Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Fungua banda la chipsi kama la Zero IQ

usiuze chipsi kizungu uza chipsi kiswahili swahili

chipsi kavu 1000 chips mayai 2000

mteja akija na buku 1800 akakuomba umpe chips mayai kapungukiwa 200

usikatae chukua hela mtengenezee chipsi yai yake..

Hakikisha hupimi chipsi nyingi kachumbari ndio iwe nyingi chipsi kidogo tu

Mishkaki uza sh 300 usiuze mishkaki mibaya itengeneze vizuri ila usikate mikubwa

finyango za 300 zinajulikana...

Kwa siku utachezea faida 30k kwenda mbele siku zingine hutojua hela zimetoka wapi

kwa jinsi utavyokua ukihesabu mpk kujikuta umeingiza 80k(siku za kismati hizi wateja wakishakuelewa)
 
bIASHARA ZOTE HIZO uweke akilini kwamba

MWANZO NI MGUMU

itakubidi uwe mvumilivu kwa muda usiopungua siku 30 ambapo ni sawa na MWEZI 1

kuwapa wateja nafasi ya kujua unafanya nini so katika mwezi huu wa kwanza usitegemee faida

kama nilivyoandika ila tu uwe na uvumilivu,kuanzia mwezi wa pili utaona kwa vitendo yote niliyoandika.
 
Miezi miwili iliyopita nilikua najihusisha na biashara ya vipodozi vya usoni vya wanawake..nilikua natumia mtaji wa tsh 30000 kwa siku nilikua naweza kupata wateja si chini ya 5 hadi 6 na kila bidhaa nilikua nauza 30000.. kwahiyo nilikua napata hadi laki na nusu faida..ila tatizo ilikua inachosha Sana na nilivyopumzika ndiyo nikapumzika mazima.
Yani faida yote iyo uliwezaje kichoka na kuacha,
Natamani hata nije PM unielekeze hii biashara inafanyika vipi nianze kufanya hata kama nitachokaje nikiweza kuingiza faida iyo sitaacha
 
Nauza mkorogo 😂😂 vifaa vinanigarimu 50000 natoa kopo 10, kila kopo nauza 25000. Kwa siku naweza kuuza kopo mbili mpk nne. Wateja Facebook na Instagram. Na business nyingine ila hii ndio inanipa faida kubwa.
wakomeshe mama sura ziwameremete wawe kama makaratasi

waekee hiyo mikorogo wachanganyie na tindikali kwa mbaliiiii

tupate wenye sura kama migomba ya kule moshi
 
Nina mpango wa kufanya ivyo nikirudi tena kwenye hiyo biashara..ila hongera kwa kupambana dear.
yna2 we mama mfatilize tu Beef Lasagna anawapiga tu msasa kina dada na kina mama

na wewe unataka anza mtuongezee idadi wa wazungu hapa TANZANIA...

go mama pambaneni ikifka 2025 TANZANIA yote ni ma afri cast rangi za mitume
 
PTER,
Hii kitu imenifikirisha sana mkuu, nina ka plot Dar. pembeni ya mji, nimewaza idea ya kujenga room sita kwa kuanzia kama guest rooms afu mbele nitengeneze room mbili moja kaunta kwa ajili ya open grocery room nyingine kwa ajili ya jiko, hii imekaaje ?
 
Biashara zenye uwezekano wa kupata faida ya 30K kwa siku :

- Tengeneza mikokoteni au vitoroli vya chuma 10 Kisha uwe unakodisha (Eg: Tsh 4,000 kwa siku kila mmoja) hasa kwa vijana wanaobeba mizigo ya wateja karibu na Hardwares shops au wanapofyayua matofali.

hiii siri natamani wanawake wenye mitaji wasiojua cha kuifanyia waijue

nilimpa X wangu hiii biashara katika vitu ananiambiaga "kwanini hatokaa anisahau,ni kumpa hii biashara"

biashara moja ambayo haijulikani na katika watu wote wataochangia huu uzi na watakaotoka na mawazo ya kuyafanyia kazi

hamna ataechukua hili wazo,ila kwa mwenye mtaji wa 1M na haina kazi ajaribu tu then aone balaa lake

