Kama unajitafuta, nenda kaishi wilaya ya Mbarali

Kama unajitafuta, nenda kaishi wilaya ya Mbarali

Wakuu maisha ni kushare love.

Nataka niwaambie vijana na watafutaji wengine ikiwemo hata watumishi wa umma wenye mishahara midogo midogo.

Hakuna sehem Tanzania hii panafaa Kwa mtu anayejitafuta Kama Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Wilaya ya Mbarali ina fursa jumuishi nyingi Sana lakini kubwa zaidi ni kilimo na biashara.

Kuna watu pande za Ubaruku, Madibira , Kapunga n.k wanapiga Sana hela kwenye kilimo cha mpunga na biashara ya mchele.

Mbarali kbiashara pia kuna fursa sana, kwenye mchele na hata mazao mengine kuna fursa Sana.

Fursa ya usafirishaji nayo haipo nyuma maana Mbarali ni Wilaya ambayo ipo active Sana na usafiri ni wa uhakika.

Fursa NI nyingi Sana ,, wengine wataongezea. Kuna jamaa anaitwa Kaponda yupo KIJIJI Fulani kinaitwa Mswiswi Mwamba anafanya vizur Sana na anatajirika kweli kweli maana kamix biashara mbalimbali now ana Scania si Chini ya 10.
Mbarali hii! Ukifika Kyela naona utachanganyikiwa, Kyela inazo fursa nyingi sana za kilimo cha korosho, michikichi, kokoa, mpunga, migomba, vanila, mahindi, minazi, uvuvi, ufugaji, parachichi na biashara ya mpakani na Malawi pia upande wa pili wa ziwa Nyasa yaani wilaya ya Nyasa.
Mbarali kilimo ni cha mpunga ni cha kugombania maji na eneo ni dogo wakulima wamebanana.
 
Tusi gani mkuu , itakuwa umechanganya Tu mafile.

Mbaga Jr alitoa maoni kuwa hajawahi fika Mbarali lakin tena akasema amewah fika Mswiswi ndio nikashindwa kumuelewa maana ni Sawa na kusema hajawahi fika Dar Ila aliwahi ishi Chanika lazima uulize Chanika ya mkoa gan
Chanika ya Kibaha, Chalinze ya Dodoma, Oysterbay ya Chunya, Ulaya ya Kilosa na Ulaya ya Nzega.
 
Unaizungumziaje Arusha?
Arusha ipo overated Sana , fursa za Arusha ni za mitaj mikubwa mikubwa. Hata kilimo tu Arusha Mashamba ni gharama Sana,. Madini nako wanufaika ni matajir , utalii vile vile

Arusha gharama za maisha ni kawaida Tu sio Kama watu wengi wavavyofata mkumbo kudai kuwa gharama NI juu Sana.

Maeneo mengi Kama Mbauda , Sanawari , Morombo , Sinoni maisha ni kawaida sana

Gharama za maisha naweza sema zipo juu Moshi kuliko Arusha
 
Upatikanaji wa maeneo ya kulima ndio changamoto kubwa na ni bei sana. Kule Kwa mwekezaji watu wa kulima Kwa share ndo wanapewa mashamba makubwa. Mbarali hakuna shughuli nyingine ya kiuchumi Zaid ya kilimo Cha Mpunga na bustan za vitunguu pale igomelo Igawa. Nipo Rujewa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Mkuu kwenye kilimo fursa kubwa ni kilimo cha mpunga lakin si Sawa kusema Mbarali fursa ni hiyo tu .

Mbarali biashara zinatembea Sana . Hata hapo Rujewa biashara zinaenda Sana .
 
Mbarali kwenye upande wa biashara mzunguko bado uko chini kwa muda mwingi isipokuwa kwenye baadhi ya vipindi vya nsimu wa kilimo, mf wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna.

Nimekaa madibira, ubaruku na chimala
Kama unataka biashara at least ubaruku mzunguko upo kwa muda mrefu.


 
Mkoa mwingine kujitafutia ni Tabora, gharama za maisha ziko chini, so unaweza pambana kwa unafuu zaidi.
Yes,nimekaa Tabora miaka 8 maisha yapo chini hapo Uyui,Urambo,gunia la mkaa 6000,mchele ukivunwa kg 1 1200,Nyama kg 1 7000 kwa sasa,zamani kidogo 5000,kuku wa kienyeji 8000 mtetea,Jogoo 10,000
 
Upatikanaji wa maeneo ya kulima ndio changamoto kubwa na ni bei sana. Kule Kwa mwekezaji watu wa kulima Kwa share ndo wanapewa mashamba makubwa. Mbarali hakuna shughuli nyingine ya kiuchumi Zaid ya kilimo Cha Mpunga na bustan za vitunguu pale igomelo Igawa. Nipo Rujewa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Tukutane kona pub au vatican
 
Tatizo lako wewe mlafi. Hakuna fursa nyingine yeyote uliyoiongelea hapo zaidi ya mchele na mpunga. Unadhani kila mtu anawaza kula tu michele..?
 
Mkuu hivi heka moja kwa kawaida huwa unavuna kiasi gani cha mpunga?
Ardhi ya Kyela kwa mazao yote ni nzuri kutokana na maji yanayotiririka kutoka milimani, maji haya huleta rutuba badala ya kutegemea mbolea za chumvi, mchele wa Kyela huuzwa Malawi na Zambia kutokana na ukaribu kuzifikia.
 
Back
Top Bottom