Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Nguruwe unatafuta maporini,vijijini,mashambani na unachinja daily.unatakiwa uchinjie machinjio ya kitimoto kama yapo ile ugongewe mihuri na mabwana afya,kazi yako inakuwa kusupply kwa wateja wako ambao ni mabucha,majiko ya wauzaji rejareja,na wanaonunua kilo nyingi kwa ku pre-order,unatakiwa uwe na kijana wa kusambaza kwa wahusika daily,Asubuhi ukiamka ni simu tu kwa wateja wako kuuliza wanahitaji kg ngapi?,hii kazi ukiacha hata siku moja unapoteza wateja wote,maana ni kazi ya 365 days.kazi ni kupata Nguruwe na kuna hasara pia.Mr nimechoka kuandika nafanya nshu nyingine saa hii
Asante kwa jibu zuri na linaloeleweka mkuu
 
Miezi miwili iliyopita nilikua najihusisha na biashara ya vipodozi vya usoni vya wanawake..nilikua natumia mtaji wa tsh 30000 kwa siku nilikua naweza kupata wateja si chini ya 5 hadi 6 na kila bidhaa nilikua nauza 30000.. kwahiyo nilikua napata hadi laki na nusu faida..ila tatizo ilikua inachosha Sana na nilivyopumzika ndiyo nikapumzika mazima.
Nawezaje kukupata...kuna jambo hapa
 
hv mawakala huwa mnakabiliana vp na hawa matapeli mfano mtu anakuja kudeposit pesa afu anakupa noti feki (unatumia njia gan kutambua noti feki)
na pia kuna wale matapeli wanakuja wanakutumia sms kiujanja kwamba wamewithdraw kumbe hamna ktu, pasipo kujua ww unawapa hela wanasepa badae kuangalia salio unakuta hamna ktu
noti feki ni simpo sana kuzitambua , ukiwa mzoefu na kazi hii ya kushika pesa automatically unazitambua. Ila pia kama una machine ya kuhesabia pesa zitakamatika . Mimi tangu naanza nimezikamata mara tatu na zipo ofisini nimezibandika kwa ajili ya wengine wazione.

Kuhusu matapeli mimi huwa nawapeleka wafanya kazi kupata semina kwa wakala mkuu. Huwa wanaelezwa mitego na mbinu za kukabiliana na matapeli
 
Achana navyo mkuu havina dili saivi

wengine tulichukua kujificha tu ila havina issue yyte

usipoteze hela yako kununua..

ila kama umedhamiria "nenda ofisi ya serikali yako ya mtaaa utavikuta vyakutosha"
Asante mkuu,
 
Nishawahi kufanya deep conversation na two most successful businessmen, mmoja ana sheri za Mafuta na maroli mwengne anamaduka ya hardware na anamaroli, pia nmetoka kuhitim elimu ya utawala biashara, hivo matumizi ya imani hayaingiliani kabisa na issue za location na changamoto zingne, in short uchawi kwenye business upo
Kama hadi msomi kama wewe unaamini imani za kishirikina,basi kama taifa tuna safari ndefu sana
 
Wajinga ndio waliwao...nenda kwa mganga kwenye nyumba yake ya nyasi huko vijijini ukampe kuku akupe utajiri uwe bilionea kama kina bakhresa
Hapa unaongelea wasomi kuamini kuwepo kwa uchawi au unaongelea wasomi ku-practice uchawi.

Uchawi upo, practice is an option. Huko kwenu hujawahi sikia watu wamerogwa na kufa? hata neno gamboshi hujawahi kulisikia au ndo huko kusema hutaki kuamini ukiwa online ila ukienda zako kitaa unafanya.
 
Back
Top Bottom