Mtaani Wananiita BOSS MATOROLI au BOSS MIKOKOTENI
 
Biashara yenye kuweza kukuingiza 30,000 per day ni nyingi
~ unawezq chagua biashara ya hesabu nafikiri hii ndio itakuwa nzuri na super (wale walio maofisini). Kwa hapa Dar es Salaam unaweza fungua banda la chips ukaomba hesabu yako, pili unaweza kodisha mkokoteni kama walivyosema wadau ,tatu unaweza toa ajira kwa vijana mfano, kuna hawa vijana wanao uza ndizi za kuchoma na kukuaanga wanapata faida nzuri, ukipata muda waweza ongea nao.

~pili unaweza chagua hesabu ya kuuza na kununua, mfano Dar es Salaam unaweza anza biashara ya kuuza maji juice ata kwa katoni 120 za brand ukauza kwa faida japokuwa ndogo ila zingatia mzunguko.

~unaweza uza ujuzi wowote ulio nao nao ni rahisi kupata faida iyo ya 30,000 mfano ufundi wa namna yoyote

..biashara yoyote inafaida kikubwa cha kuzingatia ni nidhamu ,ubunifu, uvimilivu na pia usimamizi ,usimwamini mtu kwa 100% ata kama ni mwanao.
 
Hii kitu imenifikirisha sana mkuu, nina ka plot Dar. pembeni ya mji, nimewaza idea ya kujenga room sita kwa kuanzia kama guest rooms afu mbele nitengeneze room mbili moja kaunta kwa ajili ya open grocery room nyingine kwa ajili ya jiko, hii imekaaje ?
Usiweke Glocery, Hako Ka Kaunta Nako Weka Chumba Kingine.
Kwa Siku Utapata Mpaka 30k Kwa Room Moja, Watu Wanalana Sana
Haswaa Guest Zilizo Nje Ya Mji.

Siongei Kwa Kubahatisha, Kabla Sijajiri Na Electronics Nilikuwa Nimepata Kazi Hii, Mimi Kibaka Nilikuwa Napata Mpaka 60k Per Day Wakat Huo Boss Hesabu Inasoma 150k Had 200k Guest Ilikuwa Mitaa Ya Airport Dar

Hapo Staff Room Weka Fridge Dogo Jaza Vinywaji Vya Kawaida, Jaza Condom Uza Buku

Mkuu Hautanisahau Kwa Hili.
 
Biashara nyngne inayolipa ni sales, nunua pikipiki yako then chukua Bidhaa kutoka kwenye maduka ya jumla zungusha mtaani, 30k faster tu, kama mtaji unaruhusu nunua kirikuu minimum profit apo 50k, ushawahi kujiuliza why hiz selling companies inakikirikuu tu na mtaji usiozidi 10m lakn wanamlipa salesperson 400k, wana HR, accountants,managers, madepartments kibao na wanawalipa handsomely, they pay bills kama rent kwa mamilion ya hela kwa hicho hicho kikirikuu?
Noted, thanks mkuu in advance kwa hii post yako.
 
Nimesoma comment zote kikubwa nilichogundua ambacho inaweza kuwa ni changamoto ni hii kauli kuwa " wew mwenyewe ndo uwe unafanya hyo kazi" yaani isiwe umeajiri mtu. Sasa kwa wanaokaa maofisin na wanamtaji wao watafanyaje
hapo ndipo penye changamoto haswaa

kama upo peke ako asee wakuweza pambania hela yako ni mkeo/mumeo

na awe kweli mna ndoto na malengo sawa...vinginevyo utatajirisha watu kwa pesa yako

yani pesa yako inawapa mtaji wengine then wanakuacha wanaenda fungua biashara zao.
 
Back
Top Bottom