Kama unakasirika sababu ya jambo moja kati ya haya fahamu wewe ni Mpumbavu kabisa

Naona Walevi wamepigwa spana mara 2+
 
Hahaa, soma kwa makini, mkuu. Hiyo ya kwanza ni WEVI(WEZI/WAIBAJI/THIEVES)
Sawa Mama Mtumishi emu nipe Neno la leo linasemaje leo Jumatatu yangu nataka iwe na upako nikutunukie na taji la uzima km zawadi
 
Katika mijadala na malumbano ya hoja hapa JF, kuna watu wengi waliojaa hasira vifuani mwao. Wanakasirishwa na maneno au vitendo vidogo vinavyoweza kuepukika...
 
Katika mijadala na malumbano ya hoja hapa JF, kuna watu wengi waliojaa hasira vifuani mwao. Wanakasirishwa na maneno au vitendo vidogo vinavyoweza kuepukika...
Yeap
 
Hiyo mental frame work mmekaa jopo la watu wangapia mkakubaliana kuwa iwe ivyo?
Ama umeamka tu unajisikia uandike hisia zako mkuu. Tupe research na ni wapi tafiti zilifanyika zikahitimisha ivyo
 
Sawa Mama Mtumishi emu nipe Neno la leo linasemaje leo Jumatatu yangu nataka iwe na upako nikutunukie na taji la uzima km zawadi
Neno la leo ntakupa, ila tambua kuwa atakayetoa taji ya uzima ni BWANA peke yake(2 Timotheo 4:8).

Kabla ya Neno, tafadhali omba (kwa kufuatisha kwa moyo wako wa dhati) sala hii ya toba. Omba hivi:

“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mkosaji, nimekutenda dhambi nyingi sana. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu Kristo karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Anza pia kwenda katika Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kukua kiroho.

Nakuachia sasa Neno la leo lenye upako:

“Bwana atakutangulia, Yeye atakuwa pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha; usiogope, wala usifadhaike."
Kumbukumbu la Torati 31:8
 
Pasipo msaada wake BWANA sisi hatuwezi kufanya lolote linalompendeza Mungu.
(Yohana 15:5)
 
Ahsante Mama MTUMISHI, naomba namba nichangie Sadaka ya Neno km hutojali
 
Napenda uniongoze maombi ya usiku Mama Mtumishi
Huu ni mfano(mwongozo tu) wa jinsi unavyoweza kuomba asubuhi, mchana au usiku:

"Baba wa Mbinguni, kwanza nakushukuru kwa kuniokoa na kuniahidi kuwa nikiomba lolote utanipa. Nakuja mbele zako sasa kwa unyenyekevu nikiwa na hitaji langu hili(taja hitaji lako). Ninaamini kuwa Wewe Mungu una uwezo wa kunisaidia au kuniongoza katika njia sahihi. Naamini utanipa kama ulivyoahidi. Napokea kwa imani majibu ya hitaji hili.

Katika jina la Yesu Kristo, Amina."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…