Kama unasafiri kuja Arusha ujipange hali ya hewa ni mbaya sana

Kama unasafiri kuja Arusha ujipange hali ya hewa ni mbaya sana

Nilikuwa naambiwa arusha baridi kali....ila nilipoenda, ni baridi ya kawaida tu. Hakuna maajabu.
Hii miaka minne mitano baridi imepungua nafikiri mabadiliko ya tabia nchi. Lakini miaka ya nyuma ilikuwa balaa buluu
 
Mtoa mada ushawahi kufika japo hata cape town south África?usingesema Tanzania kuna baridi!!ushawahi kukutana na maximum nyuzi joto 5?
Its all relative sasa wanaoishi Oymyakon wasemeje ?, inagonga mpaka -60 centrigrade

Point yangu ni kwamba kama umezoea baridi huwezi kuita baridi ya kawaida joto (yaani ukawa unatoa jasho)
 
Mimi chuga na njombe kote nimefika...chuga ikasome...sasa kuna Mufindi! Miez ya 6 had oct hakufai
Huko watoto WA shule ya msingi wanaambiwa wasije shule mpaka kupambazuke vizuri. Saa nyingine Hadi saa 3 asubuhi bado kumefunga, ukungu hivyo ni hatari kuvuka kwenye mabarabara hasa Barabara kuu (highway).
 
Njombe kata ya Lupembe ni balaaa kubwa mwaka juzi nilikuwa huko kuuza maziwa kwenye kiwanda Cha chai duuu hapafai
Unauzaje maziwa mkuu? Au ulikua una ngombe? Biashara ya maziwa nimejifunzia kwenye hivyo viwanda since kabinti kadogooo! Hahaa factories zote wanachukua bill..lol..those days
 
Huko watoto WA shule ya msingi wanaambiwa wasije shule mpaka kupambazuke vizuri. Saa nyingine Hadi saa 3 asubuhi bado kumefunga, ukungu hivyo ni hatari kuvuka kwenye mabarabara hasa Barabara kuu (highway).
Acha kbs nashangaa sikuwahi fikiria kuwa mtoro..leo hii ningepelekwa huko kusoma ningekua mtoro ajabu
 
Sisi wa Lushoto acha tukae kimya maana sijui mnachoongea wakati asubuhi barafu ilikua juu ya bati letu. Pale mto mgwiashighi upande huu wa kandeekampaa barafu imetawala wiki Sasa.
Kweli Bora mnyamaze 😂😂. Dar kuna vijitu vimeanza kuvaa masweta, vinachekesha!.
 
Ingekuwa unachapwa mboko vibaya yaan, na shule za enzi zetu mwalimu kukutia mtama ni Jambo la kawaida tu☹️, sio mitoto ya siku hizi inamdekea hadi mwalimu
Kama lile la juzi shule ya kiislam lililocharazwa mgongoni .nilipata hasira balaa mitoto imedeka had kero ..enzi zetu tulipigika ..
 
Dah umenikumbusha mbali sana, makete balaaa, sidhani kama kuna wilaya ina baridi kama hiyo.
Yan asubuhi barafu zimetanda kwa pahala, guest karibu zote zina. Majiko ya mikaa kwa ajili ya wageni kuota moto
Blanket inapiga kazi miaka miwili bila kuona maji chawa si chawa wale
 
Kabla ya uharibifu wa mazingira miaka ya 70 kulikuwa na barafu inamwagika kwenye majani asubuhi ilikuwa unakuta majani kama yamemwagiwa unga
Na saa4 yanakuwa na rangi ya blown..yameugua...chai inaungua,majani ya viazi mviringo yanaungua .jaman dah
 
Back
Top Bottom