Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Mimi naingiza pesa hiyo, biashasha yangu ni duka bar, mchana nauza bidhaa za kawaida kama mchele, unga, sukari mafuta nk, strategy yangu ni bei ndogo, naagiza, mkoani nauza kwa bei ya chini kuliko washindani, pia nimeweka mpesa na mitandao mingine, upande wa bar kuna supu na vinywaji, usiku nauza ganja pia hii imepelekea ongezeko kubwa la wateja , nafikilia kununua kontena la 20ft ili nipate nafasi ya kutosha.
 
mkuu, inawezekana. Mimi pia nafanya hiyo business. mchawi ni location na usimamizi. kwenye goli nililoanzia uwakala tigopesa huwa napata hadi 700k+, m pesa 400k+ airtel 250k+, halopesa 80k+.

sometimes baadhi ya wateja wa miamala mikubwa nawakataa ili nispate usumbufu wa cash na flot
 
Nimesoma comment zote kikubwa nilichogundua ambacho inaweza kuwa ni changamoto ni hii kauli kuwa " wew mwenyewe ndo uwe unafanya hyo kazi" yaani isiwe umeajiri mtu. Sasa kwa wanaokaa maofisin na wanamtaji wao watafanyaje
 
Mkuu jitahidi upate na uwakala wa mabenk utatusua sana. Nmb wako na tofauti ndogo sana na tigo pesa.
 
Nimesoma comment zote kikubwa nilichogundua ambacho inaweza kuwa ni changamoto ni hii kauli kuwa " wew mwenyewe ndo uwe unafanya hyo kazi" yaani isiwe umeajiri mtu. Sasa kwa wanaokaa maofisin na wanamtaji wao watafanyaje
Hamna mkuu, Mimi binafsi sishindi kwenye ofisi zangu nina vijana sita ila nimeweka mfumo wa ufuatiliaji hakuna anaezijua ofisi zangu kuliko mimi mwenyewe.

Kuna changamoto ya vijana ambao wako competent na wenye moyo wa kazi. Kila unapoajiri wanne unaweza pata mmoja, huyo unamtunza baada ya muda utakuta ofisi zimefanikiwa kuwa na vijana wenye ujuzi na waadilifu. Ukiajiri bora mtu ili umlipe kidogo na wateja watakukimbia tu hamna namna utayumba.
 
Bodaboda wapi huko ikuingizie 30 kwa siku?. Sehemu nyingi naona wakipata sana 15
Unaonyesha unaongea kitu usicho na uzoefu nacho

unaongea stori za kuambiana huko...

nijibu hili swali then ndipo tuendelee na Ligi maana unaonyesha unataka ligi

mafuta ya 5000 yanaweza kukupa sh ngapi kwenye Boda boda??

Assume piki piki haina mafuta kabisa then mtu akaenda sheli akakuekea kwenye tank mafuta ya 5000

Niambie mpk yale mafuta yanaisha yatakupa sio chini ya sh ngapi????

Naomba jibu..
 
Hii uliifanyia eneo gani mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…