanaokuwa na kuna muda ikifika inabidi wachangamane na jamii, wajitafutie ridhiki, n.k. changamoto za kiafya zinaweza kuwaathiri sana hapa.

- Unajijua una ugonjwa ambao mtoto wako atafanyiwa operation 14 kabla hajafikia miaka 20, unataka mtoto wa nini?

- Unajijua una ugonjwa ambao mtoto wako atakuwepo hospitalini muda mrefu na atageuka kuwa kama experiment kwa madaktari, unataka mtoto wa nini?

Kama una ugonjwa au ulemavu wa kurithi unaokutesa sana maishani jiamini usife moyo, lakini tafadhali usije kurithisha kwa mtoto; ni heri ufanye adoption ya watoto waliotekelezwa ama yatima.
 
binti huyu alikuwa na ugonjwa wa kurithi na alishaonywa na madaktari kwamba akizaa mtoto, ugonjwa wake utaenda kwa mtoto lakini yeye akaamua kupata mtoto,

sina shaka na mapenzi ya mama lakini linapokuja suala la dunia hii isiyo na huruma namuonea huruma mtoto ?

1673127673493.png

>> video <<
 
Kuna namna unaweza punguza uwezekano wa mwanao kulithi tatizo kama lako.

Akizaliwa usilale nae.
Kama ni tatizo la mama ake
Asimnyonyeshe.

Inaounguza uwezekano wa kulithi baadhi ya tabia hata magonjwa.
hayo mateso ndo hatuyataki mimi na mtoa mada.
 
binti huyu alikuwa na ugonjwa wa kurithi na alishaonywa na madaktari kwamba akizaa mtoto, ugonjwa wake utaenda kwa mtoto lakini yeye akaamua kupata mtoto,

sina shaka na mapenzi ya mama lakini linapokuja suala la dunia hii isiyo na huruma namuonea huruma mtoto ?

View attachment 2472508
Ubishi,sijui sifa? Hata kiuchumi pia...huna uwezo wa kulea au kusomesha watoto unazaa wa nn?

>> video <<
 
Hawatakusikia nakwambia ! Mtu na mkewe wana ukimwi but wanaendelea kuzaa, 5 years later wote wamefariki,watoto wanakua yatima... so selfish!
 
Nafkiri medical industry Kuna vitu inatakiwa kuviweka wazi hata Kama vina manufaa kwao Mana tafiti zinaibua vingi walivyotuaminisha kuhusu haya magonjwa.
 
Nimetoka kucheki documentary ya magonjwa yanayorithika nimeona nije kuweka maoni,

Magonjwa ya kuruthi:
  • kifafa cha kurithi.
  • sickle cell.
  • CCHS ; tunavyopumua huwa hatufikirii kupumua, wenye ygonjwa huu inabidi wafikirie ili wapumue, wanapolala inabidi watumie mashine kuwasaidia.
  • Kansa ya mifupa, maumivu ni makali sana.
  • Magonjwa ya kiakili yanayorithishwa kama tay-sachs na Huntington's n.k.
Kama nina ugonjwa unaoweza kurithishwa kwa mtoto wangu, ni heri nisiwe na mtoto maana najua kabisa watapitia hali ambayo inanitesa, na hio ndio maana halisi ya kuwa na mapenzi kwa kizazi chako, naji sacrifice mwenyewe ili watoto wasije kuishi kwa taabu, sipo tayari kumuona mtoto akiteseka maksudi kabisa kwajili yangu.

wanadamu wanaojijua kabisa wana magonjwa mazito yanayorithishwa ila wanaamua kuwa na watoto wapo selfish sana kutaka wanachotaka bila kufikiria watu wengine (watoto wao).

Tukumbuke watoto sio kama mapambo tunayonunua sokoni tunakuja kuyahifadhi tu majumbani, watoto ni binadamu wanaokuwa na kuna muda ikifika inabidi wachangamane na jamii, wajitafutie ridhiki, n.k. changamoto za kiafya zinaweza kuwaathiri sana hapa.

- Unajijua una ugonjwa ambao mtoto wako atafanyiwa operation 14 kabla hajafikia miaka 20, unataka mtoto wa nini?

- Unajijua una ugonjwa ambao mtoto wako atakuwepo hospitalini muda mrefu na atageuka kuwa kama experiment kwa madaktari, unataka mtoto wa nini?

Kama una ugonjwa au ulemavu wa kurithi unaokutesa sana maishani jiamini usife moyo, lakini tafadhali usije kurithisha kwa mtoto; ni heri ufanye adoption ya watoto waliotekelezwa ama yatima.
Imagine huyo unakwenda kumu adopt ana matatizo ya kurithi mengi kuliko ya kwako
 
Back
Top Bottom