Kama unajitafuta, nenda kaishi wilaya ya Mbarali

Mbarali hii! Ukifika Kyela naona utachanganyikiwa, Kyela inazo fursa nyingi sana za kilimo cha korosho, michikichi, kokoa, mpunga, migomba, vanila, mahindi, minazi, uvuvi, ufugaji, parachichi na biashara ya mpakani na Malawi pia upande wa pili wa ziwa Nyasa yaani wilaya ya Nyasa.
Mbarali kilimo ni cha mpunga ni cha kugombania maji na eneo ni dogo wakulima wamebanana.
 
Chanika ya Kibaha, Chalinze ya Dodoma, Oysterbay ya Chunya, Ulaya ya Kilosa na Ulaya ya Nzega.
 
Unaizungumziaje Arusha?
Arusha ipo overated Sana , fursa za Arusha ni za mitaj mikubwa mikubwa. Hata kilimo tu Arusha Mashamba ni gharama Sana,. Madini nako wanufaika ni matajir , utalii vile vile

Arusha gharama za maisha ni kawaida Tu sio Kama watu wengi wavavyofata mkumbo kudai kuwa gharama NI juu Sana.

Maeneo mengi Kama Mbauda , Sanawari , Morombo , Sinoni maisha ni kawaida sana

Gharama za maisha naweza sema zipo juu Moshi kuliko Arusha
 
Mkuu kwenye kilimo fursa kubwa ni kilimo cha mpunga lakin si Sawa kusema Mbarali fursa ni hiyo tu .

Mbarali biashara zinatembea Sana . Hata hapo Rujewa biashara zinaenda Sana .
 
Mbarali kwenye upande wa biashara mzunguko bado uko chini kwa muda mwingi isipokuwa kwenye baadhi ya vipindi vya nsimu wa kilimo, mf wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.

Nimekaa madibira, ubaruku na chimala
Kama unataka biashara at least ubaruku mzunguko upo kwa muda mrefu.


 
Mkoa mwingine kujitafutia ni Tabora, gharama za maisha ziko chini, so unaweza pambana kwa unafuu zaidi.
Yes,nimekaa Tabora miaka 8 maisha yapo chini hapo Uyui,Urambo,gunia la mkaa 6000,mchele ukivunwa kg 1 1200,Nyama kg 1 7000 kwa sasa,zamani kidogo 5000,kuku wa kienyeji 8000 mtetea,Jogoo 10,000
 
Tukutane kona pub au vatican
 
Tatizo lako wewe mlafi. Hakuna fursa nyingine yeyote uliyoiongelea hapo zaidi ya mchele na mpunga. Unadhani kila mtu anawaza kula tu michele..?
 
Mkuu hivi heka moja kwa kawaida huwa unavuna kiasi gani cha mpunga?
Ardhi ya Kyela kwa mazao yote ni nzuri kutokana na maji yanayotiririka kutoka milimani, maji haya huleta rutuba badala ya kutegemea mbolea za chumvi, mchele wa Kyela huuzwa Malawi na Zambia kutokana na ukaribu kuzifikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…