Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa


Uncle nisaidie kufafanua maelezo yako ya mwanzo hapo kidgo
 
Inakuwa chini kuliko anayelala lakini inakupa wateja wengi na hawatumii huduma za msingi nyingi.
1 Mathalani mchana hawatatumia umeme sana kama usiku, maji pia ni hivyo hivyo

2 chumba kimoja kitasave watu zaidi ya mmoja kwa siku.

Wakati naanza mimi nilikuwa najidanganya sana kuwa watu wa kulala ndiyo nitatengeneza faida ila baada ya muda niligundua usiku hakukuwa na pesa kama mchana.

Mkuu PTER hiyo short time si inakuwa bei chini kuliko anayelala ama ileile?

Ningependa kujua kodi za serikali huwa kama kiasi gani kwa mwezi?
 

Biashara hii ni nzuri ..kutengeneza tent sijajua gharama zake ila ntaulizia ntakupa feedback mkuu
 
Ahsante boss
Nitaifanya
 
Inshallah,nataka nianze na 6 rooms pekee self ila mkoani.

Vipi kwa uzoefu wako kuna haja ya kuwa na vyumba vya hadhi tofauti tofauti?

Kodi vipi imekaaje?
 
Ahsante boss
Nitaifanya
jiamini maana hamna mwizi wa kukuibia TOROLI/MKOKOTENI wako

atauiba ataubebaje,ataenda uuza wapi? yani tengeneza yako 6 tu

itakukost kama 900k then laki iliyobaki kwenye ile 1M

nunulia MADUMU ya maji ya lita 20 madumu utapata 1 @ 5000

utanunua madumu 20 then ktk yale matoroli 6 chukua matoroli mawili

Yaweke madumu kila toroli liwe na madumu 8 then madumu yako ma 4 yawe reserve yatulize

ataetaka kukodisha toroli na madumu mpe bei yake na ataetaaka kodisha toroli bila madumu mpe bei yake

Kaa vuta kiti somewhere fanya biashara yyte ya kijinga hata ukikaa ndani ukfanya biashara ya online fresh

yani baada ya hapo ili usikae bure we tafuta cha kufanya simamia vitoroli vyako

DEAR MOTHER utanikumbuka siku 1
 
yna2 we mama mfatilize tu Beef Lasagna anawapiga tu msasa kina dada na kina mama

na wewe unataka anza mtuongezee idadi wa wazungu hapa TANZANIA...

go mama pambaneni ikifka 2025 TANZANIA yote ni ma afri cast rangi za mitume
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mimi nilishauzaga Sana mikorogo kitambo kidogo..Sasa hivi nimeingia kwenye losheni za matunda tu .
 
Nimefatilia comment zote sijaona hii biashara je ni kuwa watu hawaifahamu ama ina Changamoto nyingi?

Biashara yenyewe ni kutengeneza maandazi, then Una pack kwenye mifuko kama wafanyavyo Azam then Una supply madukani, but yako unaifanya kama mama ntilie WA kawaida but tofauti ni kuwa Una package kwenye mifuko

Mtaji ni almost 2M,, hapo unanunua mashine ya kuchanganya unga unaweza kuanza na mashine ndogo Ile inayo mix kilo 5 at once,,, ina cost 1.2M, pesa inayobaki ndiyo ya unga,, sukari,, mafuta na kuni kwa ajili ya kukaangia maandazi yako.

Hii ukiifanya kwa umakini kwa mfuko mmoja WA unga WA kilo 25 mathalani unaweza kuingiza mpaka 15k to 20k, ukiwa unatengeneza mifuko mitatu mpaka minne utaona faida kwa siku ni kiasi gani

Na maandazi yanatoka maana unaweza kuangalia Tu mtaani kwako ni akina mama wangapi wanatengeneza locally na maduka yako mangapi wanaochukua bidhaa kutoka kwa watu lakini mzigo unaisha

Kikubwa location na utofauti wa bidhaa na wengine,,. Asante
 
Siku hizi tigo pesa/mpesa na nyingine zote wanakata "withholding tax kabisa na kupeleka TRA kupitia Tin Number yako, sasa wewe potea tu lkn jua TRA watakusubiri tu mpaka utakapofika habari zako wanazo
nieleweshe baba labda sijakuelewa vizuri
 
proskaeur,
hivi umefatilia ukagundua kuwa siku hizi watu vitafunio wanapenda

vitu fresh from jikoni mfano mihogo/viazi/chapati/bagia/nk hayo maaandazi ya kulala watu hawanunui

waulize wauza maduka maandazi ya bakhressa yanavyokaa madukani.

sikushauri hiyo biashara watu siku hizi wameanza elewa makundi ya vyakula

Anapiga hesabu asubuhi ngaano,mchana ngano,usiku ngano Halafu tena mandazi viporo (utapata hasara mkuu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…