Kama una zaidi ya watoto wanne, na unaishi mjini, kuna ushauri wenu hapa

Kama una zaidi ya watoto wanne, na unaishi mjini, kuna ushauri wenu hapa

Kama wewe ni muajiriwa, na una watoto wanne nakuendelea, na unaishi mjini, fanya yafuatayo:-​
  • Tafuta chanzo kingine cha mapato, iwe biashara, udalali n.k​
  • Tafuta shamba ulime, au nunua chakula kwa wingi pale kinapokuwa kimeshuka bei na uweke stock, ili kuweza kupata chakula cha kutosha; haya mambo ya kwenda supermarket kuhemea kila siku, hayakufai tena​
  • Kama huna marupu rupu mengine, angalia namna ya kuwekeza mikoani/vijijini​
  • Usiendelee kukaa na kijana hapo mjini akiwa jobless huku akiwa na zaidi ya miaka 26​
  • Kama ulikuwa hujaweka kibanda, anza kupunguza vitu visivyokuwa vya muhimu, ufanye vitu vya msingi.​
  • Achana na mambo ya starehe kabisa​
Kutokana na ukubwa wa familia, ni sawa na viwavi jeshi kuvamia gunia la mahindi -hela itakuwa haikai, inaingia kwa spidi ndogo, na kutoka kwa spidi kubwa.

Asubuhi -kama utawapa chai nzuri, elfu 20 itakata
Mchana - kama umewapa chakula kizuri elfu 25 itakata
Usiku - Kama utawapa mlo mzuri elfu 25 itakata

Kwa siku utakuwa umetumia shilingi elfu 70, mara mwezi mmoja, utakuwa umetumia milioni 2 kwa chakula tu.

Wenzetu vijijini, wanaweza hayo kwa sababu, watawalisha viazi, makande n.k na vyote hivyo vinakuwa vimetoka shambani walipo lima.

Kwa leo ni hayo tu; njooni kwa mjadala.
Kijana kama amemaliza elimu yeyote fukuza asikae nyumbani,ukiendekeza huruma utakuja kufukuzwa wewe..
 
Umeongea kitu kikubwa sana...maisha ya mjini kama huna vyanzo vya uhakika vya kipato ni bora kurudi kijijini kulima,una kuta familia watoto 5,na mtafutaji ni baba peke yake,anaondoka saa 10 kasoro usiku kurudi saa 4/5 usiku daily, hapo baba akilala chini familia lazima iyumbe.
 
Kuna wakati unakutana na mzee barabarani amepigwa na jua la utosi, huku akiongea mwenyewe; kumbe changamoto anatakiwa familia ipate mkate wa kila siku
Hatari unarudi home unakutana na stress kubabake 60 hutoboi
 
Wakiwa wengi, wanakuwa kama mifugo; asubuhi wale, mchana wale, usiku wale, matibabu, mavazi..na uwahudumie kwa miaka 30, na bado hawajaanza kuzalisha; na hata wakizalisha wanaweza wasikukumbuke
Ila hata wasipokukumbuka na wao karma lazima itambae nao na wao watazaa halafu watelekezwe
 
Kijana kama amemaliza elimu yeyote fukuza asikae nyumbani,ukiendekeza huruma utakuja kufukuzwa wewe..
Kwani walituma barua kuwa wanataka kuja duniani au ni nyegezi zako tuu,
Lazima watoto unazaa kwa miaka hii uwatengenezee mazingira ya kujiendeleza Otherwise ndiyo tunazalisha panya road na s
Dada poa wa kutosha
 
Back
Top Bottom