Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kama wewe ni muajiriwa, na una watoto wanne nakuendelea, na unaishi mjini, fanya yafuatayo:-
- Tafuta chanzo kingine cha mapato, iwe biashara, udalali n.k
- Tafuta shamba ulime, au nunua chakula kwa wingi pale kinapokuwa kimeshuka bei na uweke stock, ili kuweza kupata chakula cha kutosha; haya mambo ya kwenda supermarket kuhemea kila siku, hayakufai tena
- Kama huna marupu rupu mengine, angalia namna ya kuwekeza mikoani/vijijini
- Usiendelee kukaa na kijana hapo mjini akiwa jobless huku akiwa na zaidi ya miaka 26
- Kama ulikuwa hujaweka kibanda, anza kupunguza vitu visivyokuwa vya muhimu, ufanye vitu vya msingi.
- Achana na mambo ya starehe kabisa
Asubuhi -kama utawapa chai nzuri, elfu 20 itakata
Mchana - kama umewapa chakula kizuri elfu 25 itakata
Usiku - Kama utawapa mlo mzuri elfu 25 itakata
Kwa siku utakuwa umetumia shilingi elfu 70, mara mwezi mmoja, utakuwa umetumia milioni 2 kwa chakula tu.
Wenzetu vijijini, wanaweza hayo kwa sababu, watawalisha viazi, makande n.k na vyote hivyo vinakuwa vimetoka shambani walipo lima.
Kwa leo ni hayo tu; njooni kwa mjadala